Table of Contents

Aya 38 – 51: Walifika Wachawi

Maana

Basi wakakusanywa wachawi wakati wa siku maalum.

Siku yenyewe ni sikukuu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

قَالَ مَوْعِدُكُمْ يَوْمُ الزِّينَةِ وَأَنْ يُحْشَرَ النَّاسُ ضُحًى {59}

“Akasema: Miadi yenu ni siku ya sikukuu na watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.” Juz. 16 (20:59).

Na watu wakaambiwa: Je, mtakusanyika ili mshuhudie mapambano haya? Watu hawahitaji kuhimizwa kwenye mambo haya; hao wenyewe watashindana kufika. Na hili ndilo alilolitaka Musa, ili haki idhihirike na batili ibatilike machoni mwa watu.

Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakaoshinda.

Waliosema haya kwa watu ni Firauni na wakuu wake. Dhahiri ya kauli yao hii inaashiria kuwa wana shaka na dini ya wachawi na kwamba wao wanitafuta haki ili waifuate, lakini haya sio makusudio yao. Kwa sababu wao na wachawi wako kwenye dini moja. Makusudio yao ni kuwa huenda tutabaki kwenye uthabiti wa dini yetu wala hatutamfuta Musa.

Basi walipokuja wachawi wakamwambia Firauni: Je, tutapata ujira ikiwa tutashinda? Akasema: Ndio, hapo nanyi hakika mtakuwa miongoni mwa wanaokurubishwa. Musa akawaambia: Tupeni mnavyotaka kutupa. Wakatupa kamba zao na fimbo zao na wakasema:

“Kwa nguvu za Firauni hakika sisi bila shaka ni wenye kushinda. Musa akatupa fimbo yake, mara ikavimeza walivyovibuni. Wachawi wakapomoka kusujudu.Wakasema: Tumemwamini Mola wa Walimwengu. Mola wa Musa na Harun.

Akasema Firauni: Je, mmemwamini kabla sijawaruhusu. Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliyewafundisha uchawi, lakini punde mtajua. Nitawakata mikono yenu na miguu yenu kwa kubadilisha, kisha nitawasulubu nyote. Wakasema: Haidhuru, hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu. Hakika sisi tunatumai Mola wetu atughufirie makosa yetu kwa kuwa ndio wa kwanza kuamini.

Aya hizi zote zimetajwa katika Juz. 9 (7: 113 – 126); wala hakuna tofauti baina ya hapa na huko, isipokuwa katika baadhi ya ibara tu; kwa mfano kule imesemwa: ‘wakaja wachawi’ na hapa ikasemwa; ‘walipokuja wachawi,’ n.k.

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي إِنَّكُمْ مُتَّبَعُونَ {52}

Na tulimpelekea wahyi Musa kwamba nenda na waja wangu wakati wa usiku, kwa hakika mtafuatwa.

فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ {53}

Basi Firauni akawatuma mjini wakusanyao.

إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ {54}

Hakika hawa ni kikundi kidogo.

وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَائِظُونَ {55}

Nao wanatuudhi.

وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَاذِرُونَ {56}

Na sisi ni wengi wenye kuchukua hadhari.

فَأَخْرَجْنَاهُمْ مِنْ جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ {57}

Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem.

وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ {58}

Na mahazina na vyeo vya heshima.

كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا بَنِي إِسْرَائِيلَ {59}

Hivyo ndivyo! Na tukawarithisha wana wa Israil.

فَأَتْبَعُوهُمْ مُشْرِقِينَ {60}

Kisha wakawafuata walipotokewa na jua.

فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ {61}

Yalipoonana makundi mawili, watu wa Musa wakasema: Hakika tumepatikana.

قَالَ كَلَّا ۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ {62}

Akasema: Hapana! Hakika Mola wangu yuko pamoja nami, ataniongoza.

فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانْفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ {63}

Tulimpelekea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana na kila sehemu ikawa kama milima mkubwa.

وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ {64}

Na tukawajongeza hapo wale wengine.

وَأَنْجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَنْ مَعَهُ أَجْمَعِينَ {65}

Na tukamwokoa Musa na waliokuwa pamoja naye wote.

ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ {66}

Kisha tukawazamisha hao wengine.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُمْ مُؤْمِنِينَ {67}

Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara lakini wengi wao si wenye kuamini.

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ {68}

Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.