read

Aya 61 – 64: Huwi Katika Jambo Lolote

Maana

Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur’ani, wala hamtendi kitendo chochote ila sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nacho.

Msemo katika huwi unaelekezwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.) na katika hamtendi unaelekezwa kwa Mtume na uma wake. Maana kwa ujumla ni kuwa hakuna hali yoyote anayokuwa nayo Mtume na uma wake isipokuwa Mwenyezi Mungu anajua.
Na hakifichikani kwa Mola wako chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.

Kitab kinachobainisha ni Lawhin Mahfudh. Kwa ufupi Aya inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, Mjuzi, wa kila kitu. Na makusudio ya kujua kwake hapa ni malipo kwenye kauli za watu na vitendo vyao vya heri au vya shari, vikubwa au vidogo.

Juweni kuwa mawalii wa Mwenyezi Mungu hawana hofu wala wao hawahuzuniki.

Imam Ali (a.s.) anasema katika wasifu wake kwa vipenzi (mawalii) wa Mwenyezi Mungu: “Hao ni wale ambao wameiangalia dunia kwa undani wakati watu wameiangalia kwa nje. Wamejishughulisha na wakati ujao wakati watu wamejishughulisha na wakati wa sasa. Wakaua yale wanayohofia kuwauwa – yaani hawa-na wakaacha katika dunia yale ambayo wanajua kuwa yatawaacha.”

Amesema tena: “Hakika bora wa watu kwa Mitume ni yale anayejua zaidi yale waliyokuja nayo; na kwamba mpenzi wa Muhammad ni yule anayemtii Mwenyezi Mungu, hata kama mwili wake utakuwa mbali naye na adui wa Muhammad ni yule mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu hata kama atakuwa karibu naye kiudugu.”

Maana ya yote hayo ni kuwa kuamini bila ya kumcha Mwenyezi Mungu na vitendo hakuna manufaa yoyote. Ndio Mwenyezi Mungu akaashiria kwa kusema:

Hao ni ambao wameamini na wakawa na takua.

Tumeyafafanua zaidi hayo katika Juz. 2 (2:212) na Juz.4 (3:200)

Wao wana bishara katika maisha ya dunia na katika Akhera.

Wao ni wacha Mungu, na bishara yao katika dunia inatoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume kwamba wao wako katika haki ya itikadi yao na matendo yao. Hapana mwenye shaka kwamba nafsi inatulia na kuona raha, ikiwa ina imani na dini yake na matendo yake.

Ama bishara ya wanaomcha Mwenyezi Mungu katika Akhera ni furaha yao kwa neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake.

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ {171}

Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa waumini.” (3:171).

Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake, na anapotaka kitu hakuna wa kupinga matakwa yake.

وَإِنْ يَمْسَسْكَ اللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِنْ يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ {107}

“Na kama Mwenyezi Mungu akikugusisha dhara hakuna wa kuiondoa isipokuwa yeye tu na kama akikutakia heri, basi hakuna mwenye kuirudisha fadhila zake.” (10:107)

Huko ndiko kufuzu kukubwa, ambako hakuna kufuzu kwengine zaidi yake. Kila kufuzu kunakotokana na natija ya kuamini haki na jihadi katika njia yake, basi huko ni kufuzu kukubwa.

وَلَا يَحْزُنْكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ {65}

Wala isikuhuzunishe kauli yao. Hakika enzi yote ni ya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye
mwenye kusikia, Mjuzi,

أَلَا إِنَّ لِلَّهِ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَمَنْ فِي الْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ شُرَكَاءَ ۚ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ {66}

Juweni kuwa ni wa Mwenyezi Mungu wote waliomo mbinguni na waliomo ardhini. Na wale wanaoomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu hawawafuati kuwa ni washirika, hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo tu.

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَسْمَعُونَ {67}

Yeye ndiye aliyewafanyia usiku ili mtulie humo na mchana wa kuonea. Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaosikia.

قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ الْغَنِيُّ ۖ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنْ عِنْدَكُمْ مِنْ سُلْطَانٍ بِهَٰذَا ۚ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ {68}

Wanasema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto! Ametakata na hayo! Yeye ni mkwasi. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nyinyi hamna dalili kwa haya. Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua?

قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ {69}

Sema: Hakika wale ambao wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo hawatafaulu.

مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ {70}

Ni starehe katika dunia. Kisha marejeo yao ni kwetu, tena tutawaonjesha adhabu kali, kwa sababu walikuwa wakikufuru Mungu.