read

Aya 158: Swafa Na Marwa

Lugha

Swafa na Mar-wa ni vilima viwili vilivyoko Makka karibu na Al Ka’aba. Mahujaji na wanaofanya Umra huenda Saa’y kati ya vilima hivyo.

Maana

Hakika Swafa na Mar-wa ni katika alama za Mwenyezi Mungu.

Ibada ziko namna mbali mbali na wakati mbali mbali. Kwa kuangalia wakati, kuna zile za kila siku ambazo ni swala, na nyingine ni za kila mwaka ambazo ni kufunga Ramadhani na pia iko ya mara moja tu, katika umri nayo ni kuhiji kwa mwenye kuweza.

Hijja ni moja ya nguzo tano zilizojengewa Uislamu, ambazo ni: Shahada mbili, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga Ramadhan na kuhiji Al Ka’aba. Umrah ni ada kama Hijja, lakini katika Umrah hakuna kwenda Arafa, wala kulala Muzdalifa au kutupa mawe Mina. Utakuja ufafanuzi wake Inshaallah katika Aya ya 196 na Sura nyingine zinazozungumzia hilo.

Kwa ujumla ni kwamba aina zote za ibada ikiwemo Hijja hazina nafasi ya kufanyiwa Ijtihadi wala kuelezwa sababu yoyote; isipokuwa inatosha nasi (nukuu) ya Qur’an na Hadith tu na kila ambalo litazidi hayo, Mungu (s.w.t.) hajaliridhia.

Linaloonyeshwa na Aya hii, ni kwamba Swafa na Mar-wa ni sehemu za kufanyiwa ibada kunakoonyeshwa na kauli yake:

Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au kufanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka.

Kuzunguka huku ndiko kunakojulikana kwa jina la Saa’y kati ya Safa na Mar-wa. Ama namna ya kufunya Saa’y na idadi ya mizunguko yake na kuanzia Safa, utakuja ubainifu wake mahali pake Inshaallah.

Unaweza kuuliza kufanya Saa’y kati ya Swafa na Mar-wa katika Hijja ni wajibu kwa Ijmai pamoja na kuwa ibara ya “Si kosa” inafahamisha kufaa jambo hilo na wala sio lazima na kwamba hakuna dhambi kuliacha.
Jibu: Kauli yake Mwenyezi Mungu: “Si kosa” haikuja kubainisha hukumu ya Saa’y kuwa ni wajibu au la, isipokuwa imekuja kubainisha kuwa Saa’y ni sharia na Uislamu unaikubali na kuithibisha. Ama maarifa ya hukumu yake na je, ni faradhi au ni sunna, hayo yanafahamishwa na dalili nyingine

Zimekuja Hadith mutawatir za Mtume na wamekongamana Waislamu juu ya wajibu wa kufanya saa’y katika Hijja ya Kiislamu. Katika Majmaul-Bayan anasema Imam Jaffar Sadiq amesema: “Waislamu walikuwa wakiona kwamba Swafa na Mar’wa ni mambo yaliyozushwa wakati wa Jahiliya, ndipo akateremsha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Aya hizi”. Yaani anaziondoa dhana hizi na kubainisha kwamba Swafa na Mar-wa vinatokana na Uislamu tangu asili; washirikina wakivizunguukia huwa wanajikurubisha kwa masanamu, lakini Waislamu huwa wanavizungukia kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata amri yake.

Na anayefanya heri basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani (na) mjuzi.

Yaani anayefanya wema kwa kufanya Saa’y kati ya Safa na Mar-wa baada ya kutekeleza wajibu alionao, basi Mwenyezi Mungu atamlipa wema kwa wema wake. Shaakir (mwenye shukrani) ni katika sifa za Mwenyezi Mungu na maana ya Mwenyezi Mungu kumshukuru mja wake mtiifu, ni kuwa radhi naye na kumpa thawabu kutokana na shukrani yake na utiifu wake.

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنْزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِنْ بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ {159}


Hakika wale wanaoficha tuliyoyate


r


emsha, katika ubainifu na uwongofu, baada ya Sisi kuyabainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaani Mwenyezi Mungu na wanawalaaniwanaolaani.

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ {160}Il


a


wal


e


waliotub


u


na


kujirekebisha na wakabain


isha


,


bas


i


ha


o


nitawataka-


bali


a


toba


,


n


a


Mim


i


ni


Mwingi wakutakabali toba, Mwenyekurehemu.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَٰئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ {161}


Hakika wale waliokufuru, na wakafa hali ni makafiri, hao


ik


o


ju


u


ya


o


laan


a


ya Mwenyez


i


Mung


u


n


a


ya


Malaikanayawatuwote.

خَالِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنْظَرُونَ {162}


Humowatadumu, hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewamuda.