read

Aya 124 – 127: Inapoteremshwa Sura

Maana

Na inapoteremshwa Sura yoyote, basi miongoni mwao kuna wanaosema: Ninani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia imani?

Yaani baadhi ya wanafiki walikuwa wakidharau Qur’ani na kuulizana kuwa kuna ajabu gani ya hii?

Kwa hiyo wanazifanya nafsi zao, zilizochafuliwa na tamaa na dhambi, kuwa ni kipimo cha haki na ukweli.

La kushangaza ni kuwa washirikina walikuwa wakiukubali ukuu wa Qur’ani na athari zake zinazoingia nyoyoni, wakuwa wanausiana kuwa wasisikilize, kwa kuhofia kuvutwa kwenye Uislamu bila ya kujitambua. Mwenyezi Mungu anasema:

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ {26}


“NaW


alisemawaliokufuru:MsisikilizeQu


r


’anihiinafanyenizogo,huendamkashinda”(41:26)

Hii inafahamisha, moja kwa moja, kuwa wanafiki wana athari mbaya zaidi kuliko washirikina.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewajibu wanafiki kwa kuwaaambia:

Basi wale walioamini inawazidishia imani.

Yaani, ikiwa katika nafsi zenu enyi wanafiki, haina athari yoyote nzuri, baada ya kupigwa chapa ya matamanio, basi waumini inawazidishia uongofu na yakini. Kwa sababu nafsi zao ni safi hazina taka ya uchafu kama nafsi zenu.

Nao wanafurahi kila inapoteremshwa Sura au Aya katika Qur’ani, kwa sababu inawapa bishara ya Pepo na kuwaongoza kwenye njia iliyo sawa.

Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidshia uovu juu ya uovu wao.

Kila mwenye kuwa mbali na haki na hali halisi, na imani yake na rai yake ikavutwa kwenye dhati yake na mawazo yake, basi yeye ni mgonjwa wa moyo na akili. Na anapotakiwa kuwa kwenye hukumu halisi na akakataa huzidi maradhi yake.

Unafiki ni maradhi kwa sababu ni upotevu. Wanafiki wa sasa jinsi wanavyopupia dunia ni kama mfano wa funza; kila anavyozidi kujikunja ndio anakuwa mbali zaidi na kutoka mpaka anakufa.

Na wanakufa hali ni makafiri kwa uchaguzi wao mbaya; kama anavyok- ufa funza kwa sababu yake mwenyewe.
Je, hawaoni kwamba wao wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili?

Makusudio ya kujaribiwa hapa ni kufedheheshwa na kufichuka njama zao kwa wote. Aya hii inaambatana na Aya iliyo tangulia: “Na inapoteremshwa Sura …”

Njia ya kuungana ni kuwa wanafiki walikuwa wakimlia njama Mtume (s.a.w.) na wakimshutumu; kama vile kusema kuwa ni sikio, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alikuwa akimfahamisha Mtume wake njama zao, na Mtume akiwafedhei. Mara nyingine hilo hukaririka zaidi ya mara moja katika mwaka.

Katika hilo kuna dalili mkataa juu ya ukweli wa Mtume na kwamba Qur’ani inatoka mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo ilikuwa ni wajibu kwao wapate mawaidha na wamwamini badala ya kudharau na kucheza chere kwa kusema: Ni nani miongoni mwenu amezidishiwa imani hii na hii?

Kisha hawatubu wala hawakumbuki.

Na hawakumbuki ila wenye akili; na hawa wamepofushwa akili zao na nyoyo zao kwa matamanio.

Na inapoteremshwa Sura hutazamana.

Ndivyo walivyo wanafiki kila wakati na kila mahali – wanaposhindwa kuikabili haki kwa hoja basi wanakonyezana, kuonyesha kuzama kwao kwenye ukafiri na upotevu.

Je kuna yeyote anayewaona.

Yaani wanayasema haya kwa mdomo au kwa vitendo:

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ۚ {108}W


anajificha kwa watu wala hawajifichi kwa Mwenyezi Mungu, na yeye yu pamoja nao walipokula njama usiku kwa maneno asiyoyapenda” Juz.5 (4:108)

Kisha hugeuka.

Yaani wanafanya wanayoyafanya kisha hugeukia kwenye shughuli zao; kama vile hawakufanya kitu.

Mwenyezi Mungu amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.

Mwenyezi Mungu amezigeuza nyoyo zao na haki baada ya kuwasimamishia hoja na ubainifu, na baada ya kuwafanyia inadi na kukataa kusalimu amri. Kwa hiyo wao ndio sababu ya moja kwa moja ya kugeuka na ikategemzwa kwa Mwenyezi Mungu kupita kwao.

Ni desturi ya Qur’ani Tukufu kutegemeza mambo mengi ya waja kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuangalia kuwa yeye ni muumbaji wao na mwenye kuutengeneze ulimwengu na vitu vyake.

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ {128}


Hakik


aamewaji


aMtume kutokan


a


n


a


nyinyi


wenyewe.


Y


anamhuzunisha yanayo-wataabisha, anawahangaikieni sana, kwa wau-


min


i


n


i


mpole


,


mwenye


huruma.

فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ {129}


Bas


i


wakikengeuka


,


sema:


Anitoshelezeay


e


ni


Mwenyez


i


Mungu


,


hakuna


Mola (apasaye kuabudiwa) ila yeye tu; kwake ninategemea; naye ndio bwana wa Arshitukufu.