read

Aya 165-167: Wanafanya Waungu Asiyekuwa Mwenyezi Mungu

Maana

Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu”.

Yaani kuna baadhi ya watu wanamshirikisha Mwenyezi Mungu kwa sababu wao wamemfanya kuwa na mshirika katika baadhi ya mambo anayohusikana nayo; kama vile kunufaisha na kudhuru. Imam Baqir (a.s.) amesema: “Waungu ambao wamewafanya na kuwapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu ni maimamu wa dhuluma na wafuasi wao.”

Imesemwa kuwa maana ya kumpenda Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni kumpenda kwa ukamilifu, kwa sababu Yeye ni ukamilifu mtupu. Imesemwa pia: ‘Ni kujua utukufu wake, uweza wake na hekima yake.’ Na imesemwa: ‘Ni kumwamini Mwenyezi Mungu kuwa Yeye ndiye mwanzilishi na mwenye kurejesha, na kwamba kila kitu kiko chini ya mamlaka yake’.

Sisi tuko kwenye njia ambayo tunakwenda nayo - kuchagua maana yenye kuafikiana ambayo yako wazi na yaliyo rahisi kufahamika. Kwa misingi hiyo tunasema: Anayempenda Mwenyezi Mungu ni yule asiyefuata matamanio yake na akamtii Mola wake; kama alivyosema Imam Sadiq (a.s.) katika kumwelezea ambaye dini itachukuliwa kutoka kwake.
Kwa maneno mengine, kumpenda kwako Mwenyezi Mungu ni kuacha unayoyataka wewe na kufanya anayoyataka Yeye; kama ambavyo maana ya kumpenda Mtume (s.a.w.w) ni kufanya kulingana na Sunna yake.

Ama Mwenyezi Mungu kumpenda mja wake ni kumlipa thawabu. Imekuja Hadith inayosema: “Nitampa bendera kesho mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na anayependwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Yaani Ali anamtii Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atamlipa thawabu na Mtume anamtukuza na kumtanguliza Kwa hiyo basi, kila anayemtii kiumbe, huyo amefanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, atake asitake.

Lakini wale walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu sana.

Kwa sababu wao hawamshirikishi na yeyote katika twaa na humtegemea. Ama wale wasioamini wanawategema waungu wengi na wanamshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu katika twaa kutaka heri na kujikinga na shari.

Na lau waliodhulumu (nafsi zao) wangejua watakapoiona adhabu kwamba nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu.

Yaani lau washirikina ambao wamezidhulumu nafsi zao wanajua kwamba hakuna mwenye usultani katika siku ya haki na ya kupambanuliwa hukumu, isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye peke Yake ndiye Mwenye mamlaka ya kuwaadhibu waasi na kuwalipa mema watiifu, lau wangelijua hivyo, basi wangelikuwa na yakini kwamba atakayekuwa peke yake kesho katika kuendesha mambo ya akhera ndiye huyo huyo aliyepanga ulimwengu huu. Kwa hivyo jawabu la lau limeondolewa, linafahamika kutokana na mpangilio wa maneno.

Pindi waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu na kuwakatikia mafungamano.

Maneno bado yanaendelea kwa wale wanaofanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu; wao ndio wanaoongozwa na ni wafuasi, na waungu ndio viongozi. Kesho pazia litakapofunguka, kiongozi atamkataa mfuasi wake kutokana na shida ya adhabu itakayotokea, na uhusiano kwao utakatika. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Zitaondoka zile sababu zote ambazo zinafungamanisha mapenzi, udugu, cheo mikataba ya umoja, n.k. na hilo ni mwisho wa kukata tamaa.”

Aya hii inafanana na Aya inayosema:

قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِكُمْ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ فِي النَّارِ ۖ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَعَنَتْ أُخْتَهَا ۖ حَتَّىٰ إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَٰؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِنَ النَّارِ ۖ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَٰكِنْ لَا تَعْلَمُونَ {38}


“...Kila umma utakapoingia utawalaani wenzake, mpaka watakapoku- sanyikawotehumo,wanyumawaowatawasema wakwanzawao:“Mola wetu! Hawandiowaliotupoteza;basiwapeadhabuyamotomaradufu! Atasema: ‘Itakuwa kwenu nyote (adhabu) maradufu, lakini nyinyi hamjui tu’.” (7:38).

