read

Aya 148-152: Kila Umma Ulikuwa Na Qibla Chake

Maana

Na kila mmoja ana mwelekeo anaoulekea.

Alipotaja Mwenyezi Mungu Qibla ambacho amewaamrisha Waislamu kukielekea ambacho ni Al Ka’aba, na akataja kuendelea kwa Mayahudi na Manaswara kuelekea mielekeo yao, alibainisha kuwa siri ya kung’ang’ania huku kwamba kila umma ulikuwa na Qibla chake uliojichagulia kuelekea na wala haukiachi, hata kama ubaya wa mwelekeo wenyewe uko wazi kama jua. Kwa hiyo kauli Yake hii inafanana na kauli Yake:

كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ {32}


“...Kilakikundikinafurahiakilichonacho”(30:32).

Hayo ndiyo niliyoyafahamu kutokana na dhahiri ya tamko. Wafasiri wameleta kauli nyingi katika Aya hii; mwenye Majmau ametaja nne.

Basi shindaneni kufanya mema. Popote mtakapokuwa Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja, hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Yaani achaneni na watu wa Kitab na washirikina walio wakaidi, na mfanye amali njema. Kwani marejeo yenu kesho ni kwake Mwenyezi Mungu, ambapo atalipwa thawabu mwenye haki na mwenye kufanya wema na kuadhibiwa mwenye batili mtenda maovu. Kama wanavyosema wafasiri maana ya: “Popote mtakapokuwa Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja” ni ahadi ya thawabu kwa watiifu na kiaga cha adhabu kwa waasi. Ama kusema kwake: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu” ni dalili na sababu ya kuwezekana kufufuliwa viumbe baada ya mauti.

Na popote uendapo elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu hapa amekariri kuelekea Msikiti Mtakatifu mara tatu na katika Aya ya 149 mara mbili; yaani amekariri mara tano mfululizo?

Jibu: Mwenye Majmaul-Bayan ametaja kauli tatu na Razi ameleta tano. Miongoni mwa kauli hizo ni lile jibu lililozoeleka linalorithiwa ambalo ni, kutilia mkazo na umuhimu. Nafsi yangu haikutulia kabisa katika kauli hizo. Na mimi sina chochote cha kusema isipokuwa huenda kukariri huku hapa ni kutokana na jambo lililohusu wakati huo ambalo hatulijui. Kuna mambo mengi ambayo hayaingii katika udhibiti na hisabu.

Inajulikana wazi kuwa mapokezi ya Aya na sababu zake yako ya kiujumla na mahsusi, na haifai kwa yeyote kutafsiri au kuleta taawili, kwa kutegemea dhana bila ya kupata asili yake yoyote.

Ili watu wasiwe na hoja juu yenu.

Wafasiri wengi wamesema kuwa Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akiswali kuelekea Baitil Maqdis; Washirikina na Waarabu wakasema: “Vipi Muhammad anadai kwamba yeye yuko kwenye dini ya Ibrahim, na wala haswali kuelekea Al Ka’aba aliyokuwa akiswali Ibrahim na Ismail?” Na watu wa Kitab wakasema “Yaliyo katika Vitabu vyetu ni kwamba Mtume atakayeletwa katika kizazi cha Ismail ataswali kuelekea Al Ka’aba na wala sio Baitul Maqdis, sasa vipi tunaweza kuukubali Utume wa Muhammad. Kwa hiyo wakaifanya kuwa hoja, wanayoitumia kwa dhana yao. Mwenyezi Mungu akambadilishia Qibla kuelekea Al Ka’aba na akaifanya ndio Qibla cha kudumu kwa Mtume na Waislamu wote mpaka siku ya malipo, ili hawa na wengine wasibakiwe na hoja yoyote.

Dhahiri ya jumla inafahamisha kwamba kuswali kuelekea Al Ka’aba kunavunja hoja ya wapinzani. Ama kuwa ni kina nani hao wapinzani, Aya haikubainisha. Inawezekana kuwa njia ya kukata hoja ya wapinzani ni kuwa Al Ka’aba imejengwa na Ibrahim (a.s.) na akaswali hapo. Hilo ni lenye kuafikiwa na wote na Muhammad atafuata mwendo wa Ibrahim

Isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao.

