read

Aya 26 – 30: Kwa Wafanyao Wema

Maana

Kwa wafanyao wema ni wema na ziyada.

Razi anasema kuwa mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ {60}


“Je,malipoyahisanisinihisanitu”(55:60).

Lakini ilivyo ni kwamba hisani inahusika na kumfanyia mtu mwingine, na wema ni ule unaopendeza kimaumbile, ni sawa uwe ni kumfanyia mwingine au la. Huo ni pamoja na itikadi njema, kauli njema vitendo vyema na nia njema; na hata kuhisi dhambi.

Yote hayo yanapendeza kwa Mwenyezi Mungu na kwa maumbile, naye Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ataulipa wema. Kwa hiyo basi Aya iko katika mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu.

وَمَنْ يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَزِدْ لَهُ {23}


“Naanayefanyawematutamzidishiawema…”(42:23).

Wametofautiana wafasiri katika maana ya ziada. Kwa sababu ikiwa ni katika aina ya wema basi si ziada na kama siyo basi neno litakuwa halijulikani. Lile tunalolifahamu ni kuwa makusudio ya ziada hapa ni kuwa yeye Mwenyezi Mungu mtukufu atawalipa wale waliofanya wema zaidi ya wanavyostahiki. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُمْ مِنْ فَضْلِهِ ۖ {173}


“Ama wale ambao wameamini na wakatenda mema,atawalipa ujira wao sawa,naatawazidishiakwafadhilayake”Juz.6(4:173)

Na vumbi halitafunika nyuso zao wala udhalili. Hao ndio watu wa Peponi; hao humo watadumu.

Kila kilichomo moyoni kiwe ni huzuni au furaha, amani au hofu, athari yake hudhihiri usoni wazi wazi, lakini athari ya hofu na kiherehere inadhi- hiri zaidi kuliko nyingineyo; hasa nyuso za watu wa motoni watakapouona. Zitasawajika kwa hofu; kama kwamba zimegubikwa na moshi au vumbi jeusi.

Ama watu wa Peponi nyuso zao zitacheka na kufurahi:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُسْفِرَةٌ {38}

ضَاحِكَةٌ مُسْتَبْشِرَةٌ {39}

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ {40}

تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ {41}


“Nyuso siku hiyo zitanawiri.Zitacheka na kufurahika.Na nyuso nyingin sikuhiyozitakuwanavumbi.Zimefunikwanaweusi.”(80:38

41)

Na wale waliochuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake.

Hakika Mwenyezi Mungu ni mwadilifu atamlipa anayefanya uovu anayostahiki; wala hatamdhulumu hata uzani wa sisimizi, bali atasamehe mengi. Kwa sababu yeye ni mkarimu; Na kwa ukarimu humwongezea mwenye kufanya wema ziada nyingi.

Na utawafunika udhalili.

Yaani fedheha itawafunika waovu. Hakuna mwenye kudhalilika na kufedheheka zaidi kuliko yule anayefed- heheka mbele ya watu.

Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.

Kuwalinda na machukivu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.

Kama kwamba nyuso zao zimefunikwa na kipande cha usiku wenye giza. Hao ndio watu wa motoni hao humo watadumu.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kusema kuwa watu wema hazitafu- nikwa nyuso zao na vumbi wala udhalili, anasema kuwa wale waovu nyuso zao zitasawajika, kama kwamba ni kipande cha usiku.

Imam Ali (a.s.) amesema: “Heri siyo heri ikiwa baada yake ni moto; na shari si shari ikiwa baada yake ni Pepo. Na kila neema isiyokuwa Pepo ni kazi bure na kila balaa isiyokuwa moto ni nafuu”.

Na siku tutakayowakusanya wote, wale walioefanya wema na, wale waliofanya uovu; kisha tuwaambie wale walioshirikisha: Simameni mahali penu nyinyi na washirika wenu.

Kesho watasimama kwa hisabu, washirikina na wale waliokuwa wakidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu; watakabiliana uso kwa uso ili kila kikundi kitoe dalili kwa hoja yake. Hapo yatayeyuka matumaini waliyokuwa wakiyatamani washirikina na kutaraji manufaa na itawabainikia kuwa wao walikuwa kwenye upotevu katika kushirikisha kwao na inadi yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na vitabu vyake.

Kisha tutawatenga baina yao

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.), siku ya Hisabu, atapambanua viumbe vyake vyote kwa sifa zao walizo nazo, na kudhihirisha hakika ya kila mmoja. Hapo itawabainikia washirikina kwamba hakuna yeyote anayeza kujidhuru yeye au mwingine au kujinufaisha na kwamba amri ni ya Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika wala mpinzani.

Na wao walioshirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.

Wakati Mwenyezi Mungu atakapowasimamisha, mahali pamoja, washirik- ina na wale waliokuwa wakiwaabudu, na kukabiliana uso kwa uso, wataambiana: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi; isipokuwa ni mawazo yenu kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika na kwamba sisi ndio hao washirika walio katika mawazo yenu tu. Kwa hakika nyinyi hamwabudu chochote, na sisi ni chochote; kwa hiyo hamtuabudu sisi.

Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yetu na nyinyi

Yeye anajua kuwa hao washirika mliowazua kwenye mawazo yenu hawako. Vile vile anajua kuwa sisi tuko mbali na huo ushirikina wenu.

Hakika sisi tulikuwa hatuna habari na ibada yenu.

Hatujui chochote. Hiyo ni kuashiria kukana kuabudiwa na kwamba wao ni waabudu sio waabudiwa.

Huko kila nafsi itajua iliyoyatanguliza na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa haki, na yote waliyokuwa wakiyazua yatawapotea.

Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu atawakusanya watu kuwahesabu na kumlipa kila mtu aliyoyachuma, wala hatakuta kile alichokuwa akikiitakidi na kukiwazia kuwa kinafaa na kumkinga; isipokuwa mtendo ya ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake. Maana haya yamekaririka kwa mifumo mbali mbali katika Aya kadhaa.

قُلْ مَنْ يَرْزُقُكُمْ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّنْ يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَنْ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَنْ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ {31}


Sema


:


Ninani anayewaruzuk


u


kutoka


mbinguninaardhini? Auni


nan


i


anayemilik


i


usikiz


i


na


uoni na ni nani amtoaye hai


kutok


a


mait


i


n


a


akamtoa


maiti kutoka aliye hai na ni


nan


i


anayedabir


i


mambo


yote?


W


atasemaniMwenyezi Mungu.


W


aambie: Basi je hamchi?

فَذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ {32}


Bas


i


huy


o


ndiy


e


Mweyezi


Mungu Mola wenu, tena ni nini baada ya haki isipokuwa


upotevu


?


Bas


i


mnageuzwa


wapi.

كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ {33}


Hivyo ndivyo lilivyothibiti nenolaMolawakojuuyawale waliofanya ufuska kwamba hataamini.

قُلْ هَلْ مِنْ شُرَكَائِكُمْ مَنْ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ قُلِ اللَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ {34}


Sema


:


Je


,


katik


a


Miungu yen


u


y


a


ushirikin


a


yuko anayeanzish


a


kuumba


viumb


e


kish


a


akaki


r


ejesha?


Sema


:


Mwenyez


i


Mungu


ndiye anayeanzisha kuumba


kiumb


e


kish


a


akaki


r


ejesha.


Basimnadanganywavipi?