read

Aya 15 – 17: Lete Qur’an Isiyokuwa Hii

Maana

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana nasi husema: “Lete Qur’ani isiyokuwa hii, au ibadilishe.

Makusudio ya wale wasiotaraji kukutana na Mwenyezi Mungu ni washirikina. Mtume (s.a.w.) alikuwa akiwapa hoja wao, mayahudi na wakristo kwa Qur’ani; na alikuwa akijadaliana nao kwa mjadala mzuri. Mjadala wake na washirikina na mayahudi ulikuwa mkali, kwa sababu wao ndio waliokuwa maadui na wapinzani sana; kama ilivyoelezwa katika Aya kadhaa zilizotangulia.

Ama wakristo kuna waliomtembelea na wakakubali kutoa kodi; kama vile wakristo wa Najran. Na wengine walikusudia kumpiga vita Madina, Mtume akawakatia njia na kupigana nao katika ardhi ya Sham.

Washirikina walikuwa wakimpa Mtume maoni ya kila aina ya ujinga wao na mchezo wao; kama vile ilivyodokezwa katika Juz.1(2:118), walipomtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) awazungumzishe Mwenyezi Mungu kwa mdomo.

Aya hii tuliyonayo inasimulia maoni yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuwa awaletee Qur’ani nyingine au aibadilishe kwa vile Qur’ani hii imewaletea dini mpya. Inawalingania kwenye Tawhid na kuamini ufufuo na malipo.

Pia inathibitisha misingi ya uadilifu na usawa, kutupilia mbali utabaka na kuharamisha riba na dhuluma; wakati ambapo wao wana dini ya waungu wengi, wanapinga ufufuo na kuharakisha wanayoyatamani. Ndipo wakamtaka Muhammad (s.a.w.) awaletee Qur’ani itakayothibitisha dini yao na kuiga kwao au angalau, waondoe ile sehemu wasiyoiridhia.
Kuna tofauti gani kati ya maombi haya ya washirikina wa Kijahiliya na vijana wengi wa karne ya ishirini, wasemao kuwa kuna haja gani ya dini na kwa nini kuwe na halali na haramu? Na, maendeleo ya makompyuta hayahitaji msingi na dini.

Sema: Haifai mimi kubadilisha kwa hiyari ya nafsi yangu; sifuati ila niliyopewa wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimwasi Mola wangu, adhabu ya siku iliyo kuu.

Mtume ni mwenye kunakili tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu sio mwenye kuweka sharia; sawa na mpokezi wa Hadith kutoka kwa Mtume. Kuna Hadith iliyopokewa kutoka kwake isemayo “Mwenye kunikadhibisha basi na ajichagulie makazi yake motoni,” sasa itakuwaje yeye amkadhibishe Mwenyezi Mungu. Haiwezekani kwa mwenye isma kukosea au kuteleza.

Aya hii inampinga yule mwenye kutoa fatwa na kuhukumu bila ya dalili ya kisharia. Vile vile ni dalili mkataa kuwa Mtume kamwe hakutoa hukumu kwa ijtihadi yake, na kwamba hukumu zake zote zilikuwa ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mwenye kusema kuwa alifanya ijtihad basi, atakuwa hakumtofautisha na mafakihi wengine. Shia wanapinga kuwa Mtume alifanya ijitihadi ambapo Sunni wanatofautiana. Wengine wanaafikiana na Shia na wengi wamesema kuwa alifanya ijitihadi.

Sema: lau Mwenyezi Mungu angelitaka nisingliwasomea hiyo wala nisingeliwajuza.

Dhamir ya hiyo ni ya Qur’ani. Maana ni kuwa lau Mwenyezi Mungu asingeliileta nisingelifanya hayo, lakini nimefanya niliyoyafanya kwa kutekeleza matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Nimekaa kwenu umri kabla yake, basi hamfahamu.

Mtu ambaye ameishi kwa watu miaka arubaini kabla ya kupewa wahyi akiwa hakusoma kitabu chochote au kufundishwa na mwalimu, wala hakuwahi kufanya jambo la kulaumiwa; bali maisha yake yote yalikuwa ni mema, mwenye ukweli na uaminifu mpaka akaitwa Amin (mwaminifu). Pamoja na yote haya hamfahamu kuwa mtu aliye hivi yuko mbali na uwongo na uzushi?

Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo au akadhibishaye Aya zake?

Maana ya kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo ni kuweka kwenye dini jambo lililo mbali na dini. Maana ya kukadhibisha Aya zake ni kukanusha yale ambayo kwa asili yanatoka kwake. Hii ndiyo bid’a ambayo Mtume ameielezea kwa kusema: “Kila bid’a ni upotevu na kila upotevu ni katika moto.”

Hakika hawafaulu wakosefu.

Kwa sababu njia ya kufaulu na kuokoka ni ukweli na ikhlasi. Ama uwongo na uzushi ni njia ya maangamivu na utwevu, na haifati njia hiyo isipokuwa mwovu mkosefu.

وَيَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنْفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِنْدَ اللَّهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ {18}


Nawanaabuduwasiowadhuru wala kuwanufaisha badala


y


a


Mwenyez


i


Mungu


.


Na wanasema


:


“Haw


a


ndio waombez


i


wet


u


kwa


MwenyeziMungu.”Sema:Je,


mnamwambi


a


Mwenyezi Mung


u


asiyoyaju


a


katika


mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka


n


a


ha


o


wanaomshirikisha naye.

وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِنْ رَبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ {19}


Na hawakuwa watu ila ni umma mmoja tu kisha wakahitalifiana. Na lau si neno lililotangulia kutokana na Mola wako, bila shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika hayo wanayokhitalifiana.

وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنْزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِنْ رَبِّهِ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّهِ فَانْتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُمْ مِنَ الْمُنْتَظِرِينَ {20}


N


a


wanasema


:


“Kwanini


hakute


r


emshiwa ishara kutoka kwa Mola wake?” Sema


hakik


a


ghaib


u


n


i


ya Mwenyez


i


Mung


u


tu


,


basi


ngojeni na mimi niko pamoja nanyikatikakungoja.