read

Aya 58 – 64: Waliohajiri

Maana

Wale ambao wamehajiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakuawa au wakafa, bila shaka Mwenyezi Mungu atawaruzuku riziki njema. Na hakika Mwenyezi Mungu ni mbora wa wanaoruzuku.

Hijra (kuhama) katika njia ya Mwenyezi Mungu ziko aina nyingi. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:-

• Kuhama mtu kwao kwenda kupigana jihadi na madhalimu na wapotevu.

• Kukimbia mtu na dini yake kuepuka vikwazo vya kumzuia kutekeleza wajibu wake.

• Kuhama kwa ajili ya kutafuta elimu ya dini kwa ajili ya dini, kutafuta riziki halali au kutekeleza faradhi ya Hijja.

Yeyote miongoni mwa hawa na mfano wao, akiuawa au akifa katika kuhama kwake huko, basi atastahiki, mbele ya Mwenyezi Mungu, kupata malipo na riziki njema, kama wanavyostahiki mashahidi. Tumezungumzia Hijra kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 4 (3: (190 -195) na Juz.5 (97-100).
Bila shaka atawaingiza mahali watakapoparidhia, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mpole.

Makusudio ya mahali hapa ni Peponi. Kwa dhahiri ni kuwa mwenye kuiingia hataridhia pengine zaidi ya hapo.

Ndivyo hivyo.

Yaani hivyo alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamba mwenye kuhama katika njia yake na akuawa au akafa, kuwa atapata yanayomrid- hisha kutoka kwa kwa Mola wake.

Na anayelipiza mfano wa alivyoadhibiwa, yaani mwenye kupigana kujikinga. Kisha akadhulumiwa, si kwa lolote isipokuwa amekataa kudhulumiwa na kuchokozwa, bila shaka Mwenyezi Mungu atamnusuru. Yaani Mwenyezi Mungu atamsaidia mwenye kudhulumiwa na atamlipizia kisasi.

Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwingi wa maghufira.

Hapa kuna ishara kuwa msamaha kwa mkosaji ni jambo linalopendeza kwa Mwenyezi Mungu ikiwa mtu amemkosea Mwenyezi Mungu hasa, lakini haki ya umma haina msamaha.

Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu huuingiza mchana katika usiku na huuingiza usiku katika mchana na kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, mwenye kuona.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 3 (3:27).

Wafasiri wametaja njia nyingi za kuunganisha Aya hii na iliyo kabla yake, lakini hawakuleta jambo la kutuliza moyo. Katika utangulizi wa Juzuu ya kwanza tulidokeza kwamba Qur’an si kitabu cha fani cha kuwa na milango maalumu ya maudhui; isipokuwa ni kitabu cha uongofu na mawaidha.

Kinakugurisha kutoka jambo hili hadi jingine. Imam Ali (a.s.) anasema: “Hakika Aya inakuwa na jambo mwanzoni mwake na mwisho wake inakuwa na jambo jingine.”

Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na kwamba wale wanaowaomba badala yake ni batili, na hakika Mwenyzi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.

Mwenyezi Mungu ni haki kwa kudumu dhati yake na utukufu wa sifa zake, Yuko juu kwa vile hakuna mtawala zaidi ya utawala wake na ni Mkubwa ambaye amekienea kila kitu kiujuzi na kihuruma.

Makusudio ya kutaja sifa zote ni kuwa Mwenyezi Mungu huwanusuru wenye takua na huwafedhehesha wale waliokufuru na kufanya ufisadi ardhini.

Je huoni kwamba Mwenyezi Mungu huteremsha maji kutoka mbinguni na mara ardhi inakuwa chanikiwiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye habari.

Umetangulia mfano wake katika Aya ya 5 ya Sura hii na pia kwenye Juz.2 (2: 164).

Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosha, Mwenye kusifiwa.

Hahitajii walimwengu na ni msifiwa wa wanaosifiwa. Katika Najul-bal-agha imesemwa: “Yeye ni mwenye kujitosha bila ya kutaka kufaidika,” yaani kwamba utajiri wake ni wa kidhati sio wa kunasibishwa na kwamba yeye lau angelihitajia kitu asingelikuwa ni Mungu. Ibn Al-Arabi anasema, katika kitabu Futuhatul-makkiyya:

“Hakuna wa kusifiwa isipokuwa anayesifiwa na mwenye sifa.” Yaani Mwenyezi Mungu ndiye mwenye sifa; kwamba hakuna mwenye kustahiki sifa ila aliyesifiwa na Mungu au kuridhia asifiwe.”

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ سَخَّرَ لَكُمْ مَا فِي الْأَرْضِ وَالْفُلْكَ تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ وَيُمْسِكُ السَّمَاءَ أَنْ تَقَعَ عَلَى الْأَرْضِ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَحِيمٌ {65}

Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu amewadhalilishia vilivyomo ardhini na majahazi yapitayo baharini kwa amri zake. Na anazizuia mbingu zisianguke juu ya ardhi isipokuwa kwa idhini yake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa watu ni Mpole, Mwenye kurehemu.

وَهُوَ الَّذِي أَحْيَاكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۗ إِنَّ الْإِنْسَانَ لَكَفُورٌ {66}

Naye ndiye ambaye amewahuisha kisha atawafisha kisha atawahuisha. Hakika mtu ni mwenye kukufuru sana.

لِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنْسَكًا هُمْ نَاسِكُوهُ ۖ فَلَا يُنَازِعُنَّكَ فِي الْأَمْرِ ۚ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدًى مُسْتَقِيمٍ {67}

Kila umma tumeujalia sharia wanazozifuata. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na lingania kwa Mola wako; hakika wewe uko katika uongofu ulionyooka.

وَإِنْ جَادَلُوكَ فَقُلِ اللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ {68}

Na wakikujadili, basi sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi mnayoyatenda.

اللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كُنْتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ {69}

Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu siku ya Kiyama katika hayo mnayohitilafiana.

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ {70}

Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na ardhini? Hakika hayo yamo kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.