Aya 1 – 3: Kitabu Kimeteremshwa Kwako
Maana
Alif Lam Swad
Hizi huandikwa na kutamkwa kwa majina ya herufi zake kama zilivyo. Yamepita maelezo yake katika Juz.1 mwanzo wa Sura ya pili (Al- Baqara).
Kitab kimeteremshwa kwako, basi isiwe dhiki kifuani mwako kwacho. Ili upate kuonya kwacho na kiwe ni ukumbusho kwa wanaoamini.
Maneno anaambiwa Mtume Muhammad (s.a.w.). Makusudio ya Kitab ni Qur’an, na waumini ni kila anayenufaika na Qur’an, ni sawa iwe ni sababu ya kuamini kwake au kuimarisha imani yao waendelee nayo.
Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameteremsha Qur’an kwa Mtume (s.a.w.) ili awaonye kwayo walahidi na washirikina na watu wa dini za ubatilifu; na ili wanufaike nayo watu wenye maumbile safi.
Kazi hii inampa uzito Mtume (s.a.w.) kutoka kwa makafiri ambao anawakabili kwa Qur’an. Kwa sababu, inalenga katika kubatilisha itikadi zao na hali zao ambazo wamezirithi kutoka kwa mababu zao wa jadi. Hapo Mtume alipata dhiki kutokana na inadi na upinzani wao.
Mwenyezi Mungu anasema:
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ {97}
Na akasema tena Mwenyezi Mungu:
إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا {5}
Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu.
Katika Aya iliyotangulia Mwenyezi Mungu amemwamrisha Mtume wake kufikisha na kutojali upinzani. Katika Aya hii anawaamrisha watu wamfu- ate Mtume na waitumie Qur’an.
Ali Al-Murtadha (a.s.) anasema: “Hatawaadhibu Mwenyezi Mungu watu wajinga kwa kutojifundisha, mpaka awaadhibu wenye elimu kwa kutofundisha.” Na kinyume chake pia.
Wala msifuate wasimamizi badala yake.
Kwa sababu hakuna badala ya Qur’an ila upotevu na matamanio.
Ni machache mnayoyakumbuka na hali mnawaidhika na mawaidha ya Mwenyezi Mungu na nasaha zake. Kwa sababu nyinyi hamwogopi mwisho utakuwaje; na anayewaidhika ni yule anayeogopa.
Kauli yake ‘ni machache mnayokumbuka’ ni kuashiria uchache wa wale wanaowaidhika.
وَكَمْ مِنْ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ قَائِلُونَ {4}
فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُمْ بَأْسُنَا إِلَّا أَنْ قَالُوا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ {5}
فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ {6}
فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِمْ بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ {7}
وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ {8}
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ {9}
وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ ۗ قَلِيلًا مَا تَشْكُرُونَ {10}