Sura Ya Saba: Sura Al-A’raf
Imeteremshwa Makka, isipokuwa Aya 163, Mwenye Majmau anasema imeshuka Madina. Ina Aya 205.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
المص {1}
Alif Lam Mim Swad
كِتَابٌ أُنْزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُنْ فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِنْهُ لِتُنْذِرَ بِهِ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ {2}
Kitab kimeteremshwa kwako, basi isiwe dhiki kifuani mwako kwacho ili upate kuonya kwacho na kiwe ni ukumbusho kwa wanaoamini.
اتَّبِعُوا مَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ {3}
Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu. Wala msifuate wasimamizi badala yake. Ni machache mnayoyakumbuka.