read

Sura Ya Ishirini Na Mbili: Al-Hajj

Baadhi ya Aya zake zimeshuka Makka na nyingine Madina. Ina Aya 78.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ {1}

Enyi watu! Mcheni Mola wenu. Hakika tetemeko la saa ni jambo kuu.

يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُمْ بِسُكَارَىٰ وَلَٰكِنَّ عَذَابَ اللَّهِ شَدِيدٌ {2}

Siku mtakapoiona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshae na kila mwenye mimba ataiharibu mimba yake. Na utawaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali.

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُجَادِلُ فِي اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَانٍ مَرِيدٍ {3}

Na miongoni mwa watu kuna anayejadiliana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu na anamfuata kila shetani muasi.

كُتِبَ عَلَيْهِ أَنَّهُ مَنْ تَوَلَّاهُ فَأَنَّهُ يُضِلُّهُ وَيَهْدِيهِ إِلَىٰ عَذَابِ السَّعِيرِ {4}

Ameandikiwa kwamba anayemtawalisha shetani, basi huyo hakika atampoteza na atamwongoza katika adhabu ya moto mkali.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنْ كُنْتُمْ فِي رَيْبٍ مِنَ الْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِنْ مُضْغَةٍ مُخَلَّقَةٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَةٍ لِنُبَيِّنَ لَكُمْ ۚ وَنُقِرُّ فِي الْأَرْحَامِ مَا نَشَاءُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُسَمًّى ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ۖ وَمِنْكُمْ مَنْ يُتَوَفَّىٰ وَمِنْكُمْ مَنْ يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلَا يَعْلَمَ مِنْ بَعْدِ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ وَتَرَى الْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَا أَنْزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنْبَتَتْ مِنْ كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ {5}

Enyi watu! Ikiwa mna shaka ya kufufuliwa, basi kwa hakika tuliwaumba kutokana na udongo kisha kutokana na tone kisha kutokana na pande la damu kisha kutokana na pande la nyama lenye umbo na lisilokuwa na umbo. Ili tuwabainishie. Na tunaliweka katika matumbo ya kizazi mpaka muda uliowekwa. Kisha tunawatoa hali ya kuwa mtoto mchanga kisha mfikie kukomaa kwenu. Na wapo miongoni mwenu wanaokufa na wapo miongoni mwenu wanorudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa hata asijue kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imekufa, lakini tunapoyateremsha maji juu yake, husisimka na kututumka na kumea kila aina ya mimea mizuri.

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّهُ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {6}

Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ni haki na kwamba hakika yeye ndiye Mwenye kuhuisha wafu na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Na kwamba saa itakuja hapana sha وَأَنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ لَا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ اللَّهَ يَبْعَثُ مَنْ فِي الْقُبُورِ {7}

ka kwa hilo, na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.