read

Aya 18-20: Wanasema Hawa Ni Waombezi Wetu

Maana

Na wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha badala ya Mwenyezi Mungu.

Hawa ni wale waliomwambia Mtume alete Qur’ani nyingine au aibadilishe. Wao walikuwa wakiabudu masanamu; wakiamini kuwa yanawanu- faisha na kuwadhuru; kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

Na wanasema: “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini imani yao hii haina msingi wowote isipokuwa ni njozi na mawazo tu. Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.) akanushe madai yao kwa kuwaambia:

Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.

Washirikina walidai kuwa masanamu yao yatawaombea kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa haya ni kweli, basi Mwenyezi Mungu angeliujua uombezi huu na kwa kuwa haujui basi ina maana kuwa washirikina ni waongo na wazushi.

Na hawakuwa watu ila ni umma mmoja tu kulingana na maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu; kisha hawa zao zikawatenganisha kutoka asili yao na ufuasi ukawagawa vikundi katika dini yao baada ya kushindana kupata raha za maisha.

Na lau si neno lililotangulia kutokana na Mola wako, bila shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika hayo wanayokhitalifiana.

Makusudio ya neno hapa ni kutoharakisha Mwenyezi Mungu adhabu ya waasi na thawabu za watiifu; bali anangojea mpaka siku ya ufufuo; ili kila mtu, kwa hiyari na radhi ya nafsi yake, afikie heri au shari na ubora au uduni.

Lau Mwenyezi Mungu angeliharakisha adhabu ya muovu katika watu basi wangelikuwa sawa, lakini kwa kuhofia tu si kwa utiifu.

Hakuna mwenye shaka kwamba hili ni kinyume na kuondoa maana ya thawabu na adhabu. Vile vile litapingana na hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kudhihirisha hakika ya mtu kulingana na matendo yake na uchaguzi wake. Umetanglia mfano wake katika Juz. 2 (213) na Juz. 6 (6:48).

Na wanasema: “Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake?”

Mwenyezi Mungu alimteremshia Muhammad ishara nyingi na miujiza kadhaa, lakini washirikina waliosema hivi walitaka ishara kulingana na hawa zao na miujiza wanayoitaka wao; kama walivyosema:

“Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi” Juz. 1 (2:218).

لَوْلَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا {7}


“MbonahakuteremshiwaMalaikaakawamuonyajipamojanaye”(25:7).

Sema hakika ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu, basi ngojeni na mimi niko pamoja nanyi katika kungoja.

Yaani, ewe Muhammad waambie hawa wenye inadi kuwa ishara mnazozitaka ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu mimi sina langu jambo wala sijui kuwa Mwenyezi Mungu ataiteremsha kutoka mbinguni au Mimi na nyinyi katika hili ni sawa katika hilo. Basi tuone ni kundi gani litasalimika na hasira za Mwenyezi Mungu.

وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِنْ بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُمْ مَكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚ قُلِ اللَّهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ {21}


Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya dhara


kuwagusa


,


huanz


a


kuzipan


gi


anjam


a


A


y


azetu


.Sema


Mwenyezi Mungu ni mwepesi zaidi wa kupanga njama. Hakika wajumbe wetu


wanayaandik


a


mnayoyapan


ga.

هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنْتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِمْ بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِنْ كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنْجَيْتَنَا مِنْ هَٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ {22}


Y


eyendiye anayewaendesha bara na baharini. Hata mnapokuwa majahazini na yakaenda nao upepo mzuri na wakaufurahia, mara upepo mkali ukawazukia


yakawaji


a


mawimb


i


kutoka


kila upande na wakaona wamekwishazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia


ikhlasi


:


ukituoko


a


n


a


haya


bila shaka tutatakuwa miongonimwawanaoshukuru.

فَلَمَّا أَنْجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنْفُسِكُمْ ۖ مَتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {23}


Lakini alipowaokoa, mara wanafanya jeuri katika ardhi pasipo haki. Enyi watu! Hakika jeuri yenu itawarudia nyinyi wenyewe tu. Ni sta


r


ehe ya maisha ya dunia kisha ma


r


ejeo yenu ni kwetu ndipo tuwaambie mliyokuwa mkiyatenda.