read

Aya 5 – 10: Idadi Ya Miaka Na Hisabu

Maana

Yeye ndiye aliyefanya jua kuwa mwanga na mwezi kuwa nuru.

Imesemekana kuwa mwanga na nuru yana maana moja. Na ikasemekana kuwa maana yanatofautiana. Neno mwanga linafahamisha kuwa nuru yake haitegemei kitu kingine; na neno nuru lina maana ya kuwa nuru yake imetokana na kitu kingine; kama vile nuru ya mwezi iliyotokana na jua.

Lakini ilivyo ni kuwa Aya haikuja kubainisha chochote katika hayo, isipokuwa makusudio ni kutanabahisha umoja wake Mwenyezi Mugu na uwezo wake; sawa na Aya iliyotangulia; na kwamba hekima ya jua na mwezi ni ile aliyoashiria Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kauli yake:

Na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameufanyia mwezi vitu visivyobadilika wala kugeuka; sawa na desturi nyngine za maumbile. Makusudio ya kutogeuka huko ni kudhibiti nyakati ambazo uhai hauwezi kutimia ila kwazo.

Hayo tumeyazungumzia kwa ufafanuzi katika Juz.7 (6:96) na Juz.10 (9:36).

Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa haki. Anazipambanua ishara kwa watu wanaojua.
Mwenyezi Mungu amepambanua ishara za ulimwengu kimaumbile na kupatikana, na kwa kufafanua na kubainisha ili azingatie vizuri kila ambaye Mwenyezi Mungu amempa maandalizi ya kuchunguza na kutia akilini jambo ambalo linapelekea kumwamini Mwenyezi Mungu, uwezo wake na hekima yake.

Yametangulia maelezo, mara kadhaa, kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu hutegemeza dhahiri za kiulimwengu na mabadiliko kwenye desturi yake ya kimaumbile ili mtu, daima, abakie kukumbuka muumbaji wa yaliyo katika ulimwengu.

Hakika katika kuhitalifiana usiku na mchana na alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi kuna ishara kwa watu wamchao.

Umetangulia mfano wa Aya hii na tafsiri yake katika Juz.2 (2:164).

Hakika wale wasiotaraji kukutana nasi na wakawa radhi na maisha ya dunia na wakatua nayo, na wale walioghafilika na ishara zetu.

Aya hii ni kemeo na kiaga kwa yule asiyeamini akhera na hisabu yake, kwa kusema kuwa aliyekufa yake yamekwisha. Akiyasema haya kwa kusukumwa na hawa zake na matamanio yake akiwa ameghafilika na ulimwengu na yaliyomo ndani yake yakiwa ni pamoja na mazingatio mawaidha na mito ya Mitume na watu wema.

Hao makazi yao ni motoni kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

Haya ndiyo malipo ya kila mwenye kukadhibisha siku ya malipo na akayafanya matamanio yake ndiyo Mola wake, bila ya kujali haki wala uadilifu.

Ilivyo ni kuwa makemeo haya hayahusiki na mwenye kukana kukutana na Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo tu, bali yanamhusu pia yule mwenye kuamini kinadharia tu, lakini akakana kimatendo. Kwa hiyo wanaoswali na kufunga wakiwa wanaamini hisabu na adhabu, kisha wasichunge haramu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika Jahanam pamoja na wanaopinga hisabu.

Wako Wapi Wacha Mungu?

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao atawaongoza kwa sababub ya imani yao. Itapita mito chini yao katika Mabustani yenye neema.

Makusudio ya kuongozwa hapa ni thawabu; yaani Mwenyezi Mungu atawalipa thawabu kwa sababu ya imani yao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.), katika Aya zilizotangulia, amewataja wapinzani na sifa zao na mwisho wao. Katika Aya hii anawataja waumini, sifa zao na mwisho wao; kama desturi yake Mwenyezi Mungu Mtukufu yakutaja vitu na vinyume vyake.

Kwa hiyo waumini wako kinyume na wapinzani, wanatarajii kukutana na Mwenyezi Mungu, wanachunga miko yake kwa mujibu wa dini yao na imani yao. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawapa thawabu ya Pepo ipitayo mito chini yake.

Yamekuja maelezo katika Hadith kuwa Muumba, Mwenyezi Mungu Mtukufu, atasema siku ya Kiyama: “Leo nitaondoa nasabu yenu na niweke nasabu yangu. Wako wapi wacha mungu? Huo ndio mwito wa Mwenyezi Mungu siku hiyo ya haki ‘wako wapi wacha Mungu, walio wakweli katika kauli zao wenye ikhlasi katika vitendo vyao’. Ama mwito wa shetani hapa duniani, nyumba ya dhulma na ufisadi, ni: Wako wapi mataghuti wanaovunja miko walio wafisadi?

