read

Aya 97 – 99: Mabedui Wamezidi Sana

Ushamba Na Kuendelea

Mabedui wamezidi sana katika kufuru na unafiki na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Hii haina maana ya kuwagawanya watu kwenye ushamba na kuendelea kuwafanya bora watu wa mjini kuliko mabedui. Vipi? Iwe hivyo na hali Mwenyezi Mungu, katika Aya inayofuatia, anaelezea kuwa kuna watu katika mabedui wenye ikhlasi katika imani yao na matendo yao.

Kama ingelikuwa ubedui ni dhambi basi angeliuharamisha, sawa na alivyoharamisha dhulma. Na Qur’ani huwagawanya watu kwa misingi ya takua, yaani kumwamini Mwenyezi Mungu na amali njema, na imebainisha hakika hii na kuisisitiza kwa mifumo mbali mbali, bali hakika hiyo ndiyo lengo la kwanza na la mwisho la kuteremsha Qur’ani, mwito wake, mafunzo yake na sharia yake.

Aya hii tuliyo nayo inaashiria hilo kwani kauli yake hiyo Mwenyezi Mungu:

“Mabedui wamezidi sana katika kufuru na unafiki” inafahamisha kuwa sababu ya kutukanwa ni ukafiri na unafiki na kutojua hukumu za Mwenyezi Mungu alizoteremsha kwa Mtume wake, na wala ubedui sio sababu ya kutusiwa.

Ni kweli kuwa maisha ya ubedui (ushamba) na kuwa kwake mbali na maendeleo na maarifa, yanasababisha tabia ngumu na ya ovyo na kukeuka mipaka, lakini hilo ni kosa la mazingara sio kosa la ubedui. Kuna hadith isemavyo ifahamuni halali na haramu, vinginevyo basi nyinyi ni mabedui.” Yaani mtakuwa kama wao katika ujinga na kuwa mbali na maendeleo.
Baada ya utangulizi huu, sasa turudie kwenye Aya. Maana yaliyo kusudiwa katika Aya ni kuwa katika mabedui kuna makafiri na wanafiki sawa na wakazi wa mjini, isipokuwa makafiri wa kibedui na wanafiki wao ni zaidi kuliko wengine katika wakazi wa mjini.

Hayo ndio maana yanayopatikana katika dhahiri ya Aya, nasi tunaongezea kwamba ikiwa sababu inayowajibisha hilo ni ugumu wa tabia basi vile vile watakuwa ni wenye imani zaidi wakiamini na wenye ikhlasi zaidi watakapokuwa na ikhlasi, kwa vile sababu ni moja.

Kwa mnasaba huu tunadokeza maelezo yaliyokuja katika Kitabu Mizan Sha’rani, mlango wa Shahada, ninamnukuu: “Hambali hawakubali ushahidi wa bedui dhidi ya mtu wa mjini na Malik anaukubali katika kujeruhi na kuua tu, lakini sio katika haki nyingine”.

Tunajua wajihi wa anayesema kuwa haukubaliwi ushahidi wa asiyekuwa Mwislamuu dhidi ya Mwislamuu. Lakini kumlinganisha Bedui mwislamu na asiye kuwa mwislamu katika ushahidi, hatujui kumepitiwa njia gani. Mwenyezi Mungu anasema:

وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِنْكُمْ {2}

“Na mshuhudishe mashahidi wawili waadiilifu miongoni mwenu” (65:2)

na wala hakusema katika wakazi wa mjini. Linalozingatiwa katika kukubaliwa ushahidi ni uadilifu sio ushamba wala kuendelea.

Miongoni mwa mabedui wako wanaochukulia kuwa wanayoyatoa ni gharama ya bure.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja kuwa miongoni mwa mabedui wako wanafiki, hapa anataja kuwa wao wanatoa mali zao, lakini wanaona kutoa huku ni gharama za bure sizizokuwa na faida, na kwamba thawabu na malipo yake siku ya Kiyama ni mambo ya kubandikwa tu.

Na wanawangojelea misiba.

Wanangonjea maadui wawashinde waislamu na wanatamani wamalizwe ili wapumzike na gharama hii ya hasara, kama wanavyoitakidi.

Misiba mibaya itakuwa juu yao.

Kuna kundi katika wafasiri wanaosema kuwa hii ni dua kwa wanafiki kuwa yawapate yale wanayowatamania Waumini. Pia inawezekana kuwa ni kutolea habari hali ya adhabu watakayokuwa nayo wanafiki siku ya Kiyama.

Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi Mjuzi,

Anasikia wanayoyasema na anajua wanayoyaficha.

Miongoni mwa mabedui wako wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na wanachukulia wanayoyatoa ndiyo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu na dua za Mtume.

Mabedui ni kama watu wengine wako wanafiki wanaonyesha yasiyokuwa katika nyoyo na kuona wanayoyatoa ni gharama za bure sio wajibu; kama ilivyodokeza Aya iliyotangulia.

Na miongoni mwao wako Waumini wenye ikhlasi wanaotoa kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabu zake na kutaka dua ya Mtume ya kupata baraka na maghufira, kama ilivyoashiria Aya hii.

Sikilizeni! Hakika hayo ni mambo ya kuwasogeza. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.

Dhamiri ya hayo ni yale wanayoyatoa; yaani kutoa huko kunakurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Maana ni kuwa wale walioamini wakatoa kwa kutaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atakubali kutoa kwao; atawaingiza katika pepo yake na atawasamehe makosa waliyotekeleza na kuyakosa.

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ {100}


Nawaliotanguliawakwanza


katik


a


wahajir


i


n


a


Ansari.


Na wale waliowafuata kwa


wema


.


Mwenyez


i


Mungu


yuko radhi nao na wao wako


radh


i


naye


;


n


a


amewaan


dalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

وَمِمَّنْ حَوْلَكُمْ مِنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُمْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ {101}


Namiongonimwamabedui walio pambizoni mwenu wamo wanafiki na katika wenyeji wa Madina wako waliobobea katika unafiki. Huwajui, sisi tunawajua.


T


utawaadhib


u


mar


a


mbili,


kisha watarudishwa kwenye adhabukubwa.

وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّهُ أَنْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ {102}


Nawenginewamekiridham


b


i


zao


;


wakachanganya vitend


o


vyem


a


n


a


vingine viovu


.


Huend


a


Mwenyezi


Mungu akapokea toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni


Mwing


i


w


a


msamaha,


Mwenyeku


r


ehemu.