read

Sura Ya Ishirini Na Tano: Al-Furqan

Imeshuka Makka. Ina Aya 77.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا {1}

Amekuwa na baraka yule ambaye ameiteremsha Furqani kwa mtumwa wake, ili awe muonyaji kwa walimwengu wote.

الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُنْ لَهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا {2}

Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakufanya mtoto, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na ameumba kila kitu na akikadiria kipimo.

وَاتَّخَذُوا مِنْ دُونِهِ آلِهَةً لَا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ وَلَا يَمْلِكُونَ لِأَنْفُسِهِمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَلَا يَمْلِكُونَ مَوْتًا وَلَا حَيَاةً وَلَا نُشُورًا {3}

Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii dhara wala nafuu, wala haimiliki mauti wala uhai wala kufufuka.

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا إِفْكٌ افْتَرَاهُ وَأَعَانَهُ عَلَيْهِ قَوْمٌ آخَرُونَ ۖ فَقَدْ جَاءُوا ظُلْمًا وَزُورًا {4}

Na wamesema wale ambao wamekufuru: Haikuwa hii ni chochote ila ni uzushi aliouzua, na wamemsaidia haya watu wengine. Basi hakika wamekuja na dhulma na uzushi.

وَقَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ اكْتَتَبَهَا فَهِيَ تُمْلَىٰ عَلَيْهِ بُكْرَةً وَأَصِيلًا {5}

Na wakasema: Hizi ni ngano za wa kale anazoziandikisha anazosomewa asubuhi na jioni.

قُلْ أَنْزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا {6}

Sema, ameiteremsha ajuaye siri za mbinguni na ardhini. Hakika Yeye amekuwa ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu