read

Aya 159-162: Wanaoficha Yalioteremshwa

Maana

Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha katika ubainifu na uwongozi, baada ya sisi kuyabainisha kwa watu kitabuni hao anawalaani Mwenyezi Mungu na wanawalaani (kila) wanaolaani.

Dhahiri ya Aya ni kwamba inaanzia habari nyingine isiyofungamana na yaliyo kabla yake. Makusudio ni kuwa kila mwenye kujua hukumu katika hukumu za dini ambazo ubainifu wake umekuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu au katika Hadith za Mtume wa Mwenyezi Mungu au katika hukumu ya akili na akaificha, basi yeye amelaaniwa mbele ya Mwenyezi Mungu na watu wa mbinguni na ardhini. Mwenyezi Mungu ameashiria hukumu ya akili kwa kusema “Uwongofu”.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Ubainifu ni dalili za kisharia na uwongofu ni dalili za kiakili...”

Laana haiko kwa watu wa Kitabu tu, bali inamhusu kila mwenye kuficha haki kwa vile:

1. Tamko la Aya halikufungwa na jambo lolote.

2. Lau tunakadiria kuwa mashukio ya Aya ni kutokana na waliyoyafanya watu wa Kitab ya kupotoa Tawrat na Injil, basi tutasema: mashukio hayafanyi hukumu iliyo shuka kuwa mah’susi; kama wasemavyo Wanafiqh, ambao wanakusudia kusema kuwa tukio mahsusi haliwezi kufanya tamko la kiujumla kuwa mahasusi.

1. Imethibiti katika elimu ya Usul kwamba kufungamana hukumu juu ya sifa kunafahamisha kuwa sifa ni sababu. Na hapa laana inafungamana na kuficha kwenyewe. Kwa hiyo inakuwa laana inaenea kwa kila chenye kufichwa.

2. Imekuja Hadith inayosema: “Mwenye kuulizwa elimu anayoijua, akaficha, atafungwa lijamu ya moto siku ya Kiyama.

Wameafikiana mafakihi kwa tamko moja kwamba kumfundisha asiye jua hukumu za dini yake ni dharura ya wajibu kifaya (wajibu wa kutosheana) kwa kila mwenye kuijua; wakiitekeleza baadhi basi jukumu limewaondokea wote; na wakiiacha wote, basi watastahili adhabu wote.

Maana ya laana kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ni kumtoa, mwenye kulaaniwa kutoka katika rehema Yake, na maana ya laana kutoka kwa Malaika na watu ni dua ya kutaka mwenye kulaaniwa atolewe katika rehe- ma ya Mwenyezi Mungu.

Ubaya Wa Adhabu Bila Ya Ubainifu

Jukumu la mwenye kukalifiwa na sharia aliye baleghe na mwenye akili timamu, mbele ya Mwenyezi Mungu hupimwa kwa kumfikia taklifa zenyewe na kuzijua, wala sio kupatikana taklifa. Kwa sababu kuacha kumfikia ni sawa na kutokuwepo.

Hata hivyo ni wajibu kwa kila mwenye kukalifiwa na sharia (makallaf) ata- fute na kufanya utafiti wa ubainifu na dalili za hukumu katika sehemu zinakopatikana na kuwaulizia wanaohusika katika dini na sharia, wala haifai kwake kufanya uzembe na kupuuza, kisha aje atoe udhuru kuwa hajui.

Kwa sababu mwenye kuzembea ni sawa na mwenye kufanya makusudi, bali huo uzembe hasa ni makusudi, kwa vile mzembe anakuwa amekusudia kuacha kutafuta na kusoma. Kama akifanya bidii na asipate lolote, basi atakuwa hana jukumu, hata kama ubainifu uko.

Hakika huu ni msingi ulio wazi kiakili; ni akili gani inayoweza kumlaumu mwingine, ambaye hakufanya uzembe, kwa jambo asilolijua? Wanavyuoni wa Fiqh wamesema kwa pamoja kuhusu msingi huu na umethibitishwa na sharia katika Aya kadhaa; kama Aya hii tunayoizungumzia; “Baada ya sisi kuzibainisha kwa watu.”

Pia Aya inayosema: “...Na sisi si wenye kuwadhibu mpaka tumpeleke Mtume.” (17:15). Katika Hadith za Mtume iko inayosema: “Umeondolewa umma wangu yale wasioyoyajua.” Tutayarudia maudhui haya kila tutakapofikilia kwenye Aya inayoyagusia Inshaallah.

Ila wale waliotubu na kujirekebisha na wakabainisha.

Yaani wale wanaoificha haki ni wenye kulaaniwa, isipokuwa wale waliotubu na kujuta kwa ikhlas katika toba kwa kuazimia kutorudia makosa; kisha wakayabainisha wazi wazi yale waliyokuwa wameyaficha mwanzo. Kwani kutubia kwa mwizi hakutoshi maadamu hajarudisha haki ya wenyewe.

Basi hao nitawatakabalia toba na Mimi ni Mwingi wa kutakabali toba Mwenye kurehemu.

Neno tawwab (mwingi wa kukubali toba) ni katika sifa za Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Ameikutanisha rehema na kukubali toba, kwa kukumbusha kuwa sababu ya kukubali kwake toba kwa aliyemfanyia uovu ni rehema Yake kwa waja wake.

Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ni makafiri, hao wana laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.

Hata mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu na akamkanusha, hukubaliwa toba yake akitubia na husamehewa na kurehemewa, wala hataadhibiwa isipokuwa yule atakayekufa akiwa ameng’ang’ania ukafiri na maasi, kwa sababu yeye katika hali hiyo anastahili laana ya watu wa mbinguni na wa ardhini.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu anasema: “Na ya watu wote” na inajulikana kuwa katika watu kuna wasio mlaani kafiri, hasa wale makafiri?

Jibu: Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu; “Na ya Malaika wote na ya watu wote” ni kwamba huyo kafiri yuko mahali pa laana ya watu wa mbinguni na wa ardhini, iwe wamemlaani au hawakumlaani; hata kama ni makafiri kama wao, yeye ni wa kulaaniwa tu. Katika Qur’an inaelezwa kwamba makafiri kesho watalaaniana wenyewe kwa wenyewe. “...Kisha siku ya Kiyama baadhi yenu watawakufurisha wengine na baad- hi yenu watawalaani wengine...” (29:25).

Humo watadumu, hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa muda humu, ni humo mwenye laana.

Maana ya kudumu katika laana ni kukaa milele katika athari ya hiyo laana ambayo ni moto. Razi anasema: “Maana ya ‘hawatapewa muda’ ni kwam- ba wakiomba muda hawatapewa na wakilia kutaka kuokolewa hawataokolewa na wataambiwa: ‘Nyamazeni wala msiseme’”. Mwenyezi Mungu apishie mbali.

Hukumu Ya Laana Katika Sharia

Kumlaani mtu ni haramu na ni katika madhambi makubwa kwa sababu ni uadui sawa na kuingilia mali; katika Hadith inaelezwa “Hakika laana ikitoka kwa mtu, huzunguka, ikimkosa humrudia mwenyewe.”

Ziko laana zilizoruhusiwa na sharia ambazo ni:-

1. Kafiri: Aya ni nyingi sana kuhusu kafiri, kama hii tunayoizungumzia. Ama Hadith zimepetuka kuwa Mutawatir. Miongoni mwazo ni ile iliyo katika kitabu Ahkamul-Qur’an cha kadhi Abu Bakr Al-Muafiri, aliyoitaja wakati wa kutafsiri (2:161), kwamba Mtume alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu hakika Amr bin Al-Aas amenikebehi na anajua kuwa mimi si mshairi, basi mlaani.”

2. Dhalimu: Awe Mwislamu au si Mwislamu, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu“Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalim” (7 : 44)

3. Mwenye kufanya ufisadi.

4. Mwenye kufitini na kusababisha zogo.

Ama laana ya wasiokuwa hao waliotajwa kuna mushkeli na kuangaliwa vizuri. Ndio, ni kweli kwamba mwenye kudhihirisha maasia bila ya kujali inajuzu kumsengenya, lakini kusengenya ni kitu kingine na laana ni kitu kingine. Ama wanavyotumia watu kuwalaani wanyama, n.k. ni upuuzi, unaofaa kutupiliwa mbali.

وَإِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَٰنُ الرَّحِيمُ {163}


NaMunguwenuniMungu


Mmoja


,


hakun


a


Mungu


isipokuwa


Y


eye,Mwingiwa


r


ehema,Mwenyeku


r


ehemu.

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنْفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنَ السَّمَاءِ مِنْ مَاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِنْ كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ {164}


Hakik


a


katik


a


kuumbwa


mbingu na ardhi na kuhitalifiana usiku na mchana, na


vyomb


o


ambavy


o


hupita


katik


a


bahar


i


pamoj


ana


viwafaavy


o


watu


,


n


a


maji aliyoyate


r


emsh


a


Mwenyezi


Mung


u


kutok


a


mawinguni,


nakwamajihayoakaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama, na mabadiliko


y


a


pep


o


n


a


mawingu yanayoamrishw


a


kupita


baina ya mbingu na ardhi, ni isharakwawatuwenyeakili.