Kila mwenye kumtukuza mumin kwa sababu ya imani yake na takua yake, basi atakuwa ametoa mwito wa Mwenyezi Mungu ‘wako wapi wacha Mungu’ Na kila mwenye kumheshimu taghuti kwa makosa yake, basi atakuwa ametoa mwito wa Sheitan ‘wako wapi wakosaji’
Imam Ja’far As-Swadiq (a.s.) anasema: “Ni makruh kumsimamia mtu kwa kumheshimu ila mtu wa dini” Na akasema tena: “Usibusu mkono wa yoyote ila mkono wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) au wa anayekusudiwa kwaye Mtume (s.a.w.).

Hukumu ya kumheshimu mtu inatofautiana kulingana na hali ilivyo. Ikiwa ni kwa kutia mori wa dhambi na maasi ya Mwneyezi Mung basi ni haramu. Ikiwa ni kwa mapenzi na mshikamano au kutekeleza haja ya mhitaji basi ni kuzuri.

Ama kumheshimu na kumtukuza mpigania jihadi kwa juhudi yake, mwenye ikhlasi kwa ikhlasi yake, msuluhishaji kwa suluhu yake na ulama kwa elimu yake, basi hiyo ni katika kuadhimisha nembo za Mwenyezi Mungu na miko yake, ambako amekuashiria kwa kusema:

وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ {32}


“Na anayezitukuza alama za Mwenyezi Mungu, basi hilo ni katika uchaji waMoyo”(22:32).

وَمَنْ يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ عِنْدَ رَبِّهِ ۗ {30}


“Na anayevitukuza vitu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu, basi hiyo ni heri kwakembeleyaMolawake…” (22:30).

Wito wao humo ni ‘Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu! Na maamkuzi yao ni ‘Salaam’ na mwisho wa wito wao ni: ‘Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu Wote.’

Aya hii kwa ujumla inaelezea habari za watu wa Peponi wakiwa katika raha hawashughlishwi na lolote katika yale yaliyokuwa yakiwashughulisha duniani ya kutaka masilahi au kukinga madhara; hawataki uadilifu wala amani, au kuzidishiwa malipo na cheo.

Hawataki chochote kwa sababu kila kinachotamaniwa na nafsi na kuburudisha macho kiko tayari; wakitaka kitu kazi yao ni kukifikiria tu katika nyoyo zao.

Kwa ajili hiyo wanajishughulisha na Tasbih na Tahmid tu:

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا {25}

إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا {26}


“Hawatasikia humo porojo wala maneno ya dhambi, isipokuwa maneno: Salaam,Salaam”.
(56:25

26).

Salam hii waliisikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu walipokutana naye:

تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ ۚ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا {44}


“MaamkuziyaosikuyakukutananayeyatakuwaniSalaam”(33:44)

Salaam hiyo wataisikia kutoka kwa Malaika:

وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ {73}


“Nawalinziwakewatawaambia:SalaamunAlaykum,furahini,iingieni mkaemilele”(39:73).

Na, pia wataamkiana wenyewe kwa wenyewe.

Tumezungumzia kuhusu Maamkuzi ya Kiislam katika Juz.7 (6:54)

وَلَوْ يُعَجِّلُ اللَّهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُمْ بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ {11}


LauMwenyeziMunguangeli


waharakishi


a


wat


u


shari, kam


a


wanavyoharakishia


kheri, hakika wangelikwisha


timiziw


a


mud


a


wao


.


Basi


tunawaacha wale wasio taraji kukutana nasi wakihangaika katikaupotevuwao.

وَإِذَا مَسَّ الْإِنْسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنْبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَنْ لَمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَسَّهُ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {12}


N


a


dhar


a


inapomgus


amtu


hutuomb


a


nay


e


ameegesha


ubavuwake,aukatikahaliya kukaa, au katika hali ya kusi


mama


;


lakin


i


tunapomwon


dolea dhara yake huendelea


kam


a


kwamb


a


hakupata kutuomb


a


tumwondolee


dhara iliyomgusa. Namna hii


wamepambiw


a


wapetukao mipak


a


yak


e


waliyokuwa


wakiyatenda.

وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا ۙ وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ {13}


Hakik


a


tumekwishaziangamiz


a


kaum


u


za


kabla yenu walipodhulumu;


n


a


waliwaji


a


Mitum


e


wao


kwa hoja zilizo wazi, lakini


hawakuw


a


weny


e


kuamini.


Namna hii tunawalipa watu wakosefu.

ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِنْ بَعْدِهِمْ لِنَنْظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ {14}Kish


a


tukawafany


a


nyinyi ndi


o


mnaowafuati


a


baada


yaokatikaardhiilituonejinsi mtakavyotenda.