Table of Contents

Aya 160-175: Lut

Maana

Kisa cha Lut kimetangulia katika Juz. 8 (7:80 –84) na Juz. 12 (11:82– 87).

Kaumu ya Lut waliwakadhibisha mitume. Alipowaambia ndugu yao Lut: Je, hamna takua?

Ni ndugu yao katika kuwa pamoja na makazi; si katika dini wala nasabu. Kwa kuwa yeye alikuja hapo na ami yake, Ibrahim (a.s) kutoka Babel (Babylon) kupitia Misr hadi Palestina. Lut alikaa katika bonde la Jordan na Ibrahim akakaa katika nyanda za juu kaskazini. Hapo ilikuwa ni karne kumi na tisa kabla ya kuzaliwa Nabii Isa (19 B.C.)

Imetangulia kwa herufi zake, katika Aya 67 na 68 ya sura hii na pia sehemu iliyopita.

“Hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii. Na siwataki ujira juu yake, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola wa walimwengu wote.

Lut alianza kama alivyoanza Nuh, Hud na Swaleh (a.s.). Kwa sababu risala ya wote ni moja. Soma katika sura hii Aya zinazomzungumzia kila mmoja katika wao.

Je, katika viumbe wote mnawaendea wanaume?

Mnafanya kitendo hiki cha fedheha kwa wanaume katika wanadamu?

Na mnaacha alichowaumbia Mwenyezi Mungu katika wake zenu?

Kwa hiyo mnahalifu hukumu ya maumbile na kanuni, tabia na lengo la kumbwa mume na mke.

Tendo lenu halikubaliwi hata na wanyama na wadudu. Lakini bunge la Uingereza limeruhusu ulawiti. Hiyo ni dalili kuwa Uingereza ni duni zaidi kuliko wanyama katika hulka yake na thamani yake. Sio mbali kuwa hii ni natija ya historia yake ndefu ya ukoloni unaochukiwa. Kwa sababu utaghuti na uadui una mwisho mbaya.

Bali nyinyi ni watu mnaoruka mipaka.

Mmepituka mipaka yote kwa hawa, usafihi, uasi na ujeuri wenu.

Wakasema: Kama hutakoma ewe Lut bila shaka utakuwa miongoni mwa wanaotolewa.
Umetangulia mfano wake katika Aya 116 ya Sura hii.

Akasema: Hakika mimi ni katika wanaokichukia hiki kitendo chenu.

Katika maana yake ni; Aya 216 ya sura hii! “Na ikiwa watakuasi basi sema mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yatenda.”

Mola wangu! Niokoe na ahli zangu kwa wayatendao. Basi tukamuokoa na ahli zake wote. Isipokuwa kikongwe katika waliokaa nyuma.

Kisha tukwaangamiza wale wengine. Na tukawanyesheza mvua, basi ni uovu mno wa mvua ya waliyoonywa.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:83 – 84) na Juz. 14 (15:59 – 60).

Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

Imetangulia kwa herufi zake, katika Aya 67 na 68 ya Sura hii na pia sehemu iliyopita.

كَذَّبَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ الْمُرْسَلِينَ {176}

Watu wa mwituni waliwakadhibisha mitume.

إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ {177}

Alipowaambia Shua’yb: Je, hamna takua?

إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ {178}

Hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.

فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ {179}

Basi mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii.

وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ {180}

Na siwataki ujira juu yake, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola wa walimwengu wote.

أَوْفُوا الْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُخْسِرِينَ {181}

Timizeni kipimo sawasawa wala msiwe miongoni mwa wanaopunja.

وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ {182}

Na pimeni kwa mizani iliyo sawa.

وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ {183}

Wala msiwapunguzie watu vitu vyao, Wala msifanye ufisadi katika nchi mkafanya vurugu.

وَاتَّقُوا الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالْجِبِلَّةَ الْأَوَّلِينَ {184}

Na mcheni aliyewaumba nyinyi na vizazi vilivyotangulia.

قَالُوا إِنَّمَا أَنْتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ {185}

Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa tu.

وَمَا أَنْتَ إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُنَا وَإِنْ نَظُنُّكَ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ {186}

Na wewe si chochote ila ni mtu kama sisi, na kwa hakika tunakuona ni katika waongo.

فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِنَ السَّمَاءِ إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ {187}

Basi tuangushie kipande cha mbingu, ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.

قَالَ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ {188}

Akasema: Mola wangu anajua zaidi mnayoyatenda.

فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ الظُّلَّةِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ {189}

Basi wakamkadhibisha, ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُمْ مُؤْمِنِينَ {190}

Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini.

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ {191}

Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.