read

Aya 103 – 106: Chukua Sadaka Katika Mali Zao

Maana

Chukua sadaka katika mali zao uwasafishe na uwatakase kwayo.

Wameafikiana kuwa dhamir katika ‘kwayo’ ni ya sadaka, na wakahitalifiana katika dhamir ya mali zao. Ikasemwa kuwa inawarudia wale waliochanganya amali njema na mbaya Ikasemwa kuwa inawarudia matajiri wote kwa sababu Aya imeshuka katika zaka ya wajibu. Kauli hii iko karibu na maana.

Kwa hiyo maana yatakuwa ni chukua ewe Mtume! Zaka katika mali za matajiri, kwani zinawatakasa na ubakhili kwa haki ya Mwenyezi Mungu. Tumezungumzia zaka katika kufasiri Aya 60 ya Sura hii, na Juz. 3 (2: 274)

Na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao.

Yaani muombee baraka na maghufira mwenye kutoa zaka, kwani hupata furaha na raha ya nafsi kwa dua yao.

Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.

Anasikia na ataitikia maombi yako kwa watoaji zaka, na anajua nia ya anayetoa zaka kwa roho safi, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayekubali toba ya waja wake na kuzipokea sadaka?

Mfumo unaashiria kwamba toba imetajwa hapa kwa kuashiria kuwa mwenye kuzuia zaka, kisha akatubia na akaitoa, basi Mwenyezi Mungu ataikubali toba yake na kupokea sadaka yake. Maana ya kukubali ni kwamba Mweneyezi Mungu, ambaye limetukuka neno lake atailipa thawabu. Kuna Hadith isemayo: “Hakika sadaka inaingia mkononi mwa Mwingi wa rehema kabla ya kuingia katika mkono wa mwombaji.” Mkono wa Mwingi wa rehema ni fumbo la kukubali.

Na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu?

Yaani anakubali toba na kuwarehemu wenye kutubia.

Na sema: Tendeni vitendo Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wataviona vitendo vyenu.

Katika kitabu Futuhatul-Makkiyaa J4, ameitaja Muhyiddin bin Al-arabi, Aya hii na kuifafanua kuwa maana ya kuona yanatofautiana kulingana na mwonaji. Kwa hiyo maana ya kuona kwa Mwenyezi Mungu ni kukijua kitu kwa pande zake zote. Maana yake kwa Mtume (s.a.w.) ni kujua kitu kwa njia ya wahyi uliomshukia. Maana yake kwa na mumin mwenye maarifa, ni kujua kwa kadiri ya alivyojua na kufahamu kutokana na wahyi ulioteremshiwa Mtume (s.a.w.).

Kwa hiyo basi, mwenye kufanya amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu anajua hakika ya amali yake na kuiridhia; Mtume naye anajua kuwa amali hii imeridhiwa kwa Mwenyezi Mungu, na mumin pia anajua kuwa ni mwenye kuridhiwa na Mtume. Natija ya mwisho ni kuwa mwenye kufanya amali njema anaridhiwa na Mwenyezi Mungu, Mtume na waumini.
Na wengine wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu, ama atawaadhibu au awakubalie toba.

Katika Aya ya 100 na inayofuatia, Mwenyezi Mungu (s.w.t.), ametaja aina nne ya watu: Waliotangulia kuhama na waliotangulia kusaidia, waliowa- fuatia hao kwa wema, wanafiki na wenye kukiri dhambi zao.

Katika Aya hii ameashiria watu ambao hakuwapa sifa maalum, kama alivyofanya kwa aina hizo nne, wala hakuweka wazi hukumu yao; isipokuwa amesema kuwa wao wanangojea adhabu ya Mwenyezi Mungu au msamaha wake; yaani jambo lao liko Kwake Yeye Peke Yake, amewaficha. Huenda hekima ya hivi ni kuwa wawe baina ya kuhofia na kutarajia, wasiwe na tamaa wala kukata tamaa.

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Ni Mjuzi, wa yanayowafaa hawa na wengineo, na ni mwenye hekima kati- ka kufanya wangojee hukumu yao na katika kila analolifanya.

Wafasiri wengi wanasema kuwa Aya hii iliwashukia jamaa katika waislam waliobaki nyuma katika vita vya Tabuk, kisha wakajuta.

Lakini Aya 118, imeeleza kuwa masahaba watatu walibaki nyuma katika vita ya Tabuk, kisha wakatubia na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatakabalia toba yao na akatangaza kukubali kwake, wala hakuwacha baina ya kuhofia na kukata tamaa.

Haya ndiyo yaliyotudhihirikia katiaka kufasiri Aya hii tuliyo nayo; hatujui tutapata maana gani tutakapofikia Aya hiyo ya 118. Tuonane huko.

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِمَنْ حَارَبَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ مِنْ قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ {107}Na wale waliotengeza msikiti kwa ajili ya kudhuru na


ukafir


i


n


a


kuwafarikisha


W


aumin


i


n


a


mahal


i


pa


kuvizia kwa yule aliyempiga


vit


a


Mwenyez


i


Mung


u


na


Mtume hapo kabla. Na bila


shak


a


wataap


a


kwamba


hutakukusudia ila wema; na


Mwenyez


i


Mungu


anashuhudia kuwa wao ni waongo.

لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَنْ تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَنْ يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ {108}


Usisimam


ehum


o


kabisa.Msikit


i


uliojengw


a


ju


u


ya


msingi wa takua tangu siku ya mwanzo, unastahiki zaidi weweusimamehumo.Humo mna watu wanopenda kuji


takasa


;


n


a


Mwenyezi


Mungu anawapenda wanaojitakasa.

أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَمْ مَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ {109}


Je


,aliyewek


amsing


iwa


jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi (zake) ni bora au aliyeweka


msing


i


jeng


o


lak


e


ju


u


ya uking


o


w


a


shim


o


linalomomonyoka


,


na


likamomonyoka likaanguka pamojanayekatikamotowa


Jahannam


u


n


a


Mwenyezi Mung


u


hawaongoz


i


watu


madhalimu.

لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَنْ تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ {110}


Jengolaohilowalilolijenga litaendelea kuwa ni sababu ya kutiwa wasiwasi nyoyoni mwao, isipokuwa nyoyo zao


zikikatikakatika


.


Na


Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenyehekima.