read

Aya 122 – 123: Kwa Nini Kisitoke Kikundi

Maana

Wala haiwafalii waumini kutoka wote.

Aya hii inaungana na Aya iliyotangulia kuwa haifai watu wa Madina kubaki nyuma. Njia ya kuungana ni kwamba iliposhuka Aya iliyotangulia Makabila ya Kiislam yalisema: Wallahi kuanzia leo hatutabaki nyuma ya Mtume katika vita. Wakamiminika kutoka madina kwa lengo hili.

Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akateremsha Aya hii, tuliyonayo, kuwa hawatakiwi kutoka wote kwa jihadi, bali hali hiyo inatofautiana kwa kutofautiana vita. Mara nyingine jihadi inakuwa ni wajibu kwa kila mtu, mara nyingine inakuwa ni wajibu kifaya, wakitekeleza baadhi basi wajibu umewaondokea wote.

Ama atakayetofautisha kati ya wajib hizo mbili ni Mtume (s.a.w.). Watatoka Waislamu wote kama akitaka watoke, na watatoka baadhi akitaka hivyo.

Kwa nini kisitoke kikundi katika kila kundi miongoni mwao kujifunza dini na kuwaonya watu wao watakapowarudia.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kubainisha kuwa si wajibu kwa kundi lote kutoka katika kila vita, sasa ana bainisha kuwa kuna wajibu mwingine usiokuwa jihadi ambao ni wajibu kuutekeleza, sawa na jihadi; kama vile kutoka kikundi katika kila mji au kabila kwenda Madina au mahali penginepo, kujifunza dini ya Mwenyezi Mungu – wajue halali na haramu; kisha warudi kwa watu wao wawongoze na kuwatahadharisha na adhabu ya Mwenyezi Mungu inayotokana na kumwasi na kuhalifu amri zake.

Ili wapate kujihadhari.

Yaani wawasikilize wanowaongoza na wawatii.

Hivi ndivyo tulivyoona katika kufasiri Aya hii, tukiwa tumetofautiana na wafasiri wengi ambao wamefanya ‘kujifundisha’ ni sifa ya watakaobaki, sio watakaotoka; wakasema katika ufanuzi wao kuwa ni wajibu kwa Waislamu kugawanyika makundi mawili: Kundi liende kwenye Jihad na kundi jingine libaki Madina kujifunza sunna na faradhi.

Tafsiri tuliyokwenda nayo sisi ndiyo yenye asili katika riwaya za Ahlu Bait wa Mtume (s.a.w.) ambao ndio wajuzi zaidi wa Qur’ani na siri zake.

Miongoni mwa riwya hizo ni ile isemayo kuwa Mtu mmoja alimwuliza Imam Ja’far Asswadiq (a.s.) kuhusu maana ya kauli ya Mtume (s.a.w.): “Kutofautiana umati wangu ni rehema”. Akasema: Makusudio ya kutofautiana sio kuzozana, vinginevyo kuafikiana kwao ingelikuwa ni adhabu; isipokuwa makusudio ni kuhangaika duniani kutafuta elimu. Kisha Imam akaitolea dalili Aya hii kwa makusudio ya maana hayo.

Hakuna mwenye shaka kwamba dalili hiyo haikamliki ila ikiwa kujielimisha ni sifa ya kikundi kinachotoka sio kinachobaki.

Wanachuoni wa usul wameitolea dalili Aya hii kuwa ‘Habari Moja’ inayo nukuliwa kutoka kwa Masumu ni hoja inayopasa kutumiwa katika hukumu za kisharia Njia ya kutoa dalili ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ame- wajibisha kwa ulama kufundisha na kuonya. Na, ukishakuwa wajibu huu kwa ulama, basi imekuwa wajibu kwa asiyejua kukubali kauli ya ulama na kuitumia; vinginevyo itakuwa wajibu wa kujifundisha na kuonya; ni mchezo tu.

Vile vile ikiwa ni wajibu kwa asiyejua kujifundisha, basi imekuwa ni wajibu kwa ulama kufundisha; vinginevyo itakuwa wajibu wa asiyejua kujifundisha ni mchezo tu. Imam Ali (a.s.) anasema: “Mwenyezi Mungu hatawaadhibu wajinga kwa kutojifundisha mpaka awaadhibu wenye elimu kwa kutofundisha”.

Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu katika makafiri.

