read

Aya 16-18: Mnadhani Mtaachwa

Maana

Je, mnadhani kuwa mtaachwa na hali Mwenyezi Mungu hajawabain- isha wale wanaopigana jihadi miongoni mwenu.

Imetangulia tafsir yake katika Juz.4 (3:142)

Na hawakumfanya mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumin?

Utiifu bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni kuwapiga vita wabatilifu- maadui wa haki na ubinadamu. Ndipo akadokeza Mwenyezi Mungu: ‘Na hali hajawabainisha wale wanaopigana jihadi miongoni mwenu.”

Na maasi makubwa zaidi ni kuwapondokea, hapo akaeleza Mwenyezi Mungu (swt) kwa kusema: “Na hawakumfanya mwandani”

Kila mwenye kuwategemea watu wa dhulma na uadui na kuyaunganisha maslahi yake na yao, basi yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumin. Ni juu ya kila mwenye ikhlas kumtangaza na kufichua njama zake ili watu wamtofautishe yeye na mwaminifu na kumweka kila moja anapostahiki.

Na Mwenyezi Mungu ana habari za mnayoyafanya

Ndio yeye ni mjuzi mwenye habari, lakini hamwadhibu yeyote kwa anay- oyajua kwake, bali hata kwa yanayofichuka katika vitendo vyake na tabia zake.

Haiwi kwa washirikina kuamirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu.

Katika vitabu vya lugha husemwa. Nyumba imaamirika kwa wakazi wake, yaani wamekuwa wakazi humo au fulani amemuamirisha Mola wake, yaani amemwabudu. Ikaenea midomoni mwa watu Misikiti inaamirishwa kwa kutajwa Mwenyezi Mungu. Kuna Hadith isemayo: “Mwenyezi Mungu anasema: Majumba yangu katika ardhi ni misikiti, na wanaonizuru humo ndio wanaoiiamirisha.”

Hayo ndiyo maana yanayochukuliwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu kuamirisha misikiti. Yaani washirikina wasiingie na kufanya ibada zao za mizimu, kama walivyokuwa wakifanya siku za jahiliya. Ni bora pia wasiwe na usimamizi. Maana hiyo yanatiwa nguvu zaidi na kauli yake Mwenyezi Mungu:

Hali wanajishuhudia wenyewe ukafiri.

Kwa sababu kuabudu kwao masanamu na kuwaomba Lata na Uzza ni ushahidi wao juu yao wenyewe kwamba wao wanamkufuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumkufuru hastahiki kuingia majumba ya Mwenyezi Mungu.

Hao vitendo vyao vimeporomoka.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu haikubali amali pamoja na shirk.

Na katika moto watadumu.

Kwa sababu shirk imeangusha vitendo vyao vyote, hata vilivyokuwa vizuri.

Wanaoamirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale tu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wakasimamisha swala na wakatoa zaka na wasiogope ila Mwenyezi Mungu.

Yaani haijuzu kwa yeyote kuingia msikitini na kufanya ibada humo au kusimamia jambo lake lolote ila zikikusanyika humo sifa hizo. Kumwamini Mungu na Siku ya mwisho, na kuwa na nembo za dini ambazo muhimu zaidi ni kuswali na kutoa zaka na kumhofia Mwenyezi Mungu, yaani kumfanyia ikhlas katika kauli na vitendo.

Basi hao huenda wakawa miongoni mwa waliongoka kwenye haki na kuitumia.

Neno huenda kutoka kwa Mwenyezi Mungu, linamaanisha yakini kwa sababu shaka ni mahali kwake.

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ۚ لَا يَسْتَوُونَ عِنْدَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ {19}

Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِنْدَ اللَّهِ ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ {20}

Wale walioamini na wakahama na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa mali zao na nafsi zao, wana cheo kikukbwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye kufuzu.

يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُمْ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُقِيمٌ {21}

Mola wao anawabashiria rehema kutoka kwake na radhi na pepo ambazo watapata humo neema zitakazodumu.

خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ {22}

Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa