read

Aya 120 – 121: Haifai Watu Wa Madina Kubaki Nyuma

Maana

Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio kandoni mwao kubaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu; wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake.

Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Muhammad (s.a.w.). Makusudio yake hapa ni dini ya Mwenyezi Mungu na haki. Kwa sababu dini ya haki inaun- dika katika utu wake mtukufu.

Kuinusuru haki ni wajibu kwa kila Mwislamu, wala hakuhusiki na watu wa Madina na walio kandoni mwao; isipokuwa wametajwa hao kwa kuwa karibu kwao na kuwa jirani, na pia kwa kulingana na mazungumzo ya vita vya Tabuk. Maana ni kuwa ni juu ya kila Mwislamuu kuinusuru haki na kuizuia batili wala asiathirike na manufaa na masilahi kuliko dini ya Muhammad, kwa kutoa visababu vya uwongo, kama walivyofanya wanafiki.

Hayo ni kwa sababu ya kuwa hakiwapati kiu wala taabu wala njaa katika njia ya Mwenyezi Mungu; wala hawakanyagi ardhi ichukizayo makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na adui, ila huandikiwa kuwa ni amali njema.

Hayo ni ishara ya kukataza kubaki nyuma na kuacha kuwapiga jihadi wabatilifu.

Ni jambo la kutia uchungu kwa mtu yeyote, awe Mwislamuu au la, kumwacha akanyage mchanga wa mji wake na nchi yake; pengine awe kibaraka asiye na dini wala dhamiri. Uislamu haumruhusu yeyote, vyovyote alivyo, kukanyaga ardhi ya mwingine ila kwa sababu mbili; Kuzuia madhara ya watu; kama vile kuzima moto kukinga mali na mali ya jirani.

Kuingiza nguvu iliyoadilifu itakayowazuia watu wa hapo na dhuluma na uadui kwa mji mwingine; kama alivyofanya Mtume (s.a.w.) katika vita vya Tabuk, baada ya Waroma kuazimia kuipiga madina na kuumaliza Uislamu na Mtume wake.

Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa watendao mazuri.

Hakuna kitu rahisi kwa mtu kuliko kufanya wema, maadamu Mwenyezi Mungu anakuandikia wema kukaa kwake, kusimama kwake, na hata unyao mmoja tu anaoukanyaga kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu.

Wala hawatoi chochote cha kutumiwa kidogo wala kikubwa wala hawalikati bonde ila wanaandikiwa kuwa Mwenyezi Mungu awalipe mema ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

Haya na yaliyo kabla yake yanafupilizwa na kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

فَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ {7}


“Naatakayefanyaheriuzaniwasisimiziataiona”.(99:7).

Lengo la ufafanuzi huu ni kuhimiza mali ya heri na kuhimiza kumpiga jihadi anayeeneza ufisadi katika ardhi.

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنْفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِنْ كُلِّ فِرْقَةٍ مِنْهُمْ طَائِفَةٌ لِيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنْذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ {122}


W


al


ahaiwafali


iwaumini


kutoka wote. Kwa nini kisi


tok


e


kikund


i


katik


a


kila


kundi miongoni mwao kuji


funz


a


din


i


n


a


kuwaonya


watuwaowatakapowarudia. Iliwapatekujihadhari.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُمْ مِنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ {123}


Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu katika makafiri na wakute


kwen


u


ugumu


;


n


a


jueni kuw


a


Mwenyez


i


Mungu yuk


o


pamoj


a


n


a


wenye


takua.