read

Aya 65 – 70: Anazuia Mbingu

Maana

Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu amewadhalilishia vilivyomo ardhini na majahazi yapitayo baharini kwa amri zake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (14: 32) na Juz. 14 (16: 14).

Na anazizuia mbingu zisianguke juu ya ardhi isipokuwa kwa idhini yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma kwa watu.

Mwenyezi Mungu amezizuia kwa ‘nguvu ya mvutano’; kama anavyowazuia ndege kwa mbawa zao. Ametegemeza kwake Mwenyezi Mungu kuzuia, kwa sababu yeye ndiye muumba wa ulimwengu na msababishaji wa sababu. Katika baadhi ya Aya, Mwenyezi Mungu, ameleta ibara ya sababu hizo kwa neno, mikononi mwa Mwenyezi Mungu; kama vile:

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُمْ مِمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ {71}

“Je, hawaoni kuwa tumewaumbia katika vile ilivyofanya mikono yetu, wanyama nao wanawamiliki” (36:71)

قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَنْ تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ {75}

“Akasema tena: Ewe Iblis! Ni kipi kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu?” (38:75).

KwavyovyoteiwavyonikwambalengolakauliyakeMwenyeziMungu: ‘Na anazizuia mbingu...’ ni kuashiria kwamba ni lazima mtu afikirie sana katika kuumbwa ulimwengu, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyoupangilia kwa uweza wake na hekima yake. Lau si hekima na mpangilio huu, ulimwengu ungeliharibika na sayari zote zingekuwa bure tu.

Naye ndiye ambaye amewahuisha kisha atawafisha kisha atawahuisha. Hakika mtu ni mwenye kukufuru sana.

Umepita mfano wake katika Juz. 1 (2: 28) kifungu cha ‘Mauti na uhai mara mbili.’ Ama wasifu wa mtu kuwa ni mwenye kukufuru sana, dhalimu sana, mwenye kujifaharisha sana n.k. sio kuwa ni kuelezea hakika yake yote ilivyo, isipokuwa ni kutafsiri silika yake katika baadhi ya misimamo yake. Angalia Juz.12 (11:9).

Kila umma tumeujalia sharia wanazozifuata.

Makusudio ya umma ni watu wa dini. Neno sharia tumelifasiri kutokana na neno mansaka, ambalo lina maana mbalimbali; miongoni mwazo ni: Mnyama anayechinjwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika Aya 34 ya Sura hii tuliyo nayo.

Maana nyingine ni mahali pa ibada. Pia lina maana ya sharia na njia, ambayo ndiyo yaliyokusudiwa hapa, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu iliyokuja moja kwa moja baada ya neno hilo:

Basi wasizozane nawe katika jambo hili.

Yaani maadamu kila watu wa dini wana sharia zao na njia wanzozifuata, basi watu wa dini nyingine wasikuletee mzozo kwenye Uislamu na sharia yake. Sharia ya Tawrat na inajili ni kwa ajili ya waliopita, lakini sharia ya Qur’an ni kwa ajili ya watu wa sasa na watakaofuatia hadi siku ya ufufuo.

Na lingania kwa Mola wako wala usijishughulishe na upinzani wa wapinzani wala mizozo.

Hakika wewe uko katika uongofu ulionyooka.

Na atakayefuata muongozo wako hatapotea wala kuwa muovu.

Na wakikujadili, basi sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi mnayoyatenda. Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu siku ya Kiyama kati- ka hayo mnayohitilafiana.

Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake aendelee na mwito wake, aachane nao wenye mizozo na inadi na awaambie kuwa Mwenyezi Mungu anajua matendo yetu na yenu na yupi aliyeongoka kati yetu sisi na nyinyi. Na Yeye ndiye hakimu siku ya hukumu. Huko mtajua ni yupi mwenye haki na mwenye batili.

Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na ardhini? Hakika hayo yamo kitabuni.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume (s.a.w.). Makusudio ni kuwakemea makafiri kwamba waliyoyasema na wanayoyadhamiria katika kufuru na vitimbi kwa Nabii wa Mungu yamesajiliwa na yako kwake, atahisabu na atawalipa wanayostahiki.

Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

وَيَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَمَا لَيْسَ لَهُمْ بِهِ عِلْمٌ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ نَصِيرٍ {71}

Na wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambavyo hakuviteremshia dalili na ambavyo hawana ujuzi navyo. Na madhalimu hawatakuwa na wa kuwasaidia.

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ تَعْرِفُ فِي وُجُوهِ الَّذِينَ كَفَرُوا الْمُنْكَرَ ۖ يَكَادُونَ يَسْطُونَ بِالَّذِينَ يَتْلُونَ عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۗ قُلْ أَفَأُنَبِّئُكُمْ بِشَرٍّ مِنْ ذَٰلِكُمُ ۗ النَّارُ وَعَدَهَا اللَّهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ {72}

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi utaona chuki katika nyuso za waliokufuru; hukaribia kuwavamia wale wanowasomea Aya zetu. Sema: Je, niwaambiye yaliyo mabaya zaidi kuliko haya? Ni moto wa Mwenyezi Mungu aliowaahidi waliokufuru, na ni marudio mabaya hayo.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَاسْتَمِعُوا لَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ لَنْ يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ ۖ وَإِنْ يَسْلُبْهُمُ الذُّبَابُ شَيْئًا لَا يَسْتَنْقِذُوهُ مِنْهُ ۚ ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ {73}

Enyi watu! Umepigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu hawatoum- ba nzi wajapojumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Amedhoofika atakaye na anayetakiwa.

مَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ {74}

Hawakumkadiria Mwenyezi Mungu haki ya kadiri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.

اللَّهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ {75}

Mwenyezi Mungu huteua wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۗ وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ {76}

Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.