read

Aya 146-147 -Wanamjua Kama Wanavyowajua Watoto Wao

Maana

Wale tuliowapa kitabu wanamjua kama wanavyowajua watoto wao.

Yaani wanavyuoni wengi wa Kiyahudi na wa Kikristo wanajua kwa usahihi na uwazi Utume wa Muhammad (s.a.w.w); kama wanavyowajua watoto wao, kwa namna isiyokuwa na shaka yoyote. Kwa sababu Tawrat na Injil zimetoa bishara ya kuja kwake na zikamtaja kwa sifa zake na alama zake ambazo hazikupatikana kwa mwingine yeyote. Mwenyezi Mungu anasema: “...Wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurat na Injil...” (7:157).

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِنْ بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَٰذَا سِحْرٌ مُبِينٌ {6}


“NaaliposemaIssabinMaryam:EnyiwanawaIsrail! MiminiMtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu katika


T


awratnakutoabisharayaMtumeatakayekujabaadayanguambaye jinalakeniAhmad. Lakinialipowajiakwahojazilizowazi,walisema: Huuniuchawiuliowazi.”(61:6).

Abdallah bin Salam alikuwa ni mmoja wa maulamaa wa kiyahudi; kisha akasilimu. Miongoni mwa maneno aliyosema ni: “Mimi ninaujua zaidi Utume wa Muhammad kuliko ninavyomjua mwanangu.” Alipoulizwa kwa nini, alisema: “Mimi sitii shaka kwamba Muhammad ni Mtume, lakini mtoto wangu, pengine mama yake amefanya hiyana.”

Na hakika kundi katika wao wanaificha haki na hali wanaijua.

Ndio! wanaficha, hata kama wangeliona jina la Muhammad katika Lauhul Mahfudh, kwa sababu ya kupupia uongozi wa duniani na maslahi ya kibinafsi. Inadi hii ya kuficha haki haihusiki na Mayahudi na Wakristo tu. Kwani sababu ya kuficha haki ni ya kijumla. Tumekwisha waona baadhi ya Masheikh wanakana sifa za wenzao kwa sababu ya chuki na hasadi tu.

Haki ni iliyotoka kwa Mola wako, basi usiwe miongoni mwa wanao- fanya shaka.

Mtume (s.a.w.w) hawezi kutia shaka yale yaliyotoka kwa Mola wake na ni muhali kuyatilia shaka; na Mwenyezi Mungu anajua kuwa Mtume wake Mtukufu hawezi kutia shaka. Lengo la Aya hii ni kubainisha kwamba aliyomteremshia Muhammad hayana shaka wala matatizo yoyote kabisa. Mtu akiyakanusha na kuyapinga basi atakuwa anafanya hivyo kwa inadi na ukaidi tu.

Mimi Na Mhubiri

Tarehe 15-7-1963 alinitembelea mtaalamu wa mambo ya nchi za mashariki Mkristo kutoka Italia ambaye alikuwa akizungumza lugha ya Kiarabu vizuri. Basi tukawa na mjadala kwa mdomo na kwa maandishi. Miongoni mwa aliyosema ni “Qur’an inakiri wazi wazi kuhusu Injil, kwa nini Waislamu wanaikana?” Nikamjibu kuwa Qur’an inakiri Injil iliyobashiri Utume wa Muhammad (s.a.w.w); kama ilivyosema: “...Na mwenye kutoa bishara ya Mtume atakayekuja baada yangu ambaye jina lake ni Ahmad...” (61:6). “...Wanamuona ameandikwa kwao katika Tawrat na Injil...” (7:157).

Kisha Qur’an inaendelea kusema: “Hakika mfano wa Issa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia ‘kuwa basi akawa. (3:59).

Injil yenu inasema Issa ni Mungu, sasa vipi mnatutaka tuiamini na wakati huo huo tuiamini Qur’an? Ikiwa Wakristo wanakataa kupingana na kukosana katika hukumu ya akili tu, na kukubali kuwa akili inaweza kupingana na kutoafikiana katika dini na itikadi, basi Waislamu wanaliona hilo ni muhali; haliwezekani kiakili na kidini na katika kila kitu. Kwa sababu misingi ya dini kwao inakuwa ndani ya akili tu.

وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {148}


Na kila mmoja ana mwelekeo anaouelekea. Basi shindaneni kufanya mema. Popote mtakapokuwa, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. HakikaMwenyeziMunguni


Muwezawakilakitu.

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ ۗ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ {149}


Napopoteuendapoutakako


kuw


a


elekez


a


us


o


wako


kweny


e


Msikit


i


Mtakatifu;


na hiyo ndiyo haki itokayo


kw


a


Mol


a


wako


.


Na


Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda.

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنْتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ {150}


N


apopot


eutakapotoka


utakokuwa elekeza uso wako


upand


e


w


a


Msikiti


Mtakatifu, na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande (uliko msikiti) huo ili watu


wasiw


e


n


a


hoj


a


ju


u


yenu,


isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi


msiwaogope


,


niogopeni


Mimi, iliniwatimizie neema Zangu na ili mpate kuongoka.

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِنْكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُمْ مَا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ {151}


Kam


atulivyomlet


aMtume


kwen


u


anayetokan


a


na nyinyi


,anayewasome


a


A


y


a


zet


u


n


a


kuwatakas


a


na kuwafundish


a


Kitab


u


na hekim


a


n


a


kuwafundisha


mliyokuwahamyajui.

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ {152}


Bas


i


nikumbukeni nitawakumbuka


,


na


nishukuruni wala msinikufuru.