read

Aya 51-60: Ibrahim

Maana

Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uongofu wake zamani na tulikuwa tunamjua.

Wametofautiana wafasiri kuhusu maana ya uongofu. Ikasemekana kuwa ni kuongoka kwenye utengenefu wa dini na dunia. Pia ikasemekana kuwa ni utume.

Kauli hii ndiyo yenye nguvu zaidi kwa dalili ya kauli ‘zamani’ maana yake ni kabla ya mitume waliokuja baada ya Ibrahim (a.s.); kama vile Musa (a.s.), Isa (a.s.) na Muhammad (s.a.w.). Pia kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu ‘Na tulikuwa tunamjua’ ambayo maana yake ni kauli yake:

اللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ {124}

“Mwenyezi Mungu diye Mjuzi zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbe wake.” Juz. (6:124).

Utume unatoka kwa Mungu, anamuhusisha nao mwenye kuustahiki, wala haupatikanai kwa bidii ya mtu; kama vile imani na takua. Ndio maana husemwa kuwa mumin, kuwa mcha Mungu, lakini haisemwi kuwa Mtume.

Alipomwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayoyanga’ng’ania?
Swali hili linaelekezwa kwa kila mwenye majukumu ya matendo yake na matumizi yake. Vipi mnavitukuza na kuviabudu visivyodhuru wala kunufaisha; na nyinyi mna akili na utambuzi?

Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.

Mantiki hii anaikimbilia kila mwenye kushindwa na hoja na dalili. Ukimuuliza kwa nini umefanya hivi, atasema: Fulani amefanya.

Hakuna la kuwaambia watu wa aina hii, isipokuwa kauli ya Nabii Ibrahim:

Akasema: Hakika nyinyi na baba zenu mmekuwa kwenye upotofu ulio dhahiri.

Na upotofu hauwezi kubadilika kuwa uongofu hata ukifuatwa na wengi.

Wakasema: Je, umetujia kwa haki au wewe ni katika wafanyao mchezo?

Walijitia mshangao kutokana na kauli ya Ibrahim, kwa vile wanawaona baba zao wametakaswa na makosa; si kwa lolote ila ni kwa kuwa ni baba zao tu.

Mantiki haya hawahusiki nao kaumu ya Ibrahim tu, wala washirikina wengine; bali kila mwenye kuigiza wengine kwa upofu, yuko sawa na waabudu masanamu.

Akasema: Bali Mola wenu ni Mola wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliyeziumba,

Mimi sifanyi mchezo wala sitii shaka. Vipi nifanye mchezo na kutia shakashaka na hali Yeye ndiye muumba wa mbingu na ardhi na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo?

Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu baada ya kunipa mgogo.

Ilivyo ni kwamba masanamu hayawezi kufanyiwa vitimbi, kwa sabau hayana hisia; isipokuwa wanaofanyiwa vitimbi ni waabudu masanamu, kwa hiyo kuyafanyia vitimbi ni majazi, sio hakika; isipokuwa yamefanywa ni nyenzo ya kufanyiwa vitimbi wanaoyaabudu.

Basi akayavunja vipande vipande isipokuwa kubwa lao ili wao walirudie.

Ibrahim aliyavunja masanamu yote na akaliacha lile kubwa lao, ili wale wanaoyaabudu waliulize, kwa nini halikuweza kuwatetea wenzake wadogo nalo lina nguvu? Makusudio yako wazi; nayo ni kuwa washirikina wazingatie kuwa masanamu haya ikiwa hayo yenyewe hayawezi kujitetea, basi ndio hayawezi kumtetea mwengine.

Wakasema: Ni nani aliyeyafanyia haya miungu wetu? Hakika huyu ni katika madhalimu.

Usawa ni kuwa waulize miungu yao imemfanyia nini aliyeyavunja? Lakini haya ndiyo mantiki ya kijinga na kuiga.

Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.

Hii inaashiria kauli ya Ibrahim (a.s.): “Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu.”

Baada ya kuandika Juzuu ya sita, nilisoma kwenye mojawapo ya magazeti, kwamba wafukuaji, wamegundua mji wa kwanza wa Ibrahim, Uru. Ikabainika kwamba watu wake walikuwa wakiabudu nyota tatu: ndogo, wastani na kubwa.

Kwa hiyo mpangilio huu uliokuja katika Qur’an kupitia ulimi wa Ibrahim ndio mpangilio wa kimantiki ambao unafuatana na maisha ya wakati huo. Hivi ndivyo elimu inavyoleta dalili kila siku juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w.) katika kila aliyoyaeleza.

قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ {61}

Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu, wapate kumshuhudia.

قَالُوا أَأَنْتَ فَعَلْتَ هَٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ {62}

Wakasema: Je, wewe ndiwe uliyeifanyia haya mingu yetu ewe Ibrahim?

قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِنْ كَانُوا يَنْطِقُونَ {63}

Akasema: Bali ameyafanya hayo mkubwa wao huyu. Basi waulizeni ikiwa wanatamka.

فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنْفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنْتُمُ الظَّالِمُونَ {64}

Basi wakajirudi nafsi zao. Wakasema: Hakika nyinyi ndio madhalimu.

ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَٰؤُلَاءِ يَنْطِقُونَ {65}

Kisha wakasimamia vichwa vyao. Wewe unajua kwamba hawa hawasemi.

قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لَا يَنْفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ {66}

Akasema: Basi nyinyi mnaabudu badala ya Mwenyezi Mungu visivyo wanufaisha kitu wala kuwadhuru?

أُفٍّ لَكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ {67}

Kefule yenu na mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Basi hamtii akili?

قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانْصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ فَاعِلِينَ {68}

Wakasema: Mchomeni na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo.

قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ {69}

Tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!

وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ {70}

Na wakamtakia ubaya, lakini tukawafanya wao ndio wenye kupata hasara.