read

Aya 31 – 34: Ni Nani Anayewaruzuku?

Maana

Nguzo za imani ya haki kwa Mwenyezi Mungu ni tatu: Umoja, Utume na Ufufuo. Qur’ani imeonyesha aina mbali mbali za dalili ya nguzo hizi. Umetangulia ubainifu wake kwa ufanuzi pamoja na Aya hii tunayoifasiri sasa na iliyo baada yake.

Kwani Aya hizi zimekuja kubatilisha ushirikina na madai ya washirikina kuwa masanamu yao yanawakuribisha kwa Mwenyezi Mungu na kwamba hakuna ufufuo wala hisabu, na Qur’ani ni uzushi wa Muhammad kwa Mwenyezi Mungu. Yafuatayo ni kubadilisha madai hayo:

Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini?

Kila sababu miongoni mwa sababu za riziki, iwe yakaribu au mbali, haina budi kuwa ni ya mbinguni au ya kiardhi. Miongoni mwa sababu za mbingu ni mvua mwangaza na mengineyo ambayo wameyangudua wataalamu au watakuja kuyagundua. Na, katika sababu za ardhi ni mimea, wanyama na madini.

Sababu zote hizo zinarudia kwa Mwenyezi Mungu peke yake kupita desturi za kiulimwengu; kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu mtukufu ndiye muumbaji; na washirikina wanajua hakika hii na kukiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji mwenye kuruzuku.

Kwa hiyo hapa linakuja swali kuwa:

Enyi Washirikina! Maadamu mnaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji mwenye kuruzuku, vipi mnamfanyia washirika? Vipi kitu kinaweza kuwa mshirika, na inajulikana kuwa hakina athari naye kabisa? Je, inafaa wewe msomaji uwe mshirika wangu katika kutunga kitabu hiki, na mimi ndiye niliyefikiri, nikavumilia na kuandika?

Tumefafanua maudhui haya katika Juz. 5 (4: 48)

Au ni nani anayemiliki usikizi na uoni?

Mwenyezi Mungu amezihusisha hizi mbili, kwa sababu ndizo nyenzo za kwanza za kupata elimu; hata nadharia pia inatokana na hizo kwa sababu nadharia inakomea kwenye hisia na kuona. Razi anasema katika kufasiri Aya hii.

“Ali (r.a.) alikuwa akisema: “Utakatifu ni wa yule aliyeufanya uoni kwa shahamu na akaufanya usikizi kwa mifupa na akatamkisha kwa nyama”

Ni nani amtoaye hai kutoka maiti na akamtoa maiti kutoka aliyehai.

Yaani anayemiliki mauti na uhai. Miongoni mwa mifano ya kutoa hai kati- ka maiti ni vinavyoliwa na wanyama na kupitia matumboni kisha vinasagwa hatimae zinapatikana chembe mpya za uhai. Na mfano wa kutoa maiti katika hai ni kufa chembe ambazo zinatokana na mwili ulio hai kwa kupumua. Tumezugumza kwa ufafanuzi katika Juz.7 (4:95) kifungu cha ‘uhai umetoka wapi?’

Na ni nani anayeyadabiri mambo yote yaliyo katika ulimwengu?

Watasema ni Mwenyezi Mungu. Waambie basi je hamchi katika washirika mliowazusha?

Wao hawakatai kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja aliyepeke yake, anayeruzuku, anayemiliki usikizi, uoni, mauti, uhai, na mambo yote. Lakini pamoja na hayo wanamfanyia Mwenyezi Mungu washirika.

Siri ya mgongano huu ni kwamba wao wanamtazama muumba kwa mtazamo wa kimaudhui. Wameamini kuwa yeye ndiye muumba na mwenye kupatisha vitu vyote; kisha wakatazama yale yatakayowakurubisha kwake kwa mtazamo wa kimapenzi yao, wakakosea. Badala ya kujikurubisha kwake kwa vitendo na ikhlasi, wamemzuishia washirika na wakajikurubisha kwa hao wanaowashirikisha

Basi huyo ndiye Mweyezi Mungu Mola wenu, tena ni nini baada ya haki isipokuwa upotevu?

Hakuna usaidizi baina yao; ama haki na uongofu au batili na upotevu. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ndiye aliyeumba mbingu na ardhi ambazo ndani yake mna sababu za riziki. Na akaumba usikizi na uoni kwa haki ambazo ndio njia za elimu.

