Table of Contents

Sura Ya Ishirini Na Sita: Shua’rau

Twabrasiy amesema imeshuka Makka isipokuwa Aya 224 hadi mwisho, zimeshuka Madina. Ina Aya 227

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.

طسم {1}

Twaa Siin Miim.

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ {2}

Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ {3}

Huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa kuwa hawawi waumini.

إِنْ نَشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِمْ مِنَ السَّمَاءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ {4}

Tungelipenda tungeliwateremshia kutoka mbinguni ishara zikainyenyekea shingo zao.

وَمَا يَأْتِيهِمْ مِنْ ذِكْرٍ مِنَ الرَّحْمَٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ {5}

Na hauwajii ukumbusho mpya kutoka kwa Mwingi wa rehema ila hujitenga nao.

فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنْبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ {6}

Kwa hakika wamekadhibisha, kwa hivyo zitakujawafikia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai.

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ {7}

Je hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُمْ مُؤْمِنِينَ {8}

Hakika katika hayo kuna ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ {9}

Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.