read

Aya 11 – 14: Lau Mweneyezi Mungu Angeliwaharakishia Shari

Maana

Lau Mwenyezi Mungu angeliwaharakishia watu shari, kama wanavyoharakishia heri, hakika wangelikwishatimiziwa muda wao.

Makusudio ya heri hapa ni yale yanayowanufaisha watu katika maisha haya. Kwa ajili hii ndio wanaiharakia wala hawana subira nayo. Makusudio ya shari ni yale wanavyodhurika nayo; huyakataa na kuyaachukia kwa maumbile yao; ila kukiwa na sababu; kama vile kuondoa ambayo ni shari zaidi. Mshairi anasema: Navumilia shari kuhofia shari Shari nyingine ni shari kuliko shari.

Au pengine mtu akiwa katika hali isiyo ya kawaida; kama vile mtu anayetaka kujinyonga. Au kuwa katika hali ya inadi ya kumkabili hasimu aliyemshinda kwa hoja; kama vile walivyoshindwa washirikina kumjibu Muhammad (s.a.w.) wakati Mwenyezi Mungu alipodhihirisha miujiza mikononi mwake wakasema:

“Ewe Mungu! Ikiwa (anayoyasema Muhammad) ni haki, basi tuteremshie mvua ya mawe au tuletee adhabu iumizayo.” Juz. 8 (8:32)

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimjibu kila anayeharakisha adhabu na shari kwamba hekima ina inapitisha kutomkubalia matakwa yake mpaka wakati mwingine. Pengine linaweza kutokea jambo jengine la heri baada yake; kama ilivyotokea kwa wengi waliosema: Tuteremshie mvua ya mawe. Kuna kundi katika wao walisilimu na wengine wakazaa waumini wengi. Kama Mwenyezi Mungu angehiharakisha muda wao kusingelitokea kitu.

Kwa ufupi ni kwamba wao waliharakisha shari, sawa na wanavyoharak- isha heri, lakini Mungu (s.w.t.) aliwachelewesha mpaka alipowatakia heri.

Basi tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotevu wao.

Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu haharikishi adhabu kwa yule asiyeamini kufufuliwa katika wale waliomkufuru Muhammad, bali anaachana nao; hata kama wameasi amri yake na kuendelea katika uasi.

Na dhara inapomgusa mtu hutuomba naye ameegesha ubavu wake au katika hali ya kukaa, au katika hali ya kusimama.

Kuegesha ubavu, kukaa na kusimama ni fumbo la unyenyekevu wake kati- ka hali zake zote harakati zake na kutulia kwake.

Maana ni kuwa lau inamshukia chembe ya shari aliyoiharakisha, atakosa subira na atahangaika na kutukimbilia kwa unyenyekevu kwa kujidhalilisha katika hali zake zote ili tumuondolee.

Lakini tunapomwondolea dhara yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondolee dhara iliyomgusa.

Hali mbaya inaweza kumlazimisha mtu kusema uwongo, ria na kujipendekeza kwa mtu aliye na haja naye. Lakini ni jambo gani linalomlazimisha mtu kuasi, kukana jambo zuri na kumkana ambaye jana alikuwa akimyenyekea amtekelezee haja yake? Na alipompatia tu haja yake akamsahau kwamba hakumwomba kitu?

Hakuna tafsiri nyingine ya hilo zaidi ya kutojali, kuikana haki na misimamo na kupetuka mipaka katika hayo.

Namna hii wamepambiwa wapetukao mipaka yake waliyokuwa wakiyatenda.

Waliopambiwa vitendo vibaya ni wale wasiojali chochote ila manufaa yao na tamaa zao.

Hakika tumekwishaziangamiza kaumu za kabla yenu walipodhulumu; na waliwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini. Namna hii tunawalipa watu wakosefu.

Hili ni onyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wale waliomkadhibisha Muhammad (s.a.w.) kwamba nao itawafika adhabu kama iliyowafikia waliokua kabla yao walipowakadhibisha Mitume yao. Umepita mfano wa Aya hii katika Juz.7 (6:6).

Kisha tukawafanya nyinyi ndio mnaowafuatia baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyotenda.

Umma unaondoka na kufuatiwa na mwingine. Ama lengo la kuweko mtu katika ardhi hii ni elimu na amali ya kunufaisha. Utauliza kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ {56}


“Sikuumba



majini



na



watu



ila



waniabudu”



(51:56).

Na wewe unasema kuwa Mwenyezi Mungu amemuumba mtu kwa elimu ya manufaa.

Jibu: Makusudio ya ibada iliyotajwa ni amali njema kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ ۚ {10}


“Na



amali



njema



huiinua



…”



(35:10)

Bali Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameumba ulimwengu pamoja na ardhi yake na mbingu yake kwa ajili ya amali njema. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ {7}



Y


eye



ndiye



aliyeziumba



mbingu



na



ardhi



katika



siku



sita



na Arshi



yake ilikuwa juu ya maji, ili awajaribu ajulikane ninani miongoni mwenu ni mzuri



zaidi



wa



vitendo”



(


1


1:7).

Tumebanisha maana ya kujaribiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika Juz.7 (5:94)

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ ۙ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِنْ تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۖ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ {15}


Na



wanaposomewa



A


ya



zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana



nasi



husema:



“Lete


Qu


r


’an


i


isiyokuw


a


hii


,


au ibadilishe


.


Sema


:


Haifai


mimi kubadilisha kwa hiyari


y


a


nafs


i


yangu


;


sifuat


i


ila


niliyopew


a


wahyi


.


Hakika


mim


i


naogopa


,


nikimwasi


Mola wangu, adhabu ya siku iliyo



kuu.”

قُلْ لَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُمْ بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِنْ قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ {16}


Sema: lau



Mwenyezi



Mungu


angelitak


a


nisingeliwasomea


hiy


o


wal


a


nisingeliwajuza.


Nimekaa kwenu umri kabla yake,



basi



hamtii



akili.

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ {17}


Bas


i


n


i


nan


i


aliy


e


dhalimu


zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au


akadhibishay


e


A


y


a



zake?


Hakika



hawafaulu



wakosefu.