Na watasema wale waliofuata: ‘Lau kama tungeweza kurudi nasi tukawakataa kama wanavyotukataa’.

Kesho atatamani kila muasi arudi duniani kutengeneza yale aliyokuwa ameyaharibu, hasa wafuasi wa watu wapotevu. Na hakuna kitu kilicho mbali zaidi ya matamanio haya, bali ni majuto yanayoichoma nafsi, sawa na moto unavyochoma mwili. Majuto hayo ni matunda ya kufuata matamanio na kupetuka mipaka.

Dhahiri ya tamko la Aya inafahamisha kwamba inahusika na makafiri, laki- ni kwa mujibu wa sababu ya hukumu, inamhusu kila mwenye kufuata na kusaidia dhuluma na ufisadi, na kila mwenye kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kunufaisha na kudhuru.

Vile vile mwenye kuchukua dini yake kutoka kwa wasio jua na wapotevu. Kwa hakika Aya hii inawahusu wote; hata mwenye kutamka shahada mbili, akaswali na kutoa zaka; isipokuwa asiyejua ambaye hakuzembea katika kujua uhakika wa mambo na kujua mambo yanayoweza kujulikana na akili yoyote iliyo timamu.

Taqlid Na Maimamu Wanne

Yamekuja maelezo katika tafsiri ya Al-Manar kwa kunakiliwa kutoka kwa Sheikh Muhammad Abduh kwamba, Maimamu wane: Abu Hanifa, Malik, Shafi na Bin Hambal wamekataza kufuatwa na kuchukuliwa kauli zao, na kwamba wao wanaamrisha ziachwe kauli zao na kifuatwe Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake. Baada ya kunakili kauli ya kila Imam katika hilo, akasema: “Lakini Karkhi - mmoja wa mafakihi wa Kihanafi - anasema wazi kwamba asili ni kauli ya Abu Hanifa. Kama Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake zitaafikiana na kauli ya Hanafi ni sawa; na kama si hivyo, basi ni lazima kauli ya Mwenyezi Mungu au Hadith ifanyiwe taawili ili iweze kuafikiana na kauli ya Abu Hanifa.”

Maana yake ni kuwa kauli ya Abu Hanifa ndiyo inayohukumu na kuitan- gulia Qur’an na Hadith. Kauli hii kwa dhati yake ni kufru. Kuna kufru gani kubwa zaidi kuliko kuiacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa sababu ya kauli ya Abu Hanifa na wafuasi wake? Je, kuna tofauti gani kati ya mwenye kusema haya na wale waliotajwa na Mwenyezi Mungu aliposema:

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ {170}


“Na wanapoambiwa; Fuateni aliyoyateremsha MwenyeziMunguhusema;“balitunafuatayaletuliyowakutanayobabazetu...”(2:170).

Tutafafanua kwa upana zaidi suala la taqlid katika kufasiri Aya ya 170 ya
Sura hii Inshaallah.

Kwa hiyo kufanya amali kwa kutegemea kauli za Maimamu wane ni kufanya amali bila ya ijitihadi wala taqlid, kwa sababu hao wane wamekataza kufuatwa.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ {168}


Enyiwatu!Kulenivilivyomo ardhini halali na vizuri, wala


msifuat


e


nyay


o


z


a


shetani.


Hakika yeye kwenu ni adui aliyedhahiri.

إِنَّمَا يَأْمُرُكُمْ بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَنْ تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ {169}


Hakikayeyeanawaamrisha


t


u


maov


u


n


a


machafu


,


na


kusem


a


ju


u


y


a


Mwenyezi


Mungumsiyoyajua.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ {170}


Nawanapoambiwa:Fuateni


aliyoyate


r


emsh


a


Mwenyezi


Mungu; husema: Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.’ Je, hata kama baba zao walikuwa hawafa


ham


u


chochot


e


wala


hawakuongoka?