read

Aya 40 – 44: Miongoni Mwao Wapo Wanaoamini

Maana

Na miongoni mwao wapo wanaoiamini na miongoni mwao wapo wasioamini.

Dhamir katika miongoni mwao inarudi kwa washirikina na inayoaminiwa ni Qur’ani. Maana ni kuwa washirikina kwa mtazamo wa Kiqur’ani wako mafungu mawili: Kuna walioacha ushirikina na kuamini Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi. Kimsingi ni kuwa kuamini Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndio kumwamini Mohammad (s.a.w.w.).

Na wengine wameng’ang’ania ushirikina kwa inadi na kupupia manufaa. Hawa ndio wale aliowakemea Mwenyezi Mungu kwa kusema:

Na Mola wako anawajua sana wafisadi.

Hii inaonyesha kuwa neno mfisadi halimuhusu yule anayewafitini watu au kuwafanyia uovu bali linamuhusu kila aliyejua haki na asiitumie.

Na kama wakikudhabisha, basi sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa ninayoyatenda, na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.

Waumini wengi wameniuliza kuhusu jukumu lao kwa watoto wao waliopotea na wakaipuuza dini na hukumu yake.

Nikawajibu kuwa ni jukumu la mzazi kuwalea wanawe wadogo malezi ya kidini na awakuze kwenye misingi ya dharura ya dini, awaeleze misingi ya kiitikadi na kuwazowesha ibada za wajib; kama vile swala na saumu n.k. Vile vile kuwajulisha mambo ya haramu; kama uwongo, kusengenya, ulevi n.k.

Wakifikia makamo ya kujiongoza, basi awe kama muonyaji na mtoa bishara. Ikiwa hawataitikia mwito wake; basi yeye hana lawama mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kisha nikawasome Aya hii na Aya nyingine iliyo na maana hii na Hadith; kama kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wenu, basi atakaye na amini na asiyetaka na akatae” (18:29) Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) anasema:

“Mtoto ni bwana wa miaka saba na mtumwa wa miaka saba na waziri wa miaka saba. Tosheka na tabia yake kwa miaka 21 vinginevyo achana naye, umeshatekeleza majukumu yako kwa Mwenyezi Mungu”

Yaani mtoto ataachwa katika miaka saba ya mwanzo kwa sbabu ya udogo wake na atatiwa adabu katika miaka saba ya pili; kama mtu asiyekuwa na hiyari na ataelekezwa katika miaka saba ya tatu; kama mtu huru. Kusema achana naye ni kukata tamaa, na kwamba mzazi hana majukumu juu ya uovu wa mwanawe.

Na miongoni mwao wapo wanaokusikiliza.

Yaani katika washirikina au wanaokadhibisha wapo wanaomsikiliza Mtume (s.a.w.w.) kwa masikio tu. Ama nyoyo zao na akili zao ziko mbali naye, sawa na asiyesikia.

Je, wewe unaweza kuwasikilizisha viziwi, ingawa hawafahamu maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno yako ewe Mtume? Yule anayesikia na asifahamu au anayefahamu na asisikie, Mwenyezi Mungu amemweka daraja ya asiyesikia.

Kwa sababu lengo la hisia za kusikia ni kufaidika na kunufaika nazo. Ikiwa lengo hilo halikutimia, basi ni sawa na kutokuwepo hizo hisia.
Na miongoni mwao wapo wanaokutazama kwa macho yao lakini hawajui cheo chako na daraja yako ewe Mtume; kama kwamba hawana macho.

Je, wewe unaweza kuwaongoza vipofu ingawa hawaoni?

Yaani kama ambavyo huwezi kumfanya kiziwi asikie na kipofu aone, basi vile vile huwezi kumwongoza na Qur’ani yule anayekusikiliza na kukuangalia kwa sababu ya malengo yake na tamaa yake. Walisema wahenga: “Tamaa inapofusha na kufanya uziwi.”

Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu watu chochote, lakini watu wanajidhulumu wenyewe.

Hilo halina shaka kwani Mwenyezi Mungu amewapa uwezo na utambuzi, akawabainishia njia ya kheri na ya shari, akawakataza hili akawaamrisha lile na akawapa hiyari. Basi atakayemtii Mwenyezi Mungu atakuwa amejichagulia yeye mwenyewe kuokoka na atakaye asi atakuwa amejichagulia kuangamia.

Ni ajabu kuwa hakika hii imefichika kwa Ashaira na ikadhihirika kwa Iblis mlanifu, pale atakapowaambia wafuasi wake siku ambayo haitakuwa na ubishi wala hadaa:

فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنْفُسَكُمْ ۖ {22}


“Msinilaumubalijilaumuniwenyewe”(14:22).

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَنْ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ {45}


N


asik


uatakapowakusanya


itakuwa kama kwamba wao hawakukaa isipokuwa saa moja tu ya mchana.


W


atatambuana. Hakika


wamehasirik


a


waliokanusha


kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenyekuongoka.

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ {46}


Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayowaahidi au tukakufisha, basi ma


r


ejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni shahidi wawanayoyafanya.

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَسُولٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُمْ بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ {47}


Na kila Umma una Mtume Basi anapokuja Mtume wao inahukumiwa baina yao kwa uadilifu;naohawatadhulumiwa.