read

Watu Wa Peponi Wataita Aya 44 – 45

Maana

Na watu wa Peponi watawanadia watu wa Motoni kwamba tumekuta aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli. Je, nanyi pia mmekuta aliyowaahidi Mola wenu kuwa kweli?

Watu wa Peponi wanajua fika kwamba watu wa Motoni wamekuta ukweli waliyoahidiwa na kutishiwa, lakini wao watawaelekezea swali hili kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya aliyowaneemesha na kuwakumbusha yale waliyokuwa wakiyasema yakiwa ni pamoja na dharau na stihzai kwa dini ya haki na wafuasi wake.

Watasema ndio.

Maana hakuna njia ya kukataa.

Basi mtangazaji atatangaza kati yao kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu.

Kwa laana hii, mtangazaji atainua sauti siku ya Kiyama akiwataja madhal- imu kwa sifa tatu:

1. Ambao wanazulia njia ya Mwenyezi Mungu. Yaani wanawazuia watu kuifuata haki kwa njia mbali mbali.

2. Na wakataka kuipotosha. Hawataki ukweli na ikhlasi wala msimamo, isipokuwa wanataka uwongo, unafiki na hiyana.

3. Nao hawaiamini Akhera. Hawaogopi hisabu wala adhabu kutokana na makosa yao na madhambi.

وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ {46}

Na Baina Yao Patakuwa Na Pazia. Na Juu Ya A’raf Watakuwako Watu Watakaowafahamu Wote Kwa Alama Zao. Na Watanadia Watu Wa Peponi: Salamun Alaykum. Hawajaingia Nao Wanatumai.

وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ {47}

Na Macho Yao Yanapogeuzwa Kuelekea Watu Wa Motoni, Husema: Mola Wetu Usituweke Pamoja Na Watu Waliodhulumu.

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُمْ بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنْكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ {48}

Na Watu Wa A’raf Watawanadia Watu Wanaowafahamu Kwa Alama Zao, Waseme: Haukuwasaidia Mjumuiko Wenu Wala Mlivyokuwa Mkijivunia.

أَهَٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنْتُمْ تَحْزَنُونَ {49}

Je, Hawa Ndio Wale Mliokuwa Mkiwaapia Kwamba Mwenyezi Mungu Hatawafikishia Rehma? Ingieni Peponi, Hakuna Hofu Juu Yenu Wala Hamtahuzunika.