read

Aya 142: Nini Kilichowageuza Kutoka Qibla Chao?

Lugha

Amesema Ibnul Arabi katika tafsiri yake: “Kila asiyejua hakika ya Dini ya Kiislamu huyo ni mpumbavu, kwa sababu yeye ana akili hafifu. Neno Qibla limechukuliwa kutoka katika neno Istqbal (kuelekea); yaani kila upande anaoulekea mtu.

Maana

Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: Nini kilichowageuza kutoka Qibla chao walichokuwa wakikielekea?

Mitume waliotangulia walikuwa wakiswali kuelekea Baitul Maqdis. Na Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akitamani lau Qibla kinageuzwa kuwa Al-Kaaba. Mwenyezi Mungu aliyathibitisha matamanio yake, kama itakavyoelezwa.

Makusudio ya wapumbavu hapa ni Mayahudi, ndio waliowalaumu Waislamu kwa kuacha kwao kuelekea BaitulMaqdis.

Tamko Sayaqulu (Watasema) kwa dhahiri linafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu alimfahamisha Mtume wake Mtukufu kauli ya wajinga kabla ya kutokea. Ama yule anayesema kuwa neno Sayaqulu ingawaje kwa dhahiri linafahamisha muda wa mbele, lakini makusudio ni muda uliopita; na kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume wake baada ya kusema wajinga, sio kabla ya kusema; na kwamba limekuja kwa muda ujao, kwa vile yaliyosemwa yalikuwa yamekwisha kadiriwa, ama kwa hakika kauli hii ni kujaribu kutoa tafsir nyingine (Taawil) bila ya dharura yoyote na bila ya dalili yoyote inayofahamisha hilo.

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) kuwajibu wajinga hawa kwamba: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; humwongoza amtakaye katika njia iliyonyooka. Yaani pande zote ni za Mwenyezi Mungu:

Al-Kaaba na Baitul Maqdis ni sawa tu, lakini kwa hekima na masilahi mara nyingine humwongoza anayemtaka kwenye Baitul-Maqdis na mara nyingine kwenye Al-Kaaba.

Kwa Nini Kuswali Upande Maalum?

Hili ni swali wanaloliuliza watu wengi kwa nini swala ni wajibu kwenye upande malum na haiswihi isipokuwa upande huo? Na hali yeye amekwisha sema waziwazi: Na popote mnakoelekea (mtazikuta) radhi za Mwenyezi Mungu (2:115).

Jibu: Kwanza Mwenyezi Mungu s.w.t. amesema: “...Na elekeza uso wako upande wa msikiti Mtakatifu (Al-Kaaba); na popote mlipo zielekezeni nyuso zenu upande huo...” (2:144).

Aya hii ni ubainifu na Tafsir ya Aya 115 na makusudio yake ni kuelekea kwenye upande wowote katika swala ya Sunna na katika swala ya asiyejua Qibla kiko wapi. Makusudio ya Aya 144 ni kuelekea (Al-Kaaba) katika swala ya wajibu. Umekwishatangulia ufafanuzi wa hilo katika Aya 115.

Pili, kuswali swala kunategemea amri ya Mwenyezi Mungu. Kutokana na asili hii hapana budi tuangalie: Je inawezekana tuswali upande wowote tunaoutaka sisi au kwenye upande maalum. Ikiwa kauli ya kwanza ni sawa, basi itakuwa haiswihi swala isipokuwa kwenye upande ulioamrishwa tu; ni sawa iwe ni Al-Kaaba au Baitul-Maqdis au mahali pengine.

Pia ifahamike kwamba kufuata amri ni jambo jengine na kuweko radhi za Mwenyezi Mungu kila upande ni jambo jengine.

Hakika ibada ni katika mambo yanayongoja ubainifu wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume wake, wala hakuna nafasi ya dhana na uwezekano; isipokuwa kwa kauli sahihi iliyo wazi. Na Mwenyezi Mungu aliaamrisha Waislamu kuswali kuelekea Baitul-Maqdis kwanza; lau wangeliswali kuelekea Al-Kaaba isingekubaliwa swala yao. Kisha Mwenyezi Mungu akawaamrisha kugeuka Al-Kaaba lau wangeling’ang’ania Baitul-Maqdis basi isingekubaliwa swala yao; pamoja na kuwa pande zote mbili ni za Mwenyezi Mungu. Hilo ni kwa sababu kipimo cha kusihi swala ni kuafikiana na sharti zote; kama vile ambavyo kuharibika swala ni kuhalifu amri.

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنْتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَنْ يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّنْ يَنْقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِنْ كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَحِيمٌ {143}


Nakamahivyohivyotume


wafany


a


kuw


a


umm


a


wa


wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu wote, na Mtume awe shahidi juu yenu.Na


hatukukifany


a


Qibl


a


ulichokuw


a


nach


o


il


a


tupate kumju


a


yul


e


anayemfuata


Mtumenayuleatakayegeuka akarudi nyuma .Na kwa


hakik


a


lilikuw


a


n


i


jambo


gum


u


isipokuw


a


kw


a


wale


aliowaongoz


a


Mwenyezi Mungu


.


N


a


hakuwa


MwenyeziMungunimwenye


kuwapoteze


a


iman


i


yenu. Hakik


a


Mwenyez


i


Mungu


kwa watu ni Mpole Mwenye ku


r


ehemu.