read

Aya 5: Wanakunja Vifua Vyao

Dhamir ya ‘hakika wao’ ni ya washirikina na ya ‘anayemficha’ ni Mtume

Muhammad (s.a.w.). Maana ya Aya ni kuwa baadhi ya watu walikuwa wakikunja nyoyo zao kwa kumfanyia chuki na uadui Mtume Muhammad (s.a.w.), na hilo walikuwa wakilificha. Lakini Mwenyezi Mungu akaiifichua hakika yao na kwamba yeye Mwenyezi Mungu mtukufu anajua yaliyo nyoyoni mwao na hali yao yote kwa ujumla, na yeye atawaadhibu kutokana na makusudio yao.