read

Aya 3 – 4: Kuumba Katika Siku Sita

Maana

Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akatawala juu ya Arshi. Yeye hutengeneza mambo yote.

Siku za Mwenyezi Mungu si kama siku zetu hizi. Zingelitokea wapi siku kabla ya kuumbwa ulimwengu? Kwa hiyo makusudio ya siku hapa ni awamu au vipindi. Ama Arshi ni kutawala. Aya hii imetangulia pamoja na tafsir yake katika Juz. 8 (7:54)

Hakuna mwombezi ila baada ya idhini yake.

Vile vile hii imetangulia katika Juz.3 (2:255)

Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, basi mwabuduni.

Kwa sababu yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa. Ama mali, nasabu na ufalme sio Mungu wa kuabudiwa wala nguvu ya kunyeyekewa.

Je, Hamkumbuki?

Kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja peke yake anayestahiki kuabudiwa.

Hisabu Na Malipo Ni Lazima

Kwake yeye ndiyo merejeo yenu nyote.

Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli.

Hakika yeye ndiye anayeanzisha uumbaji kisha ataurejesha.

Suala la kuanzishwa na kurudishwa kiumbe ni moja ya mushkeli mkubwa wa kifalsafa. Watu wengine wanasema ulimwengu ulipatikana wenyewe tu bila ya kuweko mpatishaji.

Fikra hii ni sawa na mtu aliyeona mandishi, kisha aseme yamepatikana kibahati; kwa vile tu hakumwona mwandishi kwa macho yake. Yule aliyechora ulimwengu ni mkuu zaidi kuliko aliyechora msitari kwa wino juu ya karatasi.

Jicho ni duni sana kuweza kumwona; na akili zimemwona katikati njia zinazosababishia kumwamini.
Tumetunga vitabu viwili kuhusu njia hizo: Allahu Wal-aq’ na Falsafa Tul- Maad. Baadhi yake tumezielezea kwa ufupi katika Juz. 1 (2:21) na Juz. 4 (3: 190)

Ama kufufuliwa wafu, kurudishwa mara ya pili kwa hisabu na malipo kumeelezwa na wahyi na wala akili haikatai, kwa hiyo ni wajibu kuku- sadiki na kukuamini.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amebainisha hekima ya kurudishwa wafu kwa kusema:

Ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na waliokufuru, watapata kinywaji kinachochemka na adhabu chungu kwa vile walivyokuwa wakikufuru.

Mwenyezi Mungu amemwezesha mtu kutenda na akampa akili inayopambanua kheri na shari akamwamrisha hili na akamkataza lile. Basi akamtii mwenye kumtii na akamwasi mwenye kumwasi.

Kila mmoja akaingia shimo lake, bila ya kupewa thawabu mtiifu wala kuadhibiwa mwasi. Tena waasi wengi wanapetuka mipaka na kufanya dhulma na kuijaza dunia dhulma na jeuri bila ya kuulizwa na yeyote.

Tukichukulia kuwa hakuna ufufuo wala hisabu basi maana yake ni kuwa dhalimu na mdhulumiwa na mumin na kafir ni sawa, bali kafiri atakuwa ni bora kuliko mumin; na taghut mharibifu atakuwa mtukufu kuliko yule aliyekufa shahidi katika njia ya radhi yake.

Hakuna shaka kuwa haya yanapingana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na hekima yake na uwezo wake; bali hata na kuweko kwake Mwenyezi Mungu. Ametakata Mwenyezi Mungu na hayo kutakata kukubwa.

Tumeona wadhulimiwa wengi wakipiga kelele wakisema; Lau Mwenyezi Mungu angelikuwako kusingelibakii dhalimu yeyote katika ardhi.

Kauli hii haifahamishi chochote isipokuwa kuakisi matakwa ya kuweko mwadilifu mwenye uwezo atakayemchukulia kisasi mdhulumiwa. Lakini wamefanya haraka kwa uchungu, wakasahau maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu1, ndio wakasema waliyoyasema.

Nimeandika vitabu na makala kuhusu ufufuo, hisabu na malipo. Vilevile wakati wa kufasiri Aya inayoambatana na hayo. Na sasa Aya hii tena inanirudisha. Nimepata kufahamu kuwa dalili yenye nguvu ya kuthibitisha ufufuo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۚ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ {17}


“Leoitalipwakilanafsikwailiyoyachuma,hapanadhulmaleo.Hakika MwenyeziMungunimwepesiwakuhisabu.”(40:17)

Ayah hii ni kama Aya tuliyonayo, lakini hii iko wazi zaidi, inajichukulia dalili yenyewe na kujijibu. Inasema: Leo italipwa kila nafsi kwa iliyoyachuma, kwa nini? Kwa sababu hakuna dhulma kwa Mwenyezi Mungu bali yeye ni mwepesi wa kuhisabu.

Utatuzi wa kiakili wa suala hili ni kwamba lau sio siku hii ambayo kila mtu atalipwa, basi Mwenyezi Mungu angelikuwa dhalimu, kuweko kwake ni mateso na sharia zake ni mchezo: Ametakata Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na wanayombandika.

Kwa hiyo natija ya mwisho ya mantiki haya ni kwamba kila mwenye kukana ufufuo, hisabu na malipo atakuwa amekana kuweko Mwenyezi Mungu, atake asitake.

هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ {5}


Y


ey


endiy


e


aliyefany


a


jua


kuwa mwanga na mwezi kuwa nuru, na akaupimia vituo ili mjueidadiyamiakanahisabu. Mwenyezi Mungu hakuvium


b


a


hivy


o


il


a


kw


a


haki.


Anazipambanua


A


yakwawatu wanaojua.

إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَّقُونَ {6}


Hakik


akatik


akuhitalifiana


usiku na mchana na alivyoviumba Mwenyezi Mungu kati


k


a


mbing


u


n


a


ardh


i


kuna


isharakwawatuwamchao.

إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ {7}


Hakika wale wasiotaraji kuku- tana nasi na wakawa radhi na maisha ya dunia na wakatua nayo, na wale walioghafilika naisharazetu.

أُولَٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ {8}


Haomakaziyaonimotonikwa


sabab


u


y


a


yal


e


waliyokuwa


wakiyachuma.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُمْ بِإِيمَانِهِمْ ۖ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ {9}


Hakik


awal


ewalioamin


ina


wakatenda mema, Mola wao atawaongoza kwa sababu ya imani yao.Itapita mito chini yao katika Mabustani yenye neema.

دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ {10}


W


it


o


wa


o


hum


o


ni,


‘UmetakasikaeweMwenyezi Mungu!’Namaamkuziyaoni ‘Salaam’ namwishowawito waoni:‘Sifanjemazoteniza Mwenyezi Mungu Mola wa walimwenguwote.’

  • 1. Angalia Juz.7 (6:41) kifungu 'Mwenyezi Mungu na maumbile'