read

Aya 59: Amani Juu Ya Waja Aliowateua

Rehema Na Amani Kwa Wenye Takua

Sema: Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu (Alhamdu lillah) na amani ishuke juu ya waja wake aliowateua.

Aya hii imetangulia mwisho wa Juzuu iliyopita. Tumeileta hapa kwa vile maelezo yake yanaungana na hapa.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja baadhi ya Mitume na baadhi ya miujiza aliyowahusisha nayo, sasa anamwamrisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.) kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema alizomhusisha nazo na kuwatakia amani mitume wote ambao amewateua kwa ujumbe wake. Amekutanisha kuwatakia amani pamoja na sifa njema kwake, kutanabahisha daraja yao na ukuu wa vyeo vyao.

Kila mwenye kumcha Mwenyezi Mungu na akazifanyia kazi Sunna za Mtume wa Mweneyzi Mungu inafaa kumuombe rehema na amani, awe hai au maiti, Mtume au asiyekuwa Mtume; hasa akiwa ni katika watu wa nyumba ya Muhammad (s.a.w.) na akapigana jihadi kwa ajili ya Uisalmu na kuenea mwito wake. Mweneyezi Mungu (s.w.t.) anasema: malaika wake ndio wanaowarehemu.” (33:43).

“Yeye na Katika Sahih Bukhari na vinginevyo, imeelezwa: “Waliuliza: “Vipi tukutakie rehema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Semeni, Allahumma swalli ala Muhammadi wwa ala ali Muhammad. Kama swal-layta ala Ibrahima wa ala ali Ibrahima. Wa barik ala Muhammadi wwa ala ali Muhammad. Kama barakta ala Ibrahima wa ala ali Ibrahim. Innaka hamidu mmajid

(Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyomrehemu Ibrahim na kizazi cha Ibrahim; na umbariki Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyombariki Ibrahim na kizazi cha Ibrahim. Hakika wewe ni Mwenye kusifiwa Mwenye kutukuzwa.”

Imekuwa ni desturi ya Waislamu, tangu wakati wa Mtume mtukufu (s.a.w.), kufungua vitabu vyao na khutba zao kwa Bismillah, kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehema Muhammad na wanaokwenda mwenendo wake katika ahli baiti wake na swahaba zake. Chimbuko la hilo ni Aya hii.

Je Mwenyezi Mungu ni bora au wale wanaowashirikisha naye?

Maelezo ya sehemu hii yatakuja kwenye juzuu inayofuatia, kwa vile yanaungana na huko.