read

Aya 48 – 56: Ni Lini Ahad Hii?

Maana

Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?
Katika Aya 45, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewatishia wale wanaokad- hibisha kuwa watakutana naye, kwamba yeye atawafufua baada ya kufa na awaadhibu kutokana na kukadhibisha kwao. Katika Aya hii 48, Mwenyezi Mungu Mtukufu anaishiria kwamba wao wanajibu vitisho hivyo kwa dharau wakisema kuwa yatakuwa lini hayo?

Sema: Similikii nafsi yangu dhara wala nafuu, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu.

Yaani nyinyi mnaniuliza jambo ambalo sina uwezo nalo, bali sina uwezo hata wa nafsi yangu sembuse hayo mengine! Mfano wa Aya hii umetangulia katika Juz.9 (7:188).

Kila umma una muda. Unapofikia muda wao hawakawii saa moja wala hawatangulii.

Tumeeleza kwa ufafanuzi, kuhusu mfano wa Aya hiyo katika Juz.4 (3:145).

Sema: Mwaonaje ikiwafikia adhabu yake usiku au mchana. Sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wenye makosa?

Washirikina walikadhibisha adhabu ya Akhera, kisha wakaihimiza kwa dharau; ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwaambia kuwa Hebu niambieni mtafanya nini ikiwashukia adhabu mkiwa mko macho au mmelala, tena ni adhabu gani hiyo mnayoihimiza enyi wapumbavu? Je, mnangoja adhabu ya dunia au adhabu ya akhera? Vyovyote iwavyo, je, mnaweza kuikinga? Kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kumkimbia Mwenyezi Mungu?

Tena, Je, ikishatokea Mtaiamini?

Tumewashuhudia watu wengi wapumbavu wakijaribu kuikabili hatari au wakiacha mambo ambayo yana manufaa kwao. Wanapopewa nasaha na wenye akili na kuwahadharisha na mwisho mbaya, wao wanaziba masikio yao na kuwa na inadi ya kufanya uovu au kuacha kufanya heri wakidharau matokeo yake na yule anayewahadharisha. Inapofikia huanza kusema: ole wetu tulikuwa tukiambiwa sisi.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa wale wanaokadhibisha siku ya mwisho. Waliikadhibisha wakati ambao kuiamini kulifaa na wataiamini siku ambayo kuiamini hakuna manufaa yoyote, wamekwisha chelewa.

Sasa tena? Na hali mlikuwa mkiihimiza?

Je, mnaikubali na kuiamini hivi sasa ambapo hakuna manufaa yoyote ya kuiamini, wakati ambao mlitakiwa kuiamini, hamkufanya hivyo. Hakika kumwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ni kumwamini ikiwa ghaibu, lakini kuamini kiaga chake na siku ya mwisho baada ya kuiona, sivyo inavyotakiwa.

Kisha waliodhulumu watambiwa: onjeni adhabu ya kudumu.

Kifungo cha maisha, katika dunia, kinaishia kwa mauti. Ama kifungo katika Jahannam hakina mwisho, kwa sababu hakuna kufa wala adhabu yake haipunguwi.

Kwani hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyachuma?

Lau wangeliadhibiwa kwa yale wasiyoyachuma, Mwenyezi Mungu angelikuwa dhalimu. Ametakata ambaye ghadhabu zake hazimfanyi kuacha uadilifu wake.

Wallahi Wewe Muhammad Ni Mtume

Na wanakuuliza, Je, ni kweli hayo? Ya adhabu tuliyoahidiwa?

Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu hiyo ni kweli nanyi hamuwezi kushinda.

Qur’ani mara nyingi imetaja ishara na ubainifu juu ya utume wa Mohammad na ukweli wake wa kauli na vitendo. Miongoni mwa Aya hizo ni Juz. 1 (2:23), Juz. 3 (3:61), Juz.11(10:16) n.k.

Inajulikana kwamba Mtume alikuwa mkweli na mwaminifu kabla ya kutangazwa kuwa Mtume. Kwa hiyo mtu ambaye watu wamemjua kuwa ni mkweli na mwaminifu kwa muda wa miaka arobaini, basi ni juu yao kumwamini katika kauli zake zote mpaka uthibitike uongo wake.

Mwenye kumjua kwa sifa hizi anapaswa amwamini katika madai yake ya utume kwa kuchukulia kuwa Mohammad ni mwaminifu. Lakini tamaa manufaa na hawa za nafsi zinaingia kati ya mtu na akili yake na moyo wake.

Ama wale ambao wameepukana na matamanio ya nafsi na wakaitafuta haki kwa njia ya haki, basi waliamini kuanzia mwanzo. Miongoni mwao wako waliotosheka, kwa kusema tu: mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, bila ya kutaka ubainifu wala kiapo; kama vile Aliy bin Abu Talib. Wengine wakataka ubainifu na wengine wakatosheka kwa kuapa, kama vile Dhamam bin Tha’laba.

Wamesema wapokezi, akiwemo Imam ibn Hambal, Bukhari na Muslim: “Wakati Mtume alipokuwa msikitini, mara aliingia mtu, akaanza kusaili: Ninani Mohammad katika nyinyi? Akaelekezwa, wakaanza mahojiano. Yule mtu akanza kwa kusema: Mimi nitakuuliza maswali mengi kwa hiyo usinichoke.

Mtume: Uliza upendavyo.

