read

Surah Ya Tisa: At – Tawba

Vile vile inaitwa Sura baraa na fadhiha, kwa vile inawafedhehi wanafiki. Aya zake ni 129. Imeshuka Madina.

Wameafikiana Masahaba na watalaamu wa kisomo cha Qur’an (qurrau)kutokuwa na Bismillahi mwanzo wake, kwa sababu ni Sura iliyoshuka kuondosha aibu na Bismillahi ni amani kutokana na Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Imesemekana kuwa hiyo na Sura Anfal (iliyotangulia) ni Sura moja.

بَرَاءَةٌ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدْتُمْ مِنَ الْمُشْرِكِينَ {1}

(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina.

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّهِ ۙ وَأَنَّ اللَّهَ مُخْزِي الْكَافِرِينَ {2}

Basi tembeeni katika nchi miezi minne; na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwadhalilisha makafiri.

وَأَذَانٌ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّهَ بَرِيءٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ ۚ فَإِنْ تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۖ وَإِنْ تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّهِ ۗ وَبَشِّرِ الَّذِينَ كَفَرُوا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ {3}

Na ni tangazo litakalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa watu siku ya Hijja kubwa ya kwamba Mwenyezi Mungu amejitoa na washirikina na pia Mtume wake. Basi kama mkitubu ndiyo heri kwenu, na kama mkikengeuka, basi jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu na wabashirie waliokufuru adhabu iumizayo.

إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدْتُمْ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنْقُصُوكُمْ شَيْئًا وَلَمْ يُظَاهِرُوا عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوا إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ {4}

Ispokuwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina kisha hawakuwapunguzia chochote wala hawakumsaidia yeyote juu yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye takua.