Na yeye anamiliki mauti na uhai kwa haki. Milki hiyo ni dalili ya uwezo na cheo. Naye ndiye mpangaji wa mambo kwa haki, ambako kunafahamisha elimu na hekima. Basi kuna nini tena baada haya yote isipokuwa upotevu, batili, ujinga na inadi.

Basi mnageuzwa wapi kuiacha haki na Tawhid na kufuata upotevu na kufuata shirk?

Hivyo ndivyo lilivyothibiti neno la Mola wako juu ya wale waliofanya ufuska.

Hiyo ni ishara ya yale yaliyotangulia kwamba hakuna baada ya haki isipokuwa upotevu. Makusudio ya neno la Mola wako hapa ni adhabu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

قَالُوا بَلَىٰ وَلَٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ {71}


“Lakinilimekwishathibitinenolahakikwamakafiri”(39:71).

Makusudio ya waliofanya ufuska ni washirikina. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu atawaadhibu washirikina, adhabu ya mwenye kuifanyia inadi haki na akakataa imani kabisa. Hiyo ndiyo stahiki yao kwani walipewa mwito wa Tawhid, zikawasimamia hoja na ubainifu, lakini pamoja na hayo walig’ang’ania shirki na wakafa nayo.

Sema: Je, katika Miungu yenu ya ushirikina yuko anayeanzisha kuumba viumbe kisha akakirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayeanzisha kuumba kiumbe kisha akakirejesha. Basi mnadanganywa vipi?

Yaani sema ewe Muhammad kuwaambia washirikina kuwa Mungu anaumba kitu bila ya kutumia kitu, anamrudishia uhai aliyekufa. Je hao mnaomshirikisha naye wanaweza hilo? Ikiwa hawawezi, basi inakuwaje mnaiacha Tawhid na kuifuata shirk?

Unaweza kuuliza kuwa hoja ya kuumba iko wazi kwa washirikina, kwa vile wanakubali hilo, lakini hoja ya kurudisha uhai haiko wazi na hilo ndilo jambo wanalolipinga, kuwa hakuna ufufuo. Sasa kuna wajihi gani hapo?
Jibu: Qur’ani katika Aya kadhaa imeleta hoja za kutosha kuhusu kurudishwa uhai na ufufuo kwa ujumla na washirikina wakashindwa kuzijibu. Kushindwa kwao huko ndiyo hoja iliyowalazimu; kwamba Mwenyezi Mungu atavirudisha viumbe kama alivyovianzisha.Kwa maneno mengine ni kuwa hukumu inasimama kwa dalili sio kusalimu amri yule anayehukumiwa.

قُلْ هَلْ مِنْ شُرَكَائِكُمْ مَنْ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ ۚ قُلِ اللَّهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَنْ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَنْ يُتَّبَعَ أَمَّنْ لَا يَهِدِّي إِلَّا أَنْ يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ {35}


Sema


:


Je


,


katik


a


Miungu


yenu ya ushirikina yuko aongozaye kwenye haki? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye aongozaye kwenye haki Basi je anayestahikikufuatwaniyule aongozaye kwenye haki au ni


yul


e


asiyeongok


a


isipokuwa


aongozwe


?


Bas


imn


a


nininyinyi?Mnahukumuvipi?

وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ {36}


N


a


weng


i


wa


o


hawafuati


isipokuwa dhana tu. Hakika dhana haifai kitu mbele yake


haki


.


Hakik


a


Mwenyezi


MunguniMjuzi wawanayoyatenda.

وَمَا كَانَ هَٰذَا الْقُرْآنُ أَنْ يُفْتَرَىٰ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَلَٰكِنْ تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ {37}


N


a


haikuw


a


Qu


r


’an


i


hii


imezushwa, kuwa haitoki kwa


Mungu


.


Lakin


i


inasadikisha


yaliyotangulia na ni ufafanuzi wa kitab. Haina shaka imeto


k


a


kw


a


Mol


a


w


a


viumbe


vyote.

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ {38}


Je, wanasema ameizuwa? Sema: Basi leteni Sura moja mfano wake na muwaite muwawezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyiniwakweli.

بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ ۖ فَانْظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ {39}


Bal


i


wamekadhibish


a


wasiy


oyajuaelimuyake.Kablahaujawajia ufafanuzi wake. Kadhalika walikanusha waliokuwa kabla yao Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwishowamadhalimu.