Table of Contents

Aya 90 – 104: Pepo Kwa Wenye Takua Na Moto Kwa Wapotevu

Maana

Na Bustani (Pepo) itasogezwa kwa wenye takua

Bila shaka iko karibu na mwenye kuongoka na akamcha Mungu na iko mbali na mwenye kupotea.

Na Jahannam itadhihirishwa kwa wapotofu.

Ataidhihirisha Mwenyezi Mungu kwa wale walioikana na kuikadhibisha.

Na wataambiwa wako wapi mliokuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Na mkiwatarajia kwa siku hii, huku mkisema kuwa mliwabudu ili wawakurubishe kwa Mwenyezi Mungu?

Je, watawasaidia au kujisaidia wenyewe?

Hakika wao hawawezi kuwasaidia wala kujisaidia wenyewe.

Basi watavurumizwa humo wao na wapotofu na majeshi ya Ibilisi yote.

Wao ni hao waungu wao na wapotofu ni wale walioabudu. Mwanajeshi wa Ibilisi ni kila mpotofu na mpotoshaji. Mwenyezi Mungu atawachanganya wote kisha awatupe kwenye shimo la Jahannam.

Watasema na hali ya kuwa wanazozana humo: Wallah! Hakika tulikuwa katika upotevu ulio wazi, tulipowafanya sawa na Mola wa walimwengu wote. Na hawakutupoteza ila wakosefu.
Wapotofu kesho watasema, baada ya kupitwa na wakati, kuwaambia waungu wao na mashetani wao, kwamba nyinyi ndio mliokuwa viongozi wetu wa upofu na upotevu, wakati tulipowaabudu na kuwafanya mko sawa na Mwenyezi Mungu. Na wakosefu ndio waliokuwa kikwazo, ambao ni viongozi wa manufaa na masilahi, asili ya ufisadi na balaa.

Basi hatuna waombezi wala rafiki wa dhati.

Kesho hakuna uombezi wala ugombezi. Hakuna kitakachomfaa mtu isipokuwa moyo ulio salama na amali njema. Na muovu ni yule asiyekuwa na mawili hayo.

Laiti tungepata kurejea tena tungelikuwa katika waumini.

Baada ya kukata tamaaa na kila kitu ndio wanatamani kurudi duniani ili waamiini na kutenda. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ {28}

“Na kama wangelirudishwa, bila shaka wangeyarudia yale waliyokatazwa na hakika wao ni waongo.” Juz. 7 (6:28)

Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.

Imetangulia kwa herufi zake, katika Aya 67 na 68 ya sura hii.

كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ {105}

Kaumu ya Nuh waliwakadhibisha mitume.

إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ {106}

Alipowaambia ndugu yao Nuh: Je, hamna takua?

إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ {107}

Hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.

فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ {108}

Basi mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii.

وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ {109}

Na siwataki ujira juu yake, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola wa walimwengu wote.

فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ {110}

Basi mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii.

قَالُوا أَنُؤْمِنُ لَكَ وَاتَّبَعَكَ الْأَرْذَلُونَ {111}

Wakasema: Je, tukuamini na hali wanaokufuata ni walio duni?

قَالَ وَمَا عِلْمِي بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {112}

Akasema: Nayajuaje waliyokuwa wakiyafanya?

إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّي ۖ لَوْ تَشْعُرُونَ {113}

Hisabu yao haiko ila kwa Mola wangu. Lau mngelitambua.

وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الْمُؤْمِنِينَ {114}

Wala mimi si mwenye kuwafukuza waumini.

إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُبِينٌ {115}

Sikuwa mimi ila ni muonyaji aliye dhahiri.

قَالُوا لَئِنْ لَمْ تَنْتَهِ يَا نُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمَرْجُومِينَ {116}

Wakasema: Kama hutakoma ewe Nuh bila shaka utapigwa mawe.

قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِي كَذَّبُونِ {117}

Akasema: Mola wangu! Hakika kaumu yangu wamenikadhibisha.

فَافْتَحْ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِي وَمَنْ مَعِيَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ {118}

Basi amua baina yagu mimi na wao uamuzi. Na uniokoe na walio pamoja nami katika waumini.

فَأَنْجَيْنَاهُ وَمَنْ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ {119}

Basi tukamuokoa na walio pamoja naye katika jahazi iliyosheheni.

ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ الْبَاقِينَ {120}

Kisha tukawagharikisha baadaye waliobaki.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُمْ مُؤْمِنِينَ {121}

Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wenye kuamini.

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ {122}

Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.