read

Maana

Ewe Mtume! Pambana na makafiri na wanafiki na uwawekee ngumu. Na makazi yao ni Jahanamu, nayo ni marejeo mabaya.

Mtume (saw) aliwachukulia upole wanafiki, lakini haikufaa, bali ndio walimtusi na kumwambia kuwa ni sikio; ndipo Mwenyezi Mungu (swt) akamwamrisha kuwawekea ngumu na kupambana nao. Lakini hakubain- isha aina ya kupambana nao. Je, ni kwa upanga ulimi au kwa njia nyingine. Maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu amemwachia Mtume (saw) kukadiria vile hekima na masilahi yanavyotaka.

Wanaapa kwa Mwenyezi Mungu, hawakusema na hakika wamekwisha sema neno la kufuru.

Waliosema ni jamaa katika wanafiki. Kwani wao walitamka neno la kufuru kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Alipowauliza waliogopa, wakaapa. Ndipo Mwenyezi Mungu akawakadhibisha na yakathibiti yale yaliyonasibishwa kwao.

Mwenyezi Mungu, mtukufu hakutaja majina ya walioapa kiapo cha uwon- go wala hilo neno la kufuru walilolitamka ili waislam wasiliabudu kwa kulisoma.

Sheikh Maraghi anasema: “Yamesahihika, yaliyopokewa, kwamba Mtume (saw) alipokuwa amelala chini ya kivuli cha mti, alisema: Atawajia mtu atawangalia kwa macho ya shetani. Akija msizungumze naye. Mara akatokea mtu mwenye mandhari ya kiuadui.Mtume akamwita na kumwambia: Kwa nini unanishutumu wewe na sahaba zako? Yule mtu akaondoka na kuleta wenzake; wakaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema. Akateremsha Mwenyezi Mungu Aya hii

Na wakakufuru baada ya kusilimu kwao

Mfano huu ni kama wa Aya 66 ya Sura hii.

Wakajihimu kufanya wasioyoweza kuyafikia.

katika Tafsir Razi, Bahrul-muhit Al-Manar, Maraghi na nyinginezo imeelezwa kuwa kikundi cha wanafiki kiliafikiana kummaliza Mtume. Mwenyezi Mungu akamfahamisha hilo akajiepusha nalo bila ya kutimia makusudio.

Katika Kitabu Ala’yan, cha Sheikh Muhammad Al-amin, kuna maelezo haya: “Mtume (s.a.w) alipokuwa akirudi kutoka Tabuk akielekea Madina, ali- fanyiwa njama na watu katika maswahaba zake. Wakala njama ya kumtupa kutoka katika njia inayopitia juu mlimani. Basi Mtume akapewa habari yao”.
Na hawakuchukia ila ni kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ame- watajirisha kwa fadhila zake.

Dhamiri inawarudia wanafiki. Wengi wao walikuwa katika dhiki ya maisha wakiwa na hali ngumu sana ya ufukara kabla ya kusilimu. Baada ya kutamka tamko la kusilimu kwa midomo yao tu, ziliwamiminikia riziki. Kwa vile Mtume alikuwa akiwagawanyia ngawira sawa na waislam wengine. Vile vile baadhi yao aliwalipia madeni yao.

Malipo yao yakawa ni hayo waliyoyasema na kuazimia kumua. Ndipo Mwenyezi Mungu akawatahayariza, na kukufuru kwao neema, kwa mfumo huu; sawa na kumwambia mtu uliye mfanyia wema kisha akakuudhi “Ubaya wangu ni kukufanyia wema?!”.

Wakitubia, itakuwa heri kwao

Mlango wa toba uko wazi kwa kila mwenye kuubisha. Njia ya kuuendea ni nyepesi sana, kiasi ambacho makafiri na wanafiki hawatakiwi lolote zaidi ya kuomba msamaha kwa yaliyopita na kusadikisha yajayo.

Na kama wakikengeuka, Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu iumizayo katika duniani na Akhera.

Adhabu yao huko Akhera inajulikana ama adhabu katika dunia ni kwamba wanafiki daima watakuwa katika hofu ya kuwafedheheka na kufichuka.

Kwa ajili hiyo wanaogopa kila kitu na wanadhani kuwa kila neno wanaambiana wao tu; kama alivyowatajia Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kauli yake:

وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِنْ يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ {4}

“Na ukiwaona miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao; wao ni kama boriti zilizotegemezwa, wanadhani kila kishindo ni juu yao” (63:4)

Hawana mlinzi katika ardhi wala msaidizi.

Ninani anayeweza kumsaidia au kujaribu kumsaidia ambaye aibu yake na maovu yake yamefichuka kwa watu wote.

وَمِنْهُمْ مَنْ عَاهَدَ اللَّهَ لَئِنْ آتَانَا مِنْ فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ {75}

Na miongoni mwao wako waliomwahidi Mwenyezi Mungu: Akitupa fadhila zake hakika tutatoa sadaka na hakika tutakuwa miongoni mwa watendao wema.

فَلَمَّا آتَاهُمْ مِنْ فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوْا وَهُمْ مُعْرِضُونَ {76}

Lakini alipowapa katika fadhila zake, walizifanyia ubakhili wakageuka na huku wakipuuza.

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ {77}

Kwa hiyo ukawalipa unafiki katika nyoyo zao mpaka siku ya kukutana nao. Kwa sababu ya kumhalifu Mwenyezi Mungu yale waliyomwahidi na kwa sababu ya kusema kwao uwongo.

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ وَأَنَّ اللَّهَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ {78}

Je,hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong’ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye sana mambo ya ghaibu.