Yaani hakuna hoja yoyote juu yako ukiswali, isipokuwa kwa mpinzani asiye na haki ambaye hategemei dalili za kiakili katika upinzani wake wala uongozi wa kidini isipokuwa kung’ang’ania, na ukaidi.

Basi msiwaogope, niogopeni Mimi.

Yaani msiogope lawama katika haki, Mimi pekee ndiye ninayewamilikia manufaa na madhara. Ibnul Arabi katika tafsiri yake anasema. Maana ya niogopeni ni, jueni Utukufu Wangu ili makafiri wasijifanye watukufu kwenu.

Amirul Muminin (a.s.) anasema: “Amekuwa mkubwa Muumbaji katika nafsi zao akawa mdogo asiyekuwa yeye katika macho yao.”

Na ili niwatimizie neema zangu na ili mpate kuongoka.

Yaani nimewaneemesha kwa Uislamu na nimewatimizia neema kwa kuwa- pa Qibla chenu kilichowafanyia umoja na kuwakusanya na kinachoelekewa na watu wa mataifa mbali mbali ya pembe zote za dunia, yenye makabila na lugha mbali mbali.

Katiba Ya Uislamu

Mtaalamu mmoja anasema kuwa katiba ya Uislamu ina vipengele vitatu Mwenyezi Mungu mmoja, Kitabu kimoja na Qibla kimoja. Waislamu hukusanyika kutoka pembe zote za dunia kila mwaka ili wamwabudu Mwenyezi Mungu mmoja kwa sharia hiyo moja kwenye nchi mmoja, nchi ya mji wa kiroho. Hivi ndivyo ulivyokuwa umoja wa itikadi, sharia na mji, ili wakumbuke Waislamu kwamba wao hata kama wakitofautiana miji, lugha, rangi na nasaba, lakini wanakuwa wamoja kwa dini, wanaabudu Mwenyezi Mungu mmoja na ni wananchi wa nchi mmoja.

Kama tulivyomleta Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anayewasomea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima na kuwafundisha mliyokuwa hamyajui.

Wanavyuoni wana maneno mengi na marefu katika maana ya neno hekima. Tunavyofahamu sisi ni kuwa kila kinachowekwa mahali pake pana- postahili, kiwe ni kitendo au kauli, basi ni hekima.

Hali yoyote iwayo, maana ya jumla ya Aya hii ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaneemesha Waarabu kwa Qibla; kama alivyowaneemesha kwa Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni katika wao na anatokana na wao. Amewapa umbo jipya; akawatwaharisha na uchafu wa shirk na tabia mbaya. Kwa hiyo, kwa fadhila zake, wakawa ni watu wa dini na sharia ya Mwenyezi Mungu ambayo misingi yake ni uadilifu na usawa; kama ambavyo wamekuwa na dola iliyopanuka, mpaka lugha yao ikawa kubwa na ikaenea kwa sababu ya Qur’an na fasihi yake.

Hapana mwenye kutia shaka kwamba lau si Muhammad na kizazi cha Muhammad, Waarabu wasingelikuwa na historia wala turathi zozote; wasingekuwa na chochote zaidi ya kuabudu masanamu, ujinga na kuwazika watoto wa kike wakiwa hai, ili kuepuka gharama za kuwalisha. Bali Muhammad (s.a.w.w), Mwarabu, ni neema kubwa juu ya watu wote. Kwa sababu yake, watu wamepiga hatua za haraka katika nyanja za elimu na maendeleo. Uhakika huu wameukiri na kuusajili wataalamu wa Kimagharibi wale wasiokuwa na ubaguzi, na tumeyanakili baadhi katika kitabu Al-Islam Wal-aql (Uislamu na Akili).

Kwa ajili ya neema hiyo aliyowaneemesha Waarabu, ndio Mwenyezi Mungu akawataka wamkumbuke na kumshukuru na akahadharisha wasije wakaikufuru neema na hisani, kwa kusema: Basi nikumbukeni nitawakumbuka na nishukuruni wala msinikufuru.

