Table of Contents

Aya 10 – 22: Musa

Maana

Aya hizi hadi kufikia Aya ya 28 ni za kisa cha Musa ambacho kimetangulia mara kadhaa. Katika Juz. 16 (20: 9) tumeleza sababu za kukaririka kisa hicho.

Na Mola wako alipomwita, Musa kwamba nenda kwa watu madhal- imu watu wa Firauni.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:24).

Hawaogopi?

Hii ni jumla nyingine, maana yake ni kuwa, umefika wakati sasa Firauni na watu wake waogope mwisho wa uovu na utaghuti.

Akasema: Mola wangu! Hakika mimi naogopa watanikadhibisha.

Katika Juz. 16 (20 45) ni: “Ewe Mola wetu! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.”

Yaani asije akatuwahi kutuadhibu kabla kufikishia ujumbe.

Na kifua changu kinadhikika, na ulimi wangu haukunjuki vyema, basi mtumie ujumbe Harun.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimtuma Musa kupeleka ujumbe wake kwa Firauni. Na hili, kwa upande mmoja, ni jambo zito na lenye mashaka sana, kutokana na utaghuti wa Firauni na nguvu za utawala wake. Na kwa upande mwingine, ujumbe wenyewe ni mzito.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwambia Mtume wake Muhammad (s.a.w.):

إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا {5}

“Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito.” (73:5).

Musa alikuwa ni mwepesi wa kughadhibika kwa ajili ya haki, na ulimi wake ulikuwa na kigugumizi kinachomzuia kutamka. Kwa hiyo akahofia kutotekeleza vizuri ujumbe mkuu. Hakuna yeyote anayehofia kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu kuliko mitume; hasa wale Ulul-a’zm. Hii inatokana na isma. Ndipo Musa akamtaka Mwenyezi Mungu kumtuma Jibril kwa nduguye, Harun, ili awe msaidizi wake katika jambo hili muhimu.

Nao wanalo kosa juu yangu basi naogopa wasije wakaniua.

Anaishiria lile tukio la kumuua mtu wa upande wa Firauni pale alipom- saidia mtu wa upande wake; kama ilivyoelezwa katika Aya hii:

فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَٰذَا مِنْ شِيعَتِهِ وَهَٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِنْ شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ {15}

“Na akakuta humo watu wawili wanapigana mmoja ni katika wenzake na mwingine ni katika maadui zake. Yule aliye katika wenzake akamtaka msaada juu ya adui yake. Musa akampiga ngumi akammaliza.” (28:15).

Musa alihofia kuchukua risala ya Mwenyezi Mungu kwa Firauni asije akamuua kabla kukamilisha lengo, lakini akiwa na nduguye na ikatokewa kuuawa, basi atachukua nafasi yake kuendeleza malengo.
Akasema – Mwenyezi Mungu – sivyo kabisa! Nendeni na ishara yetu. Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni wajumbe wa Mola wa walimwengu wote. Ya kwamba uwaachilie wana wa Israil waende nasi.

Musa alihofia dhiki ya kifua, kufungika ulimi na kuuliwa, lakini Mwenyezi Mungu akamhakikishia usalama na akamwambia kuwa hakuna kitu kitaka- chokuwa katika hayo, kwa sababu mimi nitawasaidia na kuwanusuru. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20: 46 – 47).

Akasema: Je, hatukukulea utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? Na ukatenda kitendo chako ulichokitenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?

Musa na Harun walielekea kwa Firauni, wakaingia kwake wakiwa wamevaa deraya ya sufu, mikononi mwao wakiwa na fimbo. Wakampa mwito wa kumwamini Mungu na kumpa sharti la kusilimu na kutii ili utawala wake ubakie na kudumu enzi yake.

Firauni aliwabeza wawili hawa, waliompa masharti ya kudumu utawala na enzi yake, wakiwa hawana cheo chochote wala mali. Hakutaka kuwaua kwa kuhofia asiambiwe kuwa ameshindwa na hoja akakimbilia upanga.

Lakini Firauni anaweza kuwa na hoja gani? Ni kwa mantiki gani atakayoweza kujadili? Hana kitu isipokuwa kuvungavunga na kumtajia Musa yaliyopita.

