read

Aya 117 – 119: Mwenyezi Mungu Amemkubalia Toba Mtume

Maana

Bado maelezo ni ya vita vya Tabuk na matukio yake. Vita hivi vina mambo yake mahsusi yasiyokuwa katika vita vingine.
Miongoni mwa mambo hayo au yaliyo muhimu ni kuwa jeshi lilikuwa katika joto, njaa, kiu na uchache wa vipando. Ndio maana jeshi hili likaitwa ‘Jeshi gumu.’

Wapokezi wanasema kuwa kikundi fulani cha jeshi la Waislamu walikuwa wakipokezeana kupanda ngamia mmoja; chakula chao kilikuwa ni shayiri yenye wadudu na tende yenye mabuu. Mmoja wao alikuwa anaweza kufyonza tende akipata ladha yake, humpa mwenzake. Kuhusu maji walikuwa wanapochinja ngamia wanakamua mavi yaliyo katika utumbo wake na kurambisha ndimi zao.

Wanafiki walirudi nyuma kwenye vita hivi. Yamekishatangulia maelezo kuwahusu wao. Ama Waumini, ambao walimfuata Mtume (s.a.w.) katika vita vya Tabuk, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewashiria kwa kusema:

Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Mtume na wahajiri na Answar waliomfuata saa ya dhiki.

Ikisemwa kuwa fulani ametubia basi hufahamika kuwa alikuwa na dhambi, kisha akatubia, na ikisemwa kuwa Mwenyezi Mungu amepokea toba hufahamika kuwa amemkubalia toba yake. Lakini vile vile ina maana ya kuelekezwa rehema ya Mwenyezi Mungu na radhi yake kulingana na jumla ilivyo.

Maana ya kukubaliwa toba ndiyo yaliokusudiwa kwa wale watatu. Na maana ya rehema na radhi ndiyo yaliyokusudiwa kwa Mtume na swahaba waliomfuata katika saa ya dhiki. Hii inatokana na hali halisi ilivyo ya isma ya Mtume (s.a.w.) na utiifu wa waliomfuata katika saa ya dhiki.

Baada ya nyoyo za baadhi yao kukurubia kugeuka.

Waliorudi nyuma walirudi nyuma, na Waumini katika wahajiri na Answari wakamfuata, lakini kikundi katika hawa walipozidiwa na shida na ugumu wa safari walilegea na kukusudia kuachana na Mtume, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwapa uthabiti na kuwalinda. Hivyo wakavumilia na kujitolea.

Kisha akawakubalia toba kutokana na vile walivyoazimia kumwacha Mtume.

Makusudio ya kuwakubalia toba hapa ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwachukulia kuwa hawakudhamiria dhambi. Kwa sababu mwenye kud- hamiria dhambi kisha asilitende, haandikiwi kitu.

Hakika yeye kwao ni Mpole, Mwenye kurehemu.

Kwa vile yeye alijua kwao ukweli katika imani yao na ikhlasi katika nia yao na kwamba dhamira yao ilikuwa ni jambo lililozuka tu na kuondoka bila ya kuacha athari yoyote.

Na pia wale watatu walioachwa nyuma, mpaka ardhi ikawa finyu juu yao pamoja na wasaa wake; na nafsi zao zikadhikika juu yao, na wakayakinisha kuwa hakuna kwa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake.

Wameafikiana wafasiri na wapokezi kwamba watatu hao ni katika waumini wa Kianswari, waliobaki nyuma katika vita vya Tabuk kwa uvivu na kupuuza, sio kwa unafiki na inadi. Hao ni Kaab bin Malik, Mar’wan bin Rabii na Hilal bin Umayya Al-waqif.

Masimulizi ya hao tunamwamchia Twaha Hussein aliyeleta Muhtasari wa yale waliyoyoafikiana wote na yanayofahamika katika Aya, Anasema katika Kitab mir-atul-islam:

“Watatu hawa walikuwa na imani kubwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wenye mapenzi ya ukweli kwake yaliyowafanya wasiongezee kosa la uwongo baada ya lile la kubaki nyuma. Kwa sababu ya ukweli na kuhofia Mwenyezi Mungu kuwafedhehesha waongo, walikiri makosa yao; na Mtume akawasikia na kutangaza kuwa wao ni wakweli, lakini pamoja na hayo hakuwasamehe; akaamrisha waumini wasiwasemeshe. wakawa wametengwa wakiwa mbali kabisa na watu; wakawa katika hali ambayo, jela ilikuwa bora kuliko hali hiyo.
Siku moja Mtume akatuma ujumbe wa kuwaaamuru watengane na wake zao. Hilo sio ajabu, kwa sababu wake zao ni waumini; na amri imetoka kuwa waumini wote watengane nao.

Baada ya kupita siku hamsini wakiwa wamejuta sana, Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya kuwatakabalia toba yao. Waumini wote wakalifurahi hilo wakawa wanawapongeza hawa watatu kwa kutakabaliwa toba. Kaab, alifurahi sana; akadhamiria kutoa sadaka mali yake yote, lakini Mtume akamwamuru atoe sehemu tu. Kaab akaahidi kutosema uwongo mpaka kufa”.

Kisha akawakubalia toba ili wapate kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwingi wa kukubali toba Mwenye kurehemu.

Utauliza kuwa dhahiri ya kukubaliwa toba ni kuwa walitubu na wakakubaliwa toba; na dhahiri ya ili wapate kutubu ni kuwa hawajatubia bado; sasa je, kuna wajihi gani?

Swali hilo limejibiwa kwa majibu mengi. Lenye nguvu zaidi ni lile lise- malo kuwa makusudio ya kukukabaliwa toba ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakubalia toba ili watubu na wasiendelee na dhambi na waseme lau Mwenyezi Mungu atatukubalia toba yetu, basi tutatubu kabisa. Hiyo inafanana na mtu unayempenda akikufanyia uovu nawe unataka kumsamehe, ukamfundisha msamaha ili aombe, nawe umsamehe.

Tumeweka mlango maalum wa toba katika Juz.4 (4: 17).

Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wa kweli.

Wakweli ni Mitume na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa kabisa. Kwa maneno mengine, makusudio ya ukweli hapa sio kutosema uwongo tu katika mazungumzo, kwa sababu wako watu wasiosema uwongo lakini haifai kuwafuata katika kila jambo; isipokuwa makusudio ni ukweli katika kauli vitendo na elimu ambavyo vitamwandaa mwenye navyo kuweza kufuatwa.

مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُمْ مِنَ الْأَعْرَابِ أَنْ يَتَخَلَّفُوا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنْفُسِهِمْ عَنْ نَفْسِهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ {120}


HaiwafaliiwatuwaMadina na Mabedui walio kandoni


mwa


o


kubak


i


nyum


a


ya Mtum


e


w


a


Mwenyezi


Mungu


;


wal


a


kujipendelea


nafsi zao kuliko nafsi yake. Hayonikwasababuyakuwa hakiwapati kiu wala taabu


wal


a


nja


a


katik


a


nji


a


ya Mwenyez


i


Mungu


;


wala


hawakanyagi ardhi ichukizayomakafiri,walahakiwapati chochote kutokana na adui,


il


a


huandikiw


a


kuw


a


ni amal


i


njema


.


Hakika


Mwenyezi Mungu haupotezi ujirawawatendaomazuri.

وَلَا يُنْفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {121}


W


ala hawatoi chochote cha kutumiwa kidogo wala kikubwa wala hawalikati bonde ila wanaandikiwa kuwa Mwenyezi Mungu awalipe mema ya yale


waliyokuwawakiyatenda.