read

Aya 35 – 39: Mwenye Kuongoza Kwenye Haki

Sema: Je, katika Miungu yenu ya ushirikina yuko aongozaye kwenye haki?

Aya hii nikumfunga mdomo yule anayeabudu pamoja na Mwenyezi Mungu waungu wengine. Njia ya kufunga huko ni kwamba sifa ya kwanza anayotakikana kuwa nayo yule mwenye kuabudiwa ni kuwa yeye mwenyewe anaongoza kwenye haki bila ya kutegemea mwongozo wa mwingine. Ama yule asiyeongoza kwenye haki hastahiki uungu kabisa. Hakika hii ni wazi haina ubishi.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu amemwamrisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.w.) kuwahoji washirikina na kuwatupia swali hili, kwamba je, katika masanamu yenu haya mnayoyaabudu anapatikana anayeweza kuongoza kwenye haki? Hakuna mwenye shaka kwamba wao hawakuthubutu kujibu hili.

Kwa sababu masanamu yao ni mawe tu, waliyoyatengeneza kwa mikono yao, kwa vile Mtume (s.a.w.w.) anayo hoja mkataa kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayeongoza kwenye haki, ndipo akalielekeza swali hili kwao.

Sema: Mwenyezi Mungu ndiye aongozaye kwenye haki sio mwingine.

Na mwongozo huo ni wake mwenyewe hautokani na mwingine. Dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu anaongoza kwenye haki ni Mitume aliowatuma kwa waja wake wakitoa bishara na kuonya.
Vile vile vitabu alivyowateremshia ambavyo ndani yake mna Aya zinazobainisha ambazo zinawaon- goza watu kwenye shari yao na wema wao.

Huyu hapa Muhammad anawakabili washirikina ana kwa ana na aki- washinda kwa Qur’ani ambayo ndani yake mna ubainifu wa kila kitu.

Basi wako wapi wajumbe wa waungu wenu wa kishirikina? Viko wapi vitabu vyao. Lau Mwenyezi Mungu angelikuwa na mshirika, tungelimwona Mtume wake.

Ilivyo ni kwamba lengo sio kumlinganisha Mwenyezi Mungu, Mtume na masanamu, hapana! Ispokuwa lengo ni kuwaamsha washirikina na kuwazindua ujinga wao na upotevu wao, huenda wakazinduka.

Basi je anayestahiki kufuatwa ni yule aongozaye kwenye haki au ni yule asiyeongoka isipokuwa aongozwe?

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja utangulizi huu, hapa anabainisha natija yake, kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kufuatwa, si mwingine .

Natija hii anaidokeza kwa swali lenye jawabu lake; nalo ni: Ni nani anayestahiki kufuatwa na kuongoza? Je, ni Mwenyezi Mungu anayeongoza yeye mwenyewe au ni waungu wenu wa ushirikina wanaongozwa?

Unaweza kuuliza kuwa washirikina wa Makka wanaoambiwa maneno walikuwa wakiabudu masanamu na inajulikkana wazi kuwa masanamu hayo ni mawe ambayo hayawezi kuongozwa na walimu wala viongozi. Sasa kuna wajihi gani wa kauli ya Mwenyezi Mungu, ‘isipokuwa aongozwe?’

Wafasiri wamejibu kuwa hii ni haki ya kufaradhia na kukisia tu; yaani tufaradhie kuwa lau hayo masanamu yenu yangekuwa yanaongoza si ya takua hayo yenyewe yamefanywa kuongozwa? Na anayekuwa hivyo basi hafai kuwa Mwenyezi Mungu.

Jibu zuri ni kuwa Aya haikuwashukia washirikina wa Makka peke yao, bali imewashukia wao, na wale wanaoabudu watu au Malaika n.k.

Kwa hiyo maana yanakuwa, kila asiyeweza kuongoza, basi hastahiki kuwa Mungu ni sawa awe hana uwezo wa kuongoza hata kwa kuongozwa; kama mawe, au anaweza kuongoza baada ya kuongozwa; kama binadamu na Malaika. Wote hao hawastahiki kuwa Mungu.