Je, hatukukulea na ukakaa nyumbani kwetu miaka, kisha ukatuulia mtu wetu na ukakimbia? Hii ndio shukrani yako? Zaidi ya hayo unadai kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwetu? Unataka tukusikize na kukutii na sisi ndio mabwana zako na wafadhili wa neema zako?

Kisha Firauni akawegeukia watu wa baraza lake na akasema: “Basi mbona hakuvikwa vikukuku vya dhahabu?” (43:53). Kwenye dhahabu tu ndio kuna kuwa na siri ya mantiki ya mataghuti. Hakuna utume wala ubwana au ubora isipokuwa kwa ajili ya dhahabu na dhahabu yenyewe.

Musa (a.s.) akamjibu kuhusu kuua akasema: “Nililifanya hilo nikiwa miongoni mwa wasioelewa.”

Yaani sikuelewa kuwa ngumi yangu itamuua. Nami nilikusudia kukinga na kutia adabu, nikakosea makusudio. Basi mimi nina dhambi gani katika hilo? Kukusudia ni nguzo ya msingi ya kosa la jinai kwa watu wa sharia.

Basi niliwakimbia nilipowahofia.

Sikukimbia hukumu ya uadilifu, bali nilikimbia dhulma kwa kuhofia kunichukulia kuwa ni muuaji wa makusudi. Kuna mmoja alimwambia Musa:

إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ {20}

“Hakika wakubwa wanashauriana kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.” (28:20).

Na Mola wangu akanitunukia hukumu na akanijaalia niwe miongoni mwa mitume.

Firauni alimtajia Musa ufukara na utoro; Musa naye akamwambia kuwa utukufu haupimwi kwa mali wala kwa ufalme; isipokuwa uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, humpatia amtakaye katika waja wake. Na mimi Mwenyezi Mungu amenitunukia elimu ya dini yake na sharia yake kwa njia ya kheri na usawa na akanitukuza kwa kunituma kwako na kwa watu wako.

Musa aliendelea kumjibu Firauni, kuhusu malezi na akasema:

Na hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia na wewe umewatia utumwani wana wa Israil?

Yaani unanisimbulia kwa malezi yako kwangu na unajitia kutojua kuwa sababu ni uadui wako wa kuwachinja watoto wa kiume wa watu wangu na kuwatia utumwani watoto wao wa kike? Mama yangu alipohofia wewe kunichinja akanitupa baharini na matokeo yake yakawa ni kuishi mimi mbali ugenini bila ya huruma ya mama na mapenzi ya baba? Hii ndiyo fadhila yako kwangu? Firauni alizibwa mdomo, akaanza kuwatafuta wabatilifu wake; kama utakavyoona katika kifungu kifuatacho.

قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ {23}

Akasema Firauni: Na ni nani huyo Mola wa walimwengu wote?

قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِنْ كُنْتُمْ مُوقِنِينَ {24}

Akasema: Ni Mola wa mbingu na ardhi ikiwa nyinyi mna yakini.

قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ {25}

Akawaambia waliomzunguuka: Je, hamsikii?

قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ {26}

Akasema: Ni Mola wenu na Mola wa baba zenu wa kwanza.

قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ {27}

Akasema: Hakika mtume wenu mliyetumiwa ni mwenda wazimu.

قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ {28}

Akasema: Ni Mola wa mashariki na magharibi na viliomo baina yake, ikiwa nyinyi mna akili.

قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ {29}

Akasema: Kama ukimfanya mungu mwingine asiyekuwa mimi basi bila shaka nitakufanya miongoni mwa wafungwa.

قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُبِينٍ {30}

Akasema: Ijapokuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?

قَالَ فَأْتِ بِهِ إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ {31}

Akasema: Kilete basi kama wewe ni katika wakweli.

فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُبِينٌ {32}

Akaitupa fimbo, mara ikawa nyoka dhahiri.

وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ {33}

Na akautoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao.

قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ {34}

Akasema kuwaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi, mjuzi.

يُرِيدُ أَنْ يُخْرِجَكُمْ مِنْ أَرْضِكُمْ بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ {35}

Anataka kuwatoa katika ardhi yenu. Basi mnatoa shauri gani?

قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ {36}

Wakasema: Mwache kidogo yeye na ndugu yake, na uwatume wakusanyao watu mijini.

يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ {37}

Wakuletee kila mchawi mkubwa, mjuzi.