read

Aya 107 –110: Msikiti Wa Madhara

Maana

Aya zilizotangulia zimeonyesha aina mbali mbali za unafiki wa wanafiki. Aya hii inaonyesha aina nyingine ya unafiki wao na hila yao.

Jamaa fulani katika wanafiki wa Madina waliona njia nzuri ya kuufanyia vitimbi Uislam na Mtume wake Muhammad (s.a.w.) ni kujenga msikiti chini ya sitara ya kujumuika kumwabudu Mwenyezi Mungu na kunadi kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nyuma ya nembo hii watakuwa wamemkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kuudhuru Uislamu na waislam na kuwagawanya.

Naam walijenga msikiti huu vizuri sana na kuutolea mapesa. Baada ya kuukamilisha walimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu wakamwambia: Nyumba zetu ziko mbali na msikiti wako inakuwa vigumu kwetu kuhudhuria na tunachukia kuswali swala isiyokuwa ya Jamaa; nasi tumejenga msikiti kwa lengo hili na kwa ajili ya wanyonge na vilema. Kama utaswali humo basi itakuwa ni vizuri na tutabaruku kuswali mahali utakaposwali.

Hivi ndivyo walivyo wanafiki na wahaini kila wakati, wanabeba nembo za kutengeneza kumbe wanataka kubomoa. Lakini mara moja inafichuka aibu yao na kufedheheka mbele ya watu wote; kama walivyofedheheka wenye msikiti wa madhara, pale Mwenyezi Mungu alipomfahamisha Mtume wake hakika yao, kwa kusema:

Na wapo waliotengeza msikiti kwa ajili ya kudhuru na ukafiri na kuwafarikisha waumini na mahali pa kuvizia kwa yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume hapo kabla.

Aya tukufu inasema kuwa waliojenga msikit wa madhara wana malengo manne:

1. Kuwadhuru waislamu.

2. Kumkufuru Mwenyezi Mungu na kumtia ila Mtume wake.

3. Kuwagawanya waislamu na kuwaweka mbali na Mtume wa Mwenyezi Mungu.

4. Kuufanya msikiti ni maficho ya yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani.

Wameafikiana wafasiri na waandishi wa sera ya Mtume kwamba makusudio ya adui aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni mtu mmoja katika Khazraji anyeitwa Abu Amir Arrahib.1

Alikuwa ameingia ukiristo, mwenye cheo katika watu wake. Mtume (s.a.w.) alipofika Madina alipambana kiuadui na mlanifu huyu ambaye Mtume alikuwa akimwita fasiki.

Alipoona Mtume anazidi kupata nguvu, alikimbilia Makka kuwachochea Maquraish dhidi ya Mtume. Baada ya ushindi wa Makka alikimbilia Taif.

Watu wa Taif waliposilimu alikimbilia Sham. Huko aliwaandikia wafuasi wake wamjengee msikiti kwa sababu yeye atakuja na jeshi la Kaizari kumpiga vita Muhammad (s.a.w.).

Iliposhuka Aya hii, Mtume (s.a.w.) akiwambia baadhi ya masahaba zake: “Nendeni kwenye msikiti huu wa watu madhalimu muuvunje.”

Wakafanya hivyo na Mtume (s.a.w.) akaamrisha pale mahali pawe ni jaa. Baadhi ya mapokezi yameelezea kufananishwa msikiti wa madhara na ndama aliyeabudiwa na Waisrail na Musa akiwa hai. Kama ambavyo Nabii Musa aliamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kumvunjavunja ndama, vile vile Mtume aliamrishwa auvunje mskiti wa madhara.

Na, msikiti wowote, taasisi au klabu yoyote inayoundwa kwa sababu ya njama dhidi ya waumini basi hiyo ni ndama wa waisrail na ni msiki wa madhara, ni wajibu kuuvunja na kuufanya jaa.

Tangu yalipopatikana mafuta katika miji ya Kiarabu, mashirika ya nje ya kusimamia mafuta yalikuja na maamia ya misikiti ya madhara kwa sura mbali mbali. Miongoni mwa sura hizo ni kama hizi zifuatazo: Ile iliyobandikwa jina la sehemu ya kuabudia au vyuo, yenye jina la ofisi kuu au taasisi za kidini na yenye majina ya maendeleo ya kijamii au vilabu vya michezo.

Mingine ni ile iliyojitokeza kwa sura ya kitab, gazeti au mhadhara unao tangazwa kwenye idhaa kwa jina la dini au la nchi na mengineyo mengi ambayo dhahiri yake ni rehema na ndani yake ni adhabu. Yote hayo lengo lake ni kuharibu dini na nchi.

Tumezungumzia kuhusu nembo za kidini katika Juz 4 (3:142)

Na bila shaka wataapa kwamba hutakukusudia ila wema; na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.

Yaani hawa wanafiki waliapa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kwamba lengo la kujenga msikiti huu ni ibada tu na manufaa kwa waislamu; na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wao hawakujenga msikiti ila kwa kutaka kuwadhuru waislamu, kumkufuru Mwenyezi Mungu, kuwatenganisha Waumini na maficho ya anayempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Usisimame humo kabisa.

Maneno anaambiwa Mtume, lakini makatazo ni kwa wote; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ{78}


“SimamishaSwalajualinapopenduka.”(17:78)

Wafasiri wamesema kuwa makusudio ya usisimame, hapa, ni usiswali. Lakini kwa dhahiri hapa, kusimama ni ujumla, kunachanganya swala na mengineyo.