Basi mna nini nyinyi? Mnahukumu vipi?

Mnaamini upotevu na hali dalili ya ubatilifu na ufisadi wake iko wazi

Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu.

Wengi wao ni washirikina. Kwa sababu kulikuwa na baadhi ya washirikina waliokuwa na yakini na kukubali ukweli na utume wa Muhammad na wakijua fika kuwa masanamu yao si chochote, lakini wakafanya inadi na kiburi kwa kuchunga masilahi yao na vyeo vyao. Ama wengine ambao ndio wengi walikuwa wakiabudu masanamu kwa kufuata na kuwaiga wazazi wao.

Mwenyezi Mungu ameitolea ibara ya dhana, ibada yao hii, pamoja na kuwa wenyewe walikuwa na yakini kuwa masanamu yao yanadhuru na kunufaisha.

Kwa sababu yakini yao hii haina msingi wa usahihi. Na kila yakini inayotegemea kuiga inafaa kuitolea ibara ya dhana. Tumefafanua zaidi kuhusu kufuata na kuiga tulipofasiri Juz. Baqara (2:170).

Hakika dhana haifai kitu mbele yake haki.

Makusudioa ya dhana hapa sio kutokuwa na uhakika, kama inavyoonyesha katika ibara iliyopita, isipokuwa makusudio yake hapa ni kuamini msingi wowote katika misingi ya dini au tawi katika matawi yake bila ya dalili ya kiakili au ya wahyi; hata kama imani hiyo itaaminiwa kiuhakika; kama vile kuiga washirikina katika kuabudu masanamu na ulahidi kabla ya kufanya utafiti na kuchunguza sababu za kuweko ulimwengu na kupatikana kwake na nidhamu iliyoko ndani yake. Je ilikuwa kwa sadfa au kwa mpango wa mwenye ujuzi na hekima?

Aya hii ni dalili wazi ya kupinga kiyasi (kukisia) na kuwa haifai katika masuala ya dini. Kwa sababu kiyasi ni kutumia dhana ambayo haifai kitu mbele ya haki katika misingi ya kiitikadi na hukumu za sharia.

Ama maswala ya dunia yako nje ya maudhui ya Aya. Vipi Mungu atakataza dhana katika kilimo, biashara na mafungamano ya kijamii. Lau watu wangelingoja elimu na yakini katika kila kitu basi maisha yangedumaa Hata hivyo haifai kumtuhumu mtu na kosa au kuwa shahidi ila baada ya kujua na kupata yakini. Siri ya hilo ni kuyapeleka maisha kwenye njia iliyo sawa.

Kwa ufupi katika mambo ya kidunia kuna maswala ambayo inafaa kufuata dhana na ambayo haifai kufuata dhana na mengine kuna hiyari. Mwenye kutaka kujua ufafanuzi wa hayo na asome kitabu Faraidil-Usul kinachojulikana kama Arrasul cha Sheikh mkuu, Al-Answari. Yeye amezama sana kwenye utafiti wa suala hili na ameandika karibu kurasa

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyatenda

Hili ni kemeo kwa washirikina ambao wanafuata dhana katika kuabudu masanamu na kumkadhibisha Mtume (s.a.w.w.) bila ya kuipima dhana yao hii kwa kipimo cha maumbile na akili. Vile vile ni kemeo kwa kila anayefuata dhana katika mambo ya dini.

Na haikuwa Qur’ani hii imezushwa kuwa haitoki kwa Mungu.

Kwa sababu ya mfumo wake wa ajabu na yale yaliyomo ndani yake; kama elimu, sharia ya watu, adabu za kijamii, kutolea habari mambo ya ghaib na mengineyo ambayo ni muhali kuwa hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini inasadikisha yaliyotangulia katika vitabu vya Mwenyezi Mungu.

Na ni ufafanuzi wa kitab.

