Aya 24-25: Mfano Wa Maisha Ya Dunia
Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama mfano wa maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha ikachanganyika na mimea ya ardhi.
Yaani dunia hii mnayoshindana nayo na kujifaharisha inafanana na mvua iliyotermka ardhini, ikapata rutuba na kuotesha aina za mimea zikachanganyika kutokana na wingi wake na kukua kwake.
Wanayokula watu na wanyama
Kila kiumbe hai kinalishwa na ardhi, inajaza matumbo yaliyo na njaa. Watu wanakula nafaka na mtunda na wanyama wanakula nyasi na vinginevyo.
Mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika, kama harusi aliyejitengeza ili amfuruhishe harusi mwenzake,
Na wenyeji wake wakadhani kuwa wana nguvu juu yake na kuweza kutumia utajiri wake wakijaza mifuko yao na hazina zao. Baada ya mategemeo haya na kutulia amri yetu iliifkia ya maafa na maangamizi, usiku au mchana na tukaifanya imefyekwa, kama kwamba jana haikuweko, kutokana na kuondoka kila kitu, haikubaki hata alama ya vilivyokuwepo. matumaini yote na ndoto zote zimeyayuka.
Namna hiyo tunazieleza Aya kwa watu wenye kufikiri kuwa starehe za dunia zinaisha na kwamba mwenye kuzitegemea basi atakuwa ametege- mea kwenye mawingu na kwamba hakuna haja ya kumwagiana damu, kuanzisha vita na kuzidhalilisha akili za wajuzi.
Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye nyumba ya amani.
Wafasiri wamesema kuwa makusudio ya nyumba ya amni ni pepo. Hakuna mwenye shaka kuwa pepo ni nyumba ya wema na amani, lakini mwito wa Mwenyezi Mungu unaenea kwenye kila jambo litaklohakikisha raha kwa watu wake; bali Mwenyezi Mungu ameiharamisha pepo isipokuwa kwa watakaotumikia njia hii.
Na humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.
Mwito wa Mwenyezi Mungu wa kutenda heri, unamwenea kila aliye baleghe na mwenye akili timamu bila ya kumtoa yeyote. Basi atakayeasi na akaipuuza atakuwa amepotea na mwenye kutii akaitenda, atakuwa amaeongoka. Inafaa kutegemezwa uongofu wake kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu njia ya kuufuata ilikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
Ama upotevu wa aliyepotea, haifai kuutegemeza kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu ameukataza na Mwenyezi Mungu hawezi kukataza jambo kisha alielekeze lifuatwe.
لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ {26}
وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَا لَهُمْ مِنَ اللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ {27}
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنْتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُمْ مَا كُنْتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ {28}
فَكَفَىٰ بِاللَّهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِنْ كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ {29}
هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَا أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوا إِلَى اللَّهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ {30}
- 1642 views