Aya hii inawahimiza Waislamu kulinda mipaka na maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zao. Katika Majmaul-bayan kuna maelezo kuhusu tafsiri ya walio karibu yenu katika makafiri kuwa ni walio karibu zaidi, isipokuwa kama kuna mapatano. Hii ni dalili kuwa ni wajibu kwa watu walio katika hali ya hatari kujilinda wakihofia kuchafuliwa Uislamu au mji wa Waislamu, hata kama hayuko Imam mwadilifu”.

Tumezungumizia kwa ufafanuzi kuhusu kupigana na makafiri katika Juz. (2:193) Kwa anuani ya ‘Uislamu unapiga vita dhulma na ufisadi’.

Imam Zainulabidin Na Msingi Wa Vita

Na wakute kwenu ugumu.

Ugumu hapa ni fumbo la nguvu na kuilinda vizuri mipaka.

Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua.

Ambao wameamini imani ya kweli; wakafanya ikhlasi katika kupigana na adui yao na adui wa Mwenyezi Mungu; wakajiandaa kwa nguvu zao zote, kama alivyo waamrisha Mwenyezi Mungu.

Maelezo ya kupendeza kuhusu maudhui haya ni dua ya Imam Zainul Abidin, Ali Bin Hussein (a.s.), akimlingania Mola wake na kuwaombea watu walio katika hatari ya kushambuliwa na walinzi wa miji ya Kiislamu. Alisema katika aliyoyasema:

“Ewe Mola Wangu! Mrehemu Muhammad na Ali wa Muhammad. Na uifanye nyingi idadi yao, uzinoe silaha zao, uzilinde nchi zao, uzuie kushambuliwa kwao, ushikamanishe mjumuiko wao, uyaaangalie vizuri mambo yao, uwatoshelezee mahitaji yao, uwasaidie kwa kuwapa subra (uvumilivu), uwahurumie kwa kuwakinga na hadaa, uwafahamishe wasiyoyajua, uwaelimishe wasiyokuwa na ujuzi nayo.

Wanapokutana na adui wasahaulishe kukumbuka dunia yao iliyo na hadaa na ghururi, ufute katika nyoyo zao mawazo ya mali yenye fitna na uijalie pepo machoni mwao.”

Hiyo ndiyo misingi ya ushindi wa kuweza kulizuwiya jeshi lolote kadiri litakavyokuwa na silaha za kisasa; hata tonoradi, mizinga, mapesa ya kuwalipa wapiganaji, elimu ya vita na kutumia silaha pamoja na mbinu zote za kupigana.

Silaha kubwa zaidi ni kuunganisha majeshi na kuzifanya nyoyo ziwe na ikhlasi ya kupigana na kuwa na uvumilivu hadi kufa, kuisahau dunia na kuamini kuwa mtu kufa shahidi, katika kupigania dini yake na nchi yake ndio faida na kufuzu kukubwa.

Je, si Waarabu na Waislamu, wa zamani na wasasa, wamekuwa ni chakula kwa sababu tu ya mali yenye fitina? Dalili ya hayo ni janga la tarehe 5 June,1967.

Maneno haya ya Imam Zainul Abidin yamepitiwa na zaidi ya karne 13, lakini pamoja na hayo lau, hivi sasa, kamanda mkuu angetaka kusoma sababu za ushindi, basi hatahitajia ila kufafanua matamko haya mafupi aliyoyatamka Imam.

وَإِذَا مَا أُنْزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُمْ مَنْ يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ {124}


N


ainapote


r


emshw


a


Sura


yoyote, basi miongoni mwao kuna wanaosema: Ni nani


miongon


i


mwen


u


Sur


a


hii


imemzidishi


a


imani


?


Basi wal


e


walioamini inawazidishi


a


imani


,


nao


wanafurahi.

وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ {125}Ama wale wenye maradhi


katik


a


nyoy


o


zao


,


basi


inawazidshi


a


uov


u


ju


u


ya


uovu wao. Na wanakufa hali nimakafiri.

أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ {126}


Je


,


hawaon


i


kwamb


a


wao


wanajaribiw


a


kil


a


mwaka


mara moja au mara mbili?


Kish


a


hawatub


u


wala


hawakumbuki.

وَإِذَا مَا أُنْزِلَتْ سُورَةٌ نَظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُمْ مِنْ أَحَدٍ ثُمَّ انْصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّهُ قُلُوبَهُمْ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا يَفْقَهُونَ {127}


N


a


inapote


r


emshw


a


Sura wanatazamana


:


Je


,


kuna


yeyote anyewaona? Kisha hugeuka.Mwenyezi Mungu amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.