read

Aya 153-157: Takeni Msaada Kwa Subira

Subira

Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na swala; hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.

Mwenye Tafsiri ya Al-Manar anasema kuwa Subira (uvumilivu) katika Qur’an imetajwa mara sabini. Hiyo inafahamisha umuhimu wake, na Mwenyezi Mungu ameijaalia ni kitu cha kuusiana katika Sura Al Asr kwa kuikutanisha na haki, kwani mwenye kuilingania haki hana budi kuwa nayo.”

Mwenye Bahrul Muhit ameiweka mbali sana aliposema: “Subira na swala ni nguzo mbili za Uislamu” Ameghafilika na Hadith inayosema: “Umejengwa Uislamu juu ya mambo matano: Kushuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga mwezi wa Ramadhan na kuhiji Makka kwa mwenye kuweza njia ya kuendea.” Subira haimo katika nguzo hizo. Pia ameghafilika kuwa kuna taklifa za lazima ambazo Mukallaf anatakiwa kuzifanya na ataadhibiwa kwa kuziacha; kama, swala kulipa deni, n.k.

Na kuna taklifa nyingine ambazo ni za kimwongozo, zimekuja kinasaha, zinafanana na amri, lakini mukallaf hawezi kuadhibiwa kwa kuziacha; kama usafi, kuosha mikono kabla ya kula, kukatazwa kushiba sana, n.k. Sasa yako wapi haya na nguzo za dini, ambazo mwenye kuziacha anakuwa ametoka katika dini?

Kisha subira haisifiwi hiyo yenyewe hasa, isipokuwa inasifiwa ikiwa ni nyenzo ya kufikilia jambo kuu; kama subira katika jihad takatifu, subira juu ya ufukara na uhitaji, subira kwa ajili ya kuipata elimu na subira juu ya matatizo ya familia na kulea watoto.

Vile vile subira juu ya kumwokoa mwenye kudhulumiwa, subira juu ya kauli ya mtu mpumbavu kwa kukinga shari, au kufanya subira kwa kumkosa mpenzi asiyesahaulika. Kwani kuendelea kufazaika ni kuzidisha msiba; kama alivyosema Amirul Muminin Ali (a.s.): “Mwenye kuyakuza masaibu madogo, Mwenyezi Mungu humwingiza kwenye makubwa.”
Bazar Jamhar aliulizwa: “Kwa nini ewe mfalme mwenye hekima husikitiki kwa yaliyokupita wala hufurahi kwa yaliyopo?” Akasema: “Yaliyopita hayawezi kufutika kwa majonzi wala yaliyopo hayawezi kudumu kwa furaha.” Mwingine alisema: “Siwezi kusema kitu kilichokwisha kuwa na tamani kisingekuwa au ambacho hakikuwa natamani kingekuwa.

Mara nyingine subira huwa mbaya; kama kusubiri juu ya njaa na uwezo wa kufanya kazi upo, na kusubiri juu ya ukandamizwaji. Katika hali hii subi- ra nzuri ni kumkabili dhalimu. Unaweza kuuliza, kuna uhusiano gani kati ya swala na subira mpaka zikakutanishwa pamoja katika Aya?

Jibu: Maana ya subira ni kutulizana moyo ingawaje una machungu. Hiyo inahitajia kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuamini kuwa Yeye “Yu pamoja na wenye kusubiri”. Hakuna mwenye shaka kwamba swala inatilia mkazo mategemeo haya na ni hakikisho la imani hii, kuongezea kwamba kumwomba Mwenyezi Mungu kunapunguza machungu ya masaibu.

Wala msiseme kwamba wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai, lakini nyinyi hamtambui.

Mfano wa Aya hii ni kama nyingine isemayo:

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ {169}W


alausiwadhaniewalewaliouawakatikanjiayaMwenyeziMungu kuwaniwafu,baliwahaiwanaruzukiwakwaMola wao.”(3:169).

Inajulikana kuwa kila anayefariki hurejea kwa Mola wake, awe mwema au mwovu, shahidi au asiyekuwa shahidi; isipokuwa kwamba mwema anaondoka kwenye maisha ya chini kwenda kwenye maisha ya juu na mwovu inakuwa kinyume chake.

Hapa imehusishwa kutajwa shahidi; ama ni kwa kueleza cheo chake mbele za Mwenyezi Mungu kwa kuhimiza ushahidi; au ni kwa kutokana na yaliyonakiliwa kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Aya ilishuka kwa sababu ya waliouliwa katika vita vya Badr ambao ni Muhajirin kumi na nne na Ansar wanane; ikasemwa ameuawa fulani na fulani; ndipo ikashuka Aya hii. Haya hayako mbali, kwani kauli ya Mwenyezi Mungu: Msiwaite wafu, inafahamiisha hilo.

Vyovyote iwavyo, ambalo tunapaswa kuamini ni kwamba mwenye kufa shahidi kwa kuupigania Uislamu au kitu chochote kinachofungamana na haki, uadilifu na utu, atakuwa anahama kutoka ulimwengu unaoonekana kwenda kwenye ulimwengu usioonekana na huko atakuwa na maisha mema. Na kwamba yeye anatofautiana na aliyekufa kifo cha kawaida. Amirul Muminin anasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi ya mtoto wa Abu Twalib iko mikononi mwake, kupigwa mapigo elfu ya panga ni bora kwangu kuliko kufa kitandani.”

