read

Aya 163-164: Na Mungu Wenu Ni Mungu Mmoja

Maana

Na Mungu wenu ni Mungu mmoja, hakuna Mungu isipokuwa Yeye.

Amirul Mumini katika kumuusia Mwanawe Hassan (a.s.) alisema: “Ewe mwanangu! Jua kwaamba lau Mola wako angelikuwa na mwenzake, basi huyo mwenzake angelileta Mitume yake na ungeliona athari za ufalme na usultani wake, na ungelijua vitendo vyake na sifa zake.” Maelezo ya kukanusha ushirika yatakuja katika kufafanua Aya ya (17:42) (21:22) na (23:91).

Mbingu

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi.

Katika mbingu kuna nyota zinazozidi chembe za mchanga kwa idadi; nyota iliyo ndogo zaidi miongoni mwazo, ni ile ambayo ni kubwa zaidi ya ardhi mara milioni. Kila kundi la nyota linakuwa katika mkusanyiko mkubwa unaoitwa ‘Galaxy’ unaokusanya zaidi ya nyota milioni mia moja. Idadi ya mikusanyiko hiyo ni zaidi ya milioni mbili. Kila mji uko mbali na mwingine kwa masafa ya simu ya upepo ambayo umbali wake kufikiwa ni miaka milioni tatu, yaani mikusanyiko hiyo yote katika anga iliyo wazi ni sawa na nzi anayepotea katika dunia. Nyota zote hizo na sehemu zake zinakwenda kwa kipimo na utaratibu mzuri.

Huu ni mfano mmoja wa mamilioni ya mifano juu ya kudura ya Mwenyezi Mungu na ukubwa wake uliovumbuliwa na Sayansi. Na Qur’an tukufu bado inawaambia wavumbuzi hao:

وَمَا أُوتِيتُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا {85}


“...Nanyihamkupewaelimuilakidogo.”(17:85).

Ardhi

Ardhi ni tufe lililo hewani; inazunguuka mara moja katika kila baada ya masaa ishirini na nne, ambayo usiku na mchana unafuatana. Inaelea kandoni mwa jua mara moja kwa mwaka ambapo vinafuatana vipindi vinne kwa mwaka. Ardhi inazunguukwa na mfuniko wa gesi yenye mchanganyiko wa gesi muhimu ya uhai; gesi hiyo inahifadhi kiwango cha nyuzi joto kinachowiana na uhai. Vile vile inachukua mvuke wa maji kutoka baharini na kuupeleka masafa ya mbali juu na hatimaye yanaanguka nakuwa mvua.

Lau kama upana wa ardhi ungelikuwa mdogo kuliko ulivyo sasa, ingel- ishindwa kuhifadhi uzani; na joto lingepanda kufikia mauti; na kama unge- likuwa ni mkubwa zaidi ya ulivyo ingelizidi mvutano wake, na ziada hiyo ingeliathiri maisha.

Vile vile, lau kama umbali wa ardhi na jua ungelipungua kuliko ulivyo hivi sasa, kiasi cha joto kingelipungua, na kama ardhi ingelikurubia zaidi jua kuliko ilivyo hivi sasa, basi joto lingezidi. Katika hali zote mbili maisha yangelikuwa magumu juu ya ardhi. Kwa hivyo mduara wa ardhi, na kipimo cha sehemu wazi zinazoizunguuka, mzunguuko wake pembeni mwa jua, kuzunguukwa na mfuniko anga, kuwa mahali maalum na kuwa upana wake ni kiasi maalum, yote hayo yanaandaa sababu za kupata uhai wa mtu juu ya ardhi. Lau ingekosekana moja ya sifa hizi; kwa mfano upana wake kuwa mdogo au mkubwa, au kuwa mbali au karibu na jua au kukosa mfuniko anga, ingelikuwa vigumu mtu kuwa ni wa duniani, kwa ushahidi wa wataalamu.

Ni jambo lisiloingia akilini kuwa utaratibu huu uwe umepatikana kibahati tu. Bali yote hayo ni kwa hekima ya Mwenye hekima na mazingatio ya Mwenye kuzingatia.

Kuwapo Mungu

Katika kufasiri Aya ya 21 na 22 za Sura hii, tumetaja dalili za kuwapo Mpangaji mambo, Mwenye hekima. Miongoni mwa dalili hizo ni dalili ya kufikia kikomo, na kwamba mpangilio wa ndani uliofanywa kwa hekima kati ya mbingu na ardhi hauwezekani kuwa umepatikana kwa sadfa (kibahati) tu!

Wala hakuna tafsiri yenye kukinaisha isipokuwa kuwapo Muweza, Mwenye hekima. Qur’an imetegemea dalili hii na ikaionyesha katika Aya nyingi, kama vile Aya hii tuliyonayo.