Makusudio ya kitab hapa ni kila sharia aliyoiweka Mwenyezi Mungu ambayo binadamu anaihitajia kwa ajili ya wema wake wa dunia na akhera.

Haina shaka imetoka kwa Mola wa viumbe vyote.

Yaani haitakikani kwa mwenye akili kutia shaka katika Kitab cha Mwenyezi Mungu, kikiwa kimekusanya miujiza na Aya zinazokubalika na kila mwenye umbile safi na akili iliyo salama.

Je, wanasema ameizuwa? Sema: Basi leteni Sura moja mfano wake na muwaite muwawezao asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wa kweli.

Yametangulia maelezo yake kwa ufafanuzi zaidi katika Juz.1(2:23)

Bali wamekadhibisha wasiyoyajua elimu yake.

Ndivyo ilivyo kwa asiyejua, kufanya haraka kusadikisha na kukadhibisha, kabla ya kufanya uchunguzi.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu: ‘Wasiyoyajua elimu yake,’ ni ishara ya kwamba akili haiwezi kuthibitisha kitu au kukanusha ila baada ya kukisoma kwa utulivu kwa darasa kamili inayokusanya pande zake zote.

Kabla haujawajia ufafanuzi wake,

Yaani washirikina waliikanusha Qur’ani kabla ya kujua uhakika wake na siri zake. Lau wao wangeyatilia maanani mafunzo yake na hukumu yake, basi wangeliisadiki, ikiwa wanatafuta uhakika.

Imeelezwa katika Tafsir Majmaul-bayan: “Inasemekana kuwa Amirul- mumini, Ali (a.s.) alichukua kutokana na Aya hii kauli yake: ‘Watu ni maadui wa wasiyoyajua.’ Na kauli yake: ‘Thamani ya mtu ni yale anayoyajua,’ aliichukuwa katika Aya isemayo:

فَأَعْرِضْ عَنْ مَنْ تَوَلَّىٰ عَنْ ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا {29}

ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُمْ مِنَ الْعِلْمِ ۚ {30}


“Basi mwachilie mbali yule aupaye kisogo ukumbusho wetu na wala asitakeilamaishayadunia.Huondiomwishowaowaujuzi.”(53:29–30)

Na kauli yake isemayo: ‘Zungumzeni mtajulikana’ aliitoa katika Aya:

وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ ۚ {30}


“Nahakikautawafahamukwanamnayausemi.”(47:30).

Kadhalika walikanusha waliokuwa kabla yao; kama vile watu wa Nuh, Adi, Thamud nk, waliokanusha Mitume yao kabla ya kujua uhakika wa heri na mwongozo waliokuja nao.

Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu katika maangamizi na mabalaa.

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ {45}“Ikakatwamiziziyawatuwaliodhulumu;nasifanjemazoteniza


MwenyeziMunguMolawaviumbevyote.”(6:45)

وَمِنْهُمْ مَنْ يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُمْ مَنْ لَا يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ {40}


Na miongoni mwao wapo wanaoiamini, na miongoni mwao wapo wasioiamini. Na Mola wako anawajua sana wafisadi.

وَإِنْ كَذَّبُوكَ فَقُلْ لِي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنْتُمْ بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِمَّا تَعْمَلُونَ {41}


N


akam


a


wakikudhabisha,


basi sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyihamnajukumu kwa ninayoyatenda, na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.

وَمِنْهُمْ مَنْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنْتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ {42}


N


a


miongon


i


mwa


o


wapo wanaokusikiliza


.


Je


,


wewe


unaweza kuwasikilizisha viziwiingawahawafahamu?

وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنْتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ {43}


Na miongoni mwao wapo wanaokutazama. Je, wewe


unawez


a


kuwaogoz


a


vipofu


ingawahawaoni?

إِنَّ اللَّهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَٰكِنَّ النَّاسَ أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ {44}


Hakika MwenyeziMungu hadhulumu watu chochote,


lakin


i


wat


u


wanajidhulumu


wenyewe.