read

Aya 111 – 112: Mungu Huuza Na Kununua

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba wao wapate Pepo, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo wanaua na kuuawa.

Mnunuzi ni Mwenyezi Mungu (s.w.t.) muuzaji ni mumin, bidhaa ni nafsi na mali, cha kununuliwa ni pepo, na madalali ni Mitume. Bei yenyewe ni ya mkopo; kwamba muuzaji akabidhi bidhaa kwa mnunuzi atakapoitaka, lakini thamani yake atalipwa baadaye; na Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini; na hakuna mwenye kutekeleza ahadi na tajiri zaidi ya Yeye.

Utauliza: Mungu ni muumbaji wa nafsi na Mwenye kuruzuku mali, sasa vipi mwenye kumiliki kitu akinunue.

Jibu: Huku siko kununua kunakojulikana; isipokuwa ni kuhimiza twaa. Mwenyezi Mungu ameleta ibara ya kununua kwa mambo mawili:

Kwanza, mtiifu ategemee malipo na thawabu ya twaa yake; sawa na anavyotegemea muuzaji thamani badala ya bidhaa yake.

Pili, kuzindua kuwa imani sio tu maneno ya mdomoni, picha za akilini au matamanio yanayohisiwa katika nyoyo; isipokuwa ni kujitolea mhanga kwa nafsi na mali, kutafuta thawabu za Mwenyezi Mungu ambazo ni ghali zisizokwisha; sawa na anavyotoa mnunuzi milki yake katika bidhaa ambayo anaiona ina manufaa na yenye kufaa.

Kitu kikubwa kwa binadamu ni uhai wake na nafsi yake. Ama kupenda kwake mali ni kwa kuwa hiyo ni nyenzo ya kuhifadhi uhai na kutekeleza matakwa yake na hawaa zake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawatahini wanaodai wana imani kwa vitu wanavyovipenda ili ampabanue mkweli wa imani na mwongo; wala hataweza kutoa hoja kesho kwa saumu yake na swali yake akiwa amefanya ubakhili na kujizuia kujitolea kwa nafsi yake na mali yake.

Ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki.

Hii ni sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ {12}


AmejilazimisharehemaJuz.7(6:12)

Yaani yeye mwenyewe ndiye aliyejiwajibshia. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaahidi wapigania jihadi Pepo ikawa ni haki yao kutokana na ahadi hii;

hasa baada ya kuisajili katika Tawrat na Injil na Qur’ani. Na ni nani atekelezaye zaidi ahadi kuliko Mwenyezi Mungu?

Lengo la usisitizo huu ni kuwa wapigania jihadi wawe na uhakika wa malipo na thawabu adhimu; mpaka wawe kama walioyaona kwa macho, wafurahi na wapate bishara.

Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Huu ni usisitizo mwingine wa ahadi ya malipo mema. Watalamu wa elimu ya Tawhidi wanasema kuwa Mwenyezi Mungu akiahidi thawabu, basi atatekeleza aliyoahidi, na akiahidi adhabu basi ana hiyari, akiadhhibu ni kwa uadilifu wake na akasamehe ni kwa fadhila zake; na Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.
Tumeizungumzia thamani ya Pepo katika kufasiri Juz. 2 (2:155).

Kisha Mwenyezi Mungu akawasifu wale waliouza nafsi zao na mali zao kwa Pepo yake, kwa sifa hizi zifuatazo:

Wanaotubia kwa kila wanalolikosea; hata kama ni la makruh.

Wanaoabudu. Yaani wenye ikhlasi katika matendo yao yote.

Wanaohimidi Mwenyezi Mungu katika raha na dhiki.

Wanaohangaika katika ardhi kutafuta elimu au riziki ya halali.

Wanaorukuu, wanaosujudu. Yaani wanaoswali.

Wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu. yaani wanaoneza mwito wa Mwenyezi Mungu na twaa yake na kupamba na kila anayechezea haki yoyote miongoni mwa haki za Mungu na haki za waja wake.

Na wanaohifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu. Mipaka yake ni halali yake na haramu yake

Na wape bishara Waumini walio na sifa hizi, kuwa wao wana fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَنْ يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ {113}


Haimfali


iMtum


en


awale


walioamin


i


kuwatakia msamah


a


washirikina


ijapokuwa ni jamaa. Baada ya kuwabainikia kuwa wao niwatuwamotoni.

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَنْ مَوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِلَّهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ {114}


NahaikuwaIbrahimkumtakia msamaha baba yake ila ni kwa sababu ya ahadi aliyofanya naye, lakini ilipom


pambanuki


a


kuw


a


yey


e


ni


adui wa Mwenyezi Mungu,


alijiepush


a


naye


.


Hakika


Ibrahim alikuwa Mpole sana wamoyomvumilivu.