Kwa kunasibiana kwake, tunarudia kutoa dalili ya kuwapo Mwenyezi Mungu, lakini kwa mfumo mwingine sio ule tuliofuata wakati wa kufasiri Aya ya 21. Kabla ya kitu chochote kwanza tunatanguliza haya yafuatayo:

Wamaada wameamua sababu ya elimu na maarifa ni kuona na kujaribu tu. Kila linaloaminika ni lazima kupitia majaribio, kila linaloitakidiwa kwa njia nyingine isiyokuwa na majaribio basi hawaliiti kuwa ni elimu bali ni itikadi. Kwa hiyo elimu na itakidi - katika istihali yao - ni vitu viwili tofauti katika matokeo yake. Mtu akipata msaada wa majaribio kwa kusihi yale anayoyaitakidi, basi yanakuwa yale yanayoitakidiwa ni elimu.

Kwa msingi wao huo, kunakuwa kuamini kuwapo Mwenyezi Mungu ni itikadi si elimu. Nasi tunawaambia: Lakini vile vile kuamini kutokuwapo Mungu pia ni itikadi si elimu, kwa sababu pia hakutegemei majaribio. Kwa hiyo itikadi zimekutana. Kwa maneno mengine, ni kwamba, kila yanayoambatana na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ikiwa ni kukubali au kupinga, basi ni katika mambo ya ghaibu (yaliyojificha). Ikiwa mwenye kuamini kuwapo Mungu anaamini ghaibu bila ya majaribio, vile vile mwenye kukanusha hategemei majaribio, bali hutegemea ghaibu. Kwa hiyo wote ni sawa.

Baada ya utangulizi huu tutaonyesha kauli ya wakanushaji - Wamaada, na tutaonyesha kauli ya wenye kuamini Mungu kisha tumwachie msomaji ajichagulie.

Wakanushaji wanasema: Kupatikana ulimwengu na yaliyomo ndani yake, miongoni mwa nidhamu, mtu, pamoja na hisia zake na akili, yote hayo hayategemei udhibiti wowote isipokuwa yamepatikana kibahati (sadfa). Kwa hiyo ulimwengu ulipatikana kibahati, kisha ukapatikana mpango kibahati na kila kitu kimechukua mahali pake panapostahili kwa kibahati tu; na maada ndiyo iliyopatisha uhai na akili. Kwa maneno mengine, ni kwamba maada pofu ndiyo Mungu inayoweza kila kitu, lakini imepata uwezo hekima na kupangilia mambo kwa njia ya kibahati.

Ama wanaoamini kuwapo Mwenyezi Mungu wanasema: Ulimwengu na nidhamu yake, umepatikana kwa makusudio na kwa hekima, na mpangilio kutoka kwa Mola Muweza na Mwenye hekima.

Sasa msomaji jiulize swali hili: Ni nini chanzo cha ulimwengu, utaratibu na mipangilio? Je chanzo chake ni sadfa kama wasemavyo Walahidi? Au ni kwa makusudio na mipangilio, kama wasemavyo Waumini?

Jiulize swali hili kisha ujijibu kwa akili yako. Ama Voltaire amelijibu swali hili kwa kusema: “Fikra ya kuwapo Mwenyezi Mungu ni dharura, kwa sababu fikra ya kupinga ni upumbavu.”

Upi Uliotangulia: Usiku Au Mchana?

Wataalamu wamehitalifiana kuwa je mwangaza umetangulia giza au giza ndilo lililotangulia mwangaza katika kupatikana? Wengine wanasema mchana ndio uliotangulia usiku kwa hiyo usiku wa siku ni ule unaokuja baada ya mchana.

Wengine wamesema usiku ndio uliotangulia mchana kwa hiyo usiku unakuwa ni usiku wa mchana utakaokuja. Watu wa kwanza walipendelea kauli hii; kwa hiyo usiku wa Ijumaa kwao ni ule usiku unaokuwa kabla ya alfajiri ya ijumaa na masiku mengine yote. Katika waliyoyatolea dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَآيَةٌ لَهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ{37}


“Nausikuniisharakwao;tunauvuahumomchana...” (36:37).

وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِلَّهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ {165}


Nakatikawatukunawanaofanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini wale walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu sana. Na lauwaliodhulumu wangejua watakapoiona adhabu kwamba nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungunimkaliwakuadhibu.

إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ {166}


Pindi waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali yakuwa wamekwisha


ion


a


adhab


u


na yatawakatiki


a


mafunga


mano.

وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ {167}


W


atasemawalewaliofuata: ‘Lau kama tungeweza kurudi nasi tukawakataa kama walivyotukataa.’ Hivindivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto juu yao; wala hawatakuwa wenye kutoka motoni