Kwa vyovyote ilivyo, kauli yake Mwenyezi Mungu usisimame humo kabisa ni dalili mkataa ya kutosihi swala katika msikiti uliojengwa kuwadhuru waislamu na kuwatenganisha na kwamba mwenye kuswali humo, basi swala yake ni batil, ni lazima airudie mahali pengine. Kwa sababu ukatazo katika ibada unafahamisha kuharibika.

Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa takua tangu siku ya mwanzo, unastahiki zaidi wewe usimame humo.

Imesemekana kuwa makusudio ni msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kwa sababu ndio uliojengwa siku ya kwanza Madina. Na ikasemekana kuwa ni Msikiti Quba ambao waliujenga Bani Amr bin Auf. Kwa dhahiri ni kwamba makusudio ni kila msikiti uliojengwa kwa ajili ya kumcha mungu. Kwa sababu neno Msikiti limekuja kiujumla (nak`ra).

Na kauli yake: Tangu siku ya mwanzo,’ maana yake ni kuwa umejengwa kwa lengo la uislamu tangu siku ya kuanza kujengwa kwake. Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Unastahiki zaidi,’ maana yake ni kwa uhakika, na wala sio kuwa huu ni bora zaidi kuliko wa madhara. Kwa sababu msikiti wa Madhara sio bora hata kidogo na haifai kuswali ndani yake kwa vyovyote vile.

Humo mna watu wanopenda kujitakasa; na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.
Yaani, msikiti huu ambao umeasisiwa kwa msingi wa takua, wenye ikhlasi wanaukusudia kwa swala na ibada ya Mwenyezi Mungu tu, si kwa unafiki na njama dhidi ya uislamu na Mtume; kama walivyofanya wenye msikiti wa madhara.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameleta ibara ya swala hapa kwa neno kuji- takasa, kwa sababu swala inamtakasa mtu na madhambi. Kuna Hadith isemayo: “Hakika swala ni kama mto unaopita, mwenye kuoga humo mara tano kila siku hatabakiwa na uchafu; vile vile mwenye kuswali mara tano kila siku hatabakiwa na dhambi.

Haya ndiyo tuliyoyafahamu katika Aya hii, pamoja na kukiri kuwa hakuna mfasiri yeyote aliyefasiri kutakata kwa maana ya swala, kama tunavyojua; na kwamba wengi wao wamefasiri kwa maana ya kutakasa uchafu kwa maji.

Je, aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi (zake) ni bora au aliyeweka msingi jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalomomonyoka, na likamomonyoka likaanguka pamoja naye katika moto wa Jahannamu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

Makusudio ya Aya ni kutofautisha baina ya msikiti wa Takua na msikiti wa madhara. Kwani wa madhara hauna uthabiti na unaweza ukaanguka kwenye moto mara moja; sawa na ambaye amejenga ukingoni mwa mto au kwenye mto. Ama jengo la msikiti wa takua ni thabiti lenye msingi imara usiotingishwa na chochote; na watu wake wako katika amani. Aya hii ni mfano wa Aya isemayo:

لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۚ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ {20}“Hawalinganisawawatuwamotoninawatuwapeponi.


W


atuwapeponi ndiowenyekufuzu”(59:20).

La kushangaza ni kauli ya baadhi ya wafasiri kwamba kauli ya ‘moto wa Jahanamu’ ni ishara ya yaliyotukia duniani kuwa moto ulitoka kwenye mskiti wa madhara na moshi wake ukabakia hadi zama za Abu jafar Al-Mansuru.

Jengo lao hilo walilolijenga litaendelea kuwa ni sababu ya kutiwa wasiwasi nyoyoni mwao, isipokuwa nyoyo zao zikikatikakatika. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Makusudio ya wasiwasi hapa, ni kwamba wanafiki hawakuamini utume wa Muhammad (s.a.w.). Kukatika nyoyo ni fumbo la kufa. Maana ni kuwa wao walijenga msikiti wakiwa na shaka bila ya kumwamini Muhammad (swa). watabaki na shaka hiyo hadi kufa.

إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُمْ بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ {111}


Hakik


a


Mwenyez


i


Mungu amenunu


a


kw


a


W


aumini


nafsi zao na mali zao kwambawaowapatePepo,wanapi


gan


a


katik


a


nji


a


ya


Mwenyezi Mungu, kwa hiyo wanaua na kuuawa. Ni ahadi


aliyojilazimish


a


kw


a


haki katik


a


T


awra


t


n


a


Inji


l


na Qu


r


’ani


.


N


a


n


i


nani atekelezay


e


zaid


i


ahadi kulik


o


Mwenyez


i


Mungu?


Basi furahini kwa biashara


yen


u


mliofany


a


naye


.


Na


hukondikokufuzukukubwa.

التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّهِ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ {112}


W


anaotubia, wanaoabudu wanaohangaika,


wanaorukuu


,


wanaosujudu,


wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu na wanaohifadhi mipakaya MwenyeziMungu.Nawape bisharaW


aumini

  • 1. Fasiki huyu alikuwa na mtoto aitwaye Hantwala ambaye ni katika maswahaba watukufu, aliyekuwa na ikhlas zaidi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume. Aliuawa katika vita vya Uhud akiwa na janaba akaoshwa na malaika. Ndipo akaitwa muoshwa na malaika.