read

Aya 28-30: Wanapofanya Uchafu

Maana

Na wanapofanya machafu.

Dhamir inawarudia wale ambao hawaamini, waliotajwa mwisho wa Aya iliyotangulia. Kundi la wafasiri wamesema kuwa makusudio ya uchafu ni walivyokuwa wakifanya Waarabu wakati wa ujahilia kutufu Al-Kaaba wakiwa uchi, wake kwa waume. Lakini ilivyo hasa ni kuwa neno hilo linaenea yote ya haramu waliyokuwa wakifanya.
Wanapokatazwa husema:

Tumewakuta nayo baba zetu na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo.

Kitendo cha mababa kimekuwa ni hoja ya washirikina na wengineo; hata kwa maulamaa wengi wa kidini, lakini hawatambui. Ama madai ya washirikina kuwa Mwenyezi Mungu amewaamrisha machafu yameetole- wa dalili na Aya isemayo:

“Watasema walioshirikisha: Lau angelitaka Mwenyezi Mungu tusingelimshirikisha sisi wala baba zetu;” Mwenyezi Mungu akawarudi kwa kuwaaambia:

قُلْ هَلْ عِنْدَكُمْ مِنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِنْ تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنْتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ {148}

“Je, mnayo elimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana tu, na hamsemi ila uwongo tu.” (6:148).

Na hapa Mwenyezi Mungu akawarudi kwa kusema: Sema:

Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi machafu.

Bali “Shetani anawatisha na ufukara na anawaamrisha ubakhili”Juz.3 (2: 257).

Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua?

Na kila anayesema, bila ya ujuzi wowote, basi ni mzushi mwongo, na ameruka patupu.

Sema: Mola wangu ameamrisha uadilifu.

Nao ni usawa na msimamo. Amesema Tabrasi: “Uadilifu ni neno linaloku- sanya kheri zote.” Maana yoyote yatakayokuwa ni kuwa kuamrisha uadilifu ni kupinga madai yao kuwa Mwenyezi Mungu amewaamrisha uovu.

Na elekezeni nyuso zenu katika kila msikiti, na muombeni yeye tu kwa ikhlas.

Makusudio ya elekezeni nyuso zenu ni kumwabudu Mwenyezi Mungu. Neno ‘Masjid’ ni mahali pa kusujudia na pia wakati wa kusujudu.

Lakini limetumika sana kwa maana ya jengo maalum la ibada (msikiti) mpaka likawa ni jina lake mahsusi. Makusudio ya kila msikiti sio misikiti yote bali ni msikiti wowote.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu anawaamrisha kufanya ibada kwenye msikiti, kwa kumwabudu yeye tu kwa ikhlas katika dini yenu na ibada yenu.

Kama alivyowaumba kwanza ndivyo mtarudi kwake siku ya Kiyama kwa ajili ya hisabu na malipo. Hili ni kemeo na onyo kwa yule anayekhalifu aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa uadilifu, kufanya ibada na ikhlasi.

Kundi moja ameliongoa nao ni wale waliomfanya Mwenyezi Mungu ndiye mtawala wao na wakafuata amri yake na kujizuia makatazo yake, na wala wasihadaike na mambo ya shetani na ubatilifu wake.

Na kundi jingine limethibitukiwa na upotofu. Nao katika akhera wana adhabu kubwa. Hilo ni kuwa Hakika wao wamefanya mashetani kuwa watawala wao badala ya Mwenyezi Mungu. Na anayemfanya shetani kuwa msimamizi badala ya Mwenyezi Mungu basi amepata hasara kubwa.

Na wanadhani kwamba wao wameongoka katika kufanya machafu, kuwafuata mababa na kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo. Mwenyezi Mungu anasema:

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا {103}

الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا {104}

Sema: Je, tuwaambie wenye hasara zaidi kwa vitendo, ni ambao bidii yao imepotea katika maisha ya dunia, nao wanafikiri kuwa wanafanya vyema.” (18: 103-104).

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ {31}

Enyi Wanadamu! Chukueni mapambo yenu katika kila msikiti, na kuleni na kunyweni wala msifanye ufujaji (israf), hakika Yeye hawapendi wafanyao ufujaji (israf).

قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ {32}

Sema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amewatolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa wale walioamini katika maisha ya dunia, ni vyao tu siku ya Kiyama. Namna hii tunazieleza ishara kwa watu wajuao.

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَنْ تُشْرِكُوا بِاللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَنْ تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ {33}

Hakika Mola wangu ameharamisha mambo machafu yaliyodhihirika na yaliyofichika. Na dhambi,na dhulma bila ya haki. Na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia dalili. Na kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ {34}

Kila umma una muda, utakapofika muda wao hawatakawia (hata) saa moja wala hawatatangulia.