Yaani nikumbukeni kwa utii nami nitawakumbuka kwa malipo na thawabu. Na mnishukuru juu ya neema ya Uislamu na Utume kwa Muhammad ambaye anatokana na nyinyi wala msinikufuru. Mahali pengine Mwenyezi Mungu anasema: “...Kama mkishukuru nitawazidishia, na kama mkikufuru basi adhabu yangu ni kali sana.” (14:7).

Amirul Mumini Ali (a.s.) alisema: “Mwenyezi Mungu hawezi kufungua mlango wa shukrani na akafunga wa malipo.” Anaendelea kusema: “Mkumbukeni sana Mwenyezi Mungu, kwani huo ndio ukumbusho mzuri, na kuweni na raghba katika aliyowaahidi wanaomcha Mwenyezi Mungu, kwani ahadi Yake ni ya kweli sana.”

Kumshukuru Mneemeshaji

Moja kwa moja akili inafahamu kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ni wajibu kwa kila aliye baleghe mwenye akili, hata kama isingeshuka Aya yoyote au kuja Hadith yoyote ya kuwajibisha kushukuru. Kwani Yeye Mtukufu ndiye Muumbaji Mwenye kuruzuku.

Maana ya kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baada ya kuitakidi kwamba Yeye ndiye mwanzilishi na kwamba Yeye ni muweza wa kila kitu ni kutii amri Zake na makatazo Yake na kutegemeza mambo kwake peke Yake. Hayo ni kwa upande wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Ama mtu akimfanyia wema mtu kama yeye, je inapasa, yule aliyefanyiwa wema kumshukuru aliyemfanyia wema, kiasi ambacho kama hakumshukuru kwa namna fulani atakuwa ni mwasi mwenye kustahiki adhabu?

Hapana mwenye kutia shaka kwamba kumshukuru aliyekutendea wema ni jambo zuri, bali hiyo ni alama ya watu wema. Ama kuwa ni wajibu au la, hakuna dalili juu yake. Kwa hiyo kila habari iliyokuja kuhusu kumshukuru mwenye kutoa neema asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Mtume au Ahlul Bait wake, ni pendekezo tu ya kuwa ni vizuri; kama alivyosema Ali (a.s.): “Ukiwa unammudu adui yako, basi ufanye msamaha ndio shukrani ya uwezo huo wa kummudu”.

Kumsamehe aliyekufanyia ubaya sio wajib, lakini ni Sunna kwa Ijmai. Ama msemo unaosemwa sana: “Asiyeshukuru kiumbe ndio hamshukuru Muumba”, hiyo ni hukumu ya kimaadili tu, siyo ya lazima.

Hata hivyo kukanusha neema na kumwambia aliyekufanyia wema: “Hukufanya wema” ni haramu, kwa sababu ni uwongo; na kumfanyia uovu ndio haramu kabisa, kwa sababu uovu ni haramu kwa dhati yake, hata kwa mtu asiyekufanyia wema. Lakini pamoja na hayo wajibu wa kushukuru ni jambo jingine na uharamu wa uwongo na uovu ni jambo jingine.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ {153}


Enyi mlioamini!


T


akeni msaadakwasubiranaswala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.

وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتٌ ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَٰكِنْ لَا تَشْعُرُونَ {154}


Walamsisemekwambawale


waliouaw


a


katik


a


nji


a


ya


Mwenyezi Mungu ni wafu,


bal


i


w


a


ha


i


lakin


i


nyinyi


hamtambui.

وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ {155}


Nahakikatutawajaribukwa chembe ya hofu na njaa na


upunguf


u


w


a


mal


i


n


a


wa


nafsi na wa matunda.Na wapebisharawanaosubiri.

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ {156}


Amba


oukiwapat


amsiba,


husema: Hakikasisiniwa MwenyeziMungu,naKwake


Y


eyetuta


r


ejea.

أُولَٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ {157}


Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na


r


ehema, na hao ndio wenye kuongoka.