read

Aya 21-23: Sema: Mwenyezi Mungu Ni Mwepesi Zaidi Wa Kupanga Njama

Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya dhara kuwagusa, huanza kuzipangia njama Aya zetu.

Imesemekana kuwa makusudio ya watu ni washirikina. Kauli hii haiko mbali na mfumo wa maneno, kwa sababu Aya inawazungumzia washirikina lakini haizuwii kuwa makemeo yanamhusu kila mwenye kukana neema za Mwenyezi Mungu, ni sawa upinzani utokane na mu’min au kafiri, kabla ya madhara au baada.

Madhumuni ya Aya hii yanalingana na Aya ya 12 ya Sura hii: “Na dhara inapomgusa mtu hutuomba naye ameegesha ubavu wake au katika hali ya kukaa au katika hali ya kusimama Lakini tunapomwondolea dhara yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondolee dhara iliyomgusa.” Hiyo inasema kuwa mtu anamkumbuka Mwenyezi Mungu katika saa ya dhiki na hii tunayoifasiri sasa inasema kuwa anapomjaalia wepesi huzipangia njama Aya zake.

Mkusudio ya njama hizo ni kupinga Aya za Mwenyezi Mungu na kukataa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye msababishaji katika kumwondolea madhara na balaa na kufasiri sababu nyingine zizisizo na msingi wala asili; kama masanamu, nyota, sadfa na tafsiri nyinginezo mbovu zinazotofautiana kulingana na watu, mawazo yao na uigaji wao.

Sema, Mwenyezi Mungu ni mwepesi zaidi wa kupanga njama. Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayoyapanga.
Makusudio ya njama za Mwenyezi Mungu ni kwamba yeye anawalipa wapanga njama kwa njama zao na kuwaandalia adhabu kali bila ya wao kutambua. Pia tumelizungumzia hilo katika Juz.3 (3:54).

Makusudio ya wajumbe waandishi ni Malaika. Maana ni kuwa Yeye Mwenyezi Mungu mtukufu anavidhibiti vitendo vya wenye njama na kuwalipa wanayostahiki.

Yeye ndiye anayewaendesha bara na baharini.

Yaani Yeye Mwenyezi Mungu mtukufu amempa mja wake uwezo wa kutembea humo. Makusudio ya ishara hii ni kukumbusha fadhila zake na nema zake ili awe katika wenye shukrani. “ Utukufu ni wako ewe Mola wangu! Ni ubainifu ulioje wa ukarimu wako kwa anayekuridhisha na anayekuchukiza”

La kushangaza ni kauli ya Abu Bakr Al-mughafiri katika Kitabu Ahkamul- Qur’an, kwamba Aya hii inafahamisha kuwa usafiri wa baharini ni halali sio haramu; tena akarefusha maneno katika kutoa dalili ya uhalali wa kusafiri bahrini. Amesahau kuwa kawaida ya sharia, ambayo anaijua asiye- jua na Mjuzi, ni uharamu ndio unaohitajia dalili na sio uhalali.

Hata mnapokuwa majahazini na yakaenda nao upepo mzuri na wakaufurahia, mara upepo mkali ukawazukia yakawajia mawimbi kutoka kila upande na wakona wamekwishazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia ikhlasi: ukituokoa na haya bila shaka tutatakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

Aya hii inafahamisha kuwa binadamu ana maumbile ya kumwamini Mungu kwa sababu ya kurejea kwake katika shida. Angalia kifungu: ‘Mwenyezi Mungu na maumbile’ katika Juz.7 (6:41).

Mwenye Al-manar amesema katika kufasiri Aya hii, ninamnukuu: “Washirikina walikuwa hawamuombi yeyote wakati wa shida, isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba Mola wao. Ama waislamu wengi, zama hizi, hawamuombi Mwenyezi Mungu, kama wanavyodai hilo hao wenyewe, isipokuwa wanawaomba wafu; kama vile Badawiy, Rifai, Dasuqi, Jaylani, Almatbuli, Abu sarii na wengineo wasiokuwa na hisabu.

Na utawakuta wenye vilemba wa Azhar na wengineo hasa waangalizi wa makaburi yanayoabudiwa wakitumia wakfu na nadhiri zake kutoka kwa wale wanaowahadaa kwa shirki yao wakieguza jina katika Lugha ya kiarabu kwa kuiita tawassul n.k.” Mfano wa maneo haya yamo katika Tafsir ya Maraghi.

Nimesoma katika gazeti la Misri kuwa wamisri wanaandika karatasi wakizitupa kwenye kaburi la waliy. Humo wanaandika mashtaka ya wahasimu wao wakitaraji maiti awalipizie kisasi kutokana na dhulma na uovu walio- fanyiwa. Nimenukuu mashtaka haya katika kitabu Minhuna wa hunaka (Huku na huko).

Ama kuhusu mkusanyiko wa hafla ya mazazi ya walii, tuuchie gazeti la Aljumhuriya la tarehe 1-11-1968, likisema: “ Msongamano ulikuwa kama siku ya kufufulia watu; ni kama mawimbi au shamba lililopandwa miti”

Lakini alipowaokoa, mara wanafanya jeuri katika ardhi pasipo haki.

Walimwahidi Mwenyezi Mungu kumcha na kumshukuru akiwaondolea, lakini alipowafanyia walivunja ahadi.

Hii inakariri aya iliyotangulia kwa ibara nyingine. Ile inasema wanazipangia njama Aya zetu na hii inasema wanafanya uovu katika ardhi. Maana ni moja au yanaoana. Lengo ni kuonyesha inadi yao na jeuriyao kwa picha mbaya.

Enyi watu! Hakika jeuri yenu itawarudia nyinyi wenyewe tu.

Kwani mwenye kuchomoa upanga wa jeuri atauliwa kwa huo.

Ni starehe ya maisha ya dunia kisha marejeo yenu ni kwetu ndipo tuwaambie mliyokuwa mkiyatenda.

Mjeuri anaweza kufurahi na kuburudika na ushindi, lakini ni wa muda; kisha inakuja balaa na hasara. Mtume (saw) anasema: “Mambo matatu yanawarudia watu wake: Njama, njama za uovu hazimpati ila mwenyewe.1 Kuvunja ahadi, basi mwenye kuvunja ahadi anjivunjia ahadi mwenyewe.2 Ujeuri, enyi watu! Hakika jeuri yenu itawarudia nyinyi wenyewe tu.3

إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنْزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَنْ لَمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ {24}


Hakikamfanowamaishaya dunianikamamfanowamaji


tuliyoyate


r


emsh


a


kutoka mbinguni


,


kisha


ikachanganyika na mimea ya


ardh


i


wanayokul


a


wat


u


na


wanyama


.


Mpak


a


ardhi


ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika.Nawenyejiwake wakadhanikuwawananguvu juu yake, amri yetu iliifkia


usik


u


a


u


mchan


a


na


tukaifanya imefyekwa, kama


kwamb


a


jan


a


haikuweko.


Namnahiyotunazieleza


A


ya kwawatuwenyekufikiri.

وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ {25}


NaMwenyeziMunguanaita kwenyenyumbayaamani.Na


humwongoz


a


amtakaye


kwenyenjiailiyonyooka.

  • 1. (35:43)
  • 2. ( 48:10)
  • 3. (10:23)