Ama hakika ya maisha ya shahidi baada ya mauti na kuhusu riziki anay- oneemeshwa ni jambo tusilolijua na wala hatuna haja ya kulifanyia utafiti. Kwa sababu ni jambo tusilokalifishwa kulijua.

Thamani Ya Pepo

Na hakika tutawajaribu kwa chembe ya hofu na njaa na upungufu wa mali na wa nafsi na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri.

Yeyote anayefuata haki ni lazima aigharimie kwa nafsi yake, watu wake au mali yake; na kila haki inavyokuwa kubwa, ndivyo gharama inavyokuwa kubwa, lau kama si hivyo wanaopigania haki wasingelikuwa na fadhla yoyote; na watu wote wasingelifuata haki. Kwa hali hiyo ndiyo tunapata tafsiri ya Hadith hii tukufu: Misukosuko amepewa mumin na kwamba wenye misukosuko zaidi ni Mitume; kisha wanaowafuatia.” Vile vile misukosuko ya Mitume inakuja kwa kadiri ya daraja zao.

Mtume mtukufu (s.a.w.) amesema: “Hakuudhiwa Mtume kama nilivyoudhiwa mimi.” Amirul Muminini amesema: “Hakika haki ni nzito lakini nzuri, na batili ni hafifu, lakini mbaya.” Inatosha kuwa ni ushahidi kauli yake Mwenyezi Mungu: “Mnadhani kuwa mtaingia peponi, na hali hamjajiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara.” (2:214).

Aya hii inafahamisha kuwa pepo haipati isipokuwa mwenye kujitolea mhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kujitolea mhanga hakuwi katika uwanja wa vita vya jihadi na watu wa shirk peke yake, bali machukivu yoyote anayoyavumilia mtu kwa ajili ya kuipigania haki na uadilifu ni kujitoa mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ni thamani ya pepo; hata kama kupigania kwenyewe ni kwa neno la kumjibu dhalimu kumsaidia mwenye haki.

Baada ya kuingilia kuandika tafsiri, nimekuwa na yakini isiyo na shaka yoyote kwamba hataingia peponi isipokuwa yule aliyeudhiwa na akavumilia kwa subira, ijapokuwa ni ukandamizwaji na balaa katika njia ya haki na uadilifu.

Kwa uchache ni kuifunga nafsi yake na yaliyoharamishwa au kufanya juhudi kwa ajili ya mwingine; hata kama ni mzazi au mtoto. Kipimo cha pepo ni kuvumilia mashaka kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu. Ama kuingia peponi kutokana na “raha mstarehe” ni jambo lililo mbali sana.

Ambao ukiwapata msiba husema: ‘Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea.

Maana ya, “hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu”, ni kukiri ufalme na utumwa; na maana ya “kwake Yeye tutarejea”, ni kukubali ufufuo baada ya mauti.

Kisha kujaribiwa kwa misukosuko ni mtihani ambao unadhihirisha hakika ya mtu. Mumin mwenye akili hayumbishwi na misukosuko; wala hawezi kupayuka payuka na maneno ya ukafiri na ufasiki na ujinga, bali anakuwa na subira; wala misukosuko haiwezi kumwondolea akili yake na imani yake.

Ama mwenye akili na imani dhaifu anatawaliwa na shetani, anafuata mwenendo wote wa kufuru na shutuma na hushuka chini kwenye udhalili. Kauli nzuri kuhusu haya ni ile ya bwana wa mashahidi, Hussein bin Ali, siku ya msiba wa Karbala “Watu ni watumwa wa ulimwengu na dini iko kwenye ndimi zao, wanaipeleka kule kwenye maisha yao wakijaribiwa na misukosuko, huwa wachache wenye dini.”

Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao, na rehema.

Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni takrima na ni cheo cha juu; na rehema Yake kwa waja wake ni huruma yake kwao na kuwaongoza kwenye heri na kuwaneemesha.

Katika Hadith imeelezwa: “Hakuna Mwislamu yeyote aliyepatwa na masaibu, akakimbilia amri ya Mwenyezi Mungu kwa kusema: ‘Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea. Ewe Mola wangu Wewe ndiwe unayeyatoshea masaibu yangu, basi nilipe katika masaibu hayo na unipe badali bora.’ isipokuwa Mwenyezi Mungu humlipa na humpa badali bora.”

Aina Ya Malipo Ya Wanaosubiri

Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewapa wenye kusubiri aina nane za malipo na utukufu:

1. Mapenzi: Mwenyezi Mungu anasema: “...Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao subiri.” (3:146).

2. Ushindi: Mwenyezi Mungu anasema: “...Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanao subiri.” (2:153).

3. Ghorofa za peponi: Mwenyezi Mungu anasema: “Hao ndio watakaolipwa ghorofa kwa kuwa walisubiri.” (25:75).

4. Malipo mengi: Mwenyezi Mugnu anasema: “Hakika wanaosubiri watapewa ujira wao pasipo hisabu...” (39:10).

5. Bishara: Mwenyezi Mungu anasema: “Na wape bishara wanaosubiri.” (2:155).

6. Baraka na rehema: Mwenyezi Mungu anasema: “Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema.” (2:157).

7. Uongofu: Mwenyezi Mungu anasema: “Na hao ndio wenye kuongoka.” (2:157).

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ {158}


Hakik


aSwafa


an


aMa


r


-w


ani


katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au


akafany


a


Umra


,


s


i


kos


a


kwake


kuvizunguuka. Na anayefanya heri, basi


Mwenyez


i


Mung


u


n


i


Mwenye shukran


i(na


)Mjuzi.