Mtu: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa aliyekuwa kabla yako, Je, Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote:

Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu: Je, amekuamrisha kuswali swala tano, katika usiku na mchana?

Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu: Je amekuamrisha kufunga mwezi mmoja katika mwaka?

Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu: Je, amekuamrisha kuchukua sadaka kutoka kwa matajiri na kuigawanya kwa mafukara. Mtume: Ndio, kwa jina la Mola wangu.

Mtu: Nimeamini uliyokuja nayo, nami nitakuwa mjumbe kwa watu wangu. Mimi ni Dhamam bin Tha’laba ndugu wa Bani Sa’d bin Bakr.

Yule mtu akatoka Msikitini na alikuwa na nywele zenye misokoti miwili. Mtume akasema yule mtu akisadikisha, ataingia peponi.

Alipofika kwa watu wake maneno yake ya kwanza yalikuwa: Lata na Uza hawana maana. Watu wakasema: We! Dhamam nyamaza, usije ukapatwa na mbalanga na ukoma! Akasema: ole wenu! Hao hawadhuru wala kunufaisha. Hakika Mwenyezi Mungu amewaletea Mtume na amemteremshia Kitabu kitakachowaokoa na haya mliyokuwa nayo.

Na mimi Ninushahadia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee hana mshirika; na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na Mtume wake. Nimewaletea kutoka kwake yale mnayoamrishwa na mnayokatazwa.

Kama alivyosilimu yeye kirahisi, vilevile watu wake, waume kwa wake, walisilimu kirahisi.
Hivyo ndivyo alivyo kila ambaye matakwa yake na matamanio yake ni haki, anaiamini pale tu dalili yake inapomweka, kwa namna yoyote ile; sawa na apendaye kuwa kipofu. Ilikwishasemwa zamani: Hekima imempotea mumin, popote aipatapo huichukua. Makusudio ya mumin ni kila anayeiamini haki mara inapomdhihirikia bila ya taklifu yoyote wala mashaka.

Mwenyezi Mungu anasema:

وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ {58}

Na mji mzuri hutoa mimea yake kwa idhini ya Mola wake. Na ule ulio mbaya hautoi ila kwa taabu tu. Juz.8 (7:58)

Na lau kama kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo ardhini ingelitoa vyote kujikombolea kutokana na adhabu na ukali wake, lakini hakuna fidia yoyote itakayofaa isipokuwa imani na amali njema. Mwenyezi Mungu anasema:

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَا تَجْزِي نَفْسٌ عَنْ نَفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنْفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنْصَرُونَ {123}

“Na ogopeni siku ambayo nafsi haitafaa kitu nafsi nyingine, wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo; wala maombezi (shufaa) hayatafaa, wala hawatanusuriwa.” (2:123).

Na watakapoiona adhabu wataficha majuto lakini majuto, ya siri au dhahiri, hayafai kitu.

Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu; nao hawatadhulumiwa.

Aya hii, kama ilivyo, imetangulia katika Aya ya 47 ya Sura hii. Kule imetajwa kuwahadharisha wale wanaokadhibisha. Na hapa imerudiwa kuelezea kuwa hakuna faida ya fidia wala kikomboleo; hata kama ingeliwezekana kufanya hivyo.

Jueni kuwa hakika vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi ni vya Mwenyezi Mungu. Anahukumu na kufanya atakavyo wala hapana mwenye kuzuia matakwa yake.

Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni haki katika kuweko siku ya mwisho, thawabu zake, adhabu zake na kila kilichoahidiwa.

Lakini wengi wao hawajui kwamba Kiyama kitakuja, hakina shaka na kwamba Mwenyezi Mungu, atawafufua walio katika makaburi. Wengi wenye imani hii ya ufufuo hawaifanyii kazi. Ikiwa, kwa ujumla, wengi hawajui na wale wachache wajuao hawayatumii wanayoyajua, basi itakuwa wajuzi wanaoufanyia kazi ujuzi wao ni nadra kuliko dhahabu nyekundu.

Yeye ndiye anayefufua na anayefisha na kwake mtarudishwa ili aadhibiwe aliyejua, na asiutumie ujuzi wake, adhabu kubwa na kali kuliko ya yule aliyezembea kutafuta ujuzi. Ni kweli kuwa mzembe anajukumu, laki- ni jukumu la anayejua na asiutumie ujuzi ni kubwa zaidi.

Kuhangaika kutafuta mali kwa ajili ya kulipa deni ni wajib na mwenye kuacha atapata dhambi. Lakini dhambi ya mwenye kuacha na hali anayo mali ya kulipa ni kubwa na kali sana.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُمْ مَوْعِظَةٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ {57}

Enyi watu! Hakika yamewafikia mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na ponyo la yale yaliyomo vifuani mwenu na mwongozo na rehema kwa waumini.

قُلْ بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ {58}

Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, basi nawafurahi. Hayo ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ لَكُمْ مِنْ رِزْقٍ فَجَعَلْتُمْ مِنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّهِ تَفْتَرُونَ {59}

Sema: Je, mwaonaje zile riziki alizowateremshia Mwenyezi Mungu, kisha mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali? Sema: Je, Mwenyezi Mungu amewaruhusu au mnamzulia Mwenyezi Mungu uwongo?

وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ {60}

Nini dhana ya wale wanaomzulia uwongo Mwenyezi Mungu juu ya siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ana fadhila juu ya watu Lakini wengi wao hawashukuru.