read

Aya 168 -170: Kuleni Vilivyomo Katika Ardhi

Lugha

Halali ni kila ambalo halikuthibiti kukatazwa katika sharia; na haramu ni lile lililothibiti kukatazwa. Makusudio ya uzuri hapa ni lile ambalo linapendelewa na nafsi na kuburudika nalo kwa sharti ya kutokuwa ni lenye kukatazwa. Na ovu ni lile ambalo mwisho wake ni uovu.

Enyi watu! Kuleni vilivyomo ardhini halali na vizuri.

Msemo huu unawahusu watu wote; ni sawa awe mtu amejiharamishia mwenyewe baadhi ya vyakula au asiyejiharamisha; ni sawa awe ni Mumin au kafiri. Kwa sababu kafiri atazuiliwa neema za akhera tu sio starehe za dunia. Kuna Hadith Qudsi isemayo: “Mimi ninaumba na anaabudiwa mwingine na ninaruzuku na anashukuriwa mwingine.”

Katika vyakula kuna vya halali na haramu. Kula ambacho hakikukatazwa na sharia ni halali. Hadith inasema: “Hakika Mwenyezi Mungu amenyamazia vitu sio kwa kusahau. Kwa hivyo msijikalifishe navyo; ni rehema kwenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Mara nyingine uharamu unaotokana na sababu iliyozuka; kama vile mali iliyochukuliwa kwa riba, utapeli, rushwa au wizi.

Wala msifuate nyao za shetani. Hakika yeye kwenu ni adui aliye dhahiri.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuhalalishia watu halali anawahadharisha kuifanya haramu. Ibara ya tahadhari hii ameileta kwa kukataza kumfuata shetani na tashwishi zake ambazo zinampambia mtu yale yasiyokuwa halali kwake na kila ambalo linamhadaa, ili afanye mambo ya haramu; kama vile kunywa pombe, zinaa, uongo na ria. Au kumhadharisha kufanya wajibu; kama vile kutia hofu ya ufakiri ikiwa mtu atatekeleza haki aliyonayo kwa kutoa mali au madhara ikiwa atafanya jihadi au kusema haki. Yote hayo ni katika mawazo ya shetani. Mwenyezi Mungu ameuelezea usemi wa shetani aliposema:

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ {119}


“Nakwahakikanitawapotezananitawatiatamaa...”(4:


1


19).

قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ {16}

ثُمَّ لَآتِيَنَّهُمْ مِنْ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَنْ شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ {17}


“...Basi nitawavizia (waja wako) katika njia yako iliyonyooka kisha nitawafikiambeleyaonanyumayaonakuumenikwaonakushotonikwao;


weng


i


katik


a


wa


o


hutawakut


a


weny


e


kushukuru.”


(7:16-17).

Hakika yeye anawaamrisha mambo mabaya na machafu, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.

Huu ni ubainifu wa athari na natija zinazotokana na kufuata mwito na nyayo za shetani, nazo ni tatu: Kwanza, ubaya ambao ni kila kitendo ambacho mwisho wake ni ubaya. Pili, uchafu nao ni aina mbaya ya maasi. Tatu, kumsingizia Mwenyezi Mungu msiyoyajua kwamba yeye ana washirika na watoto, kuhalalisha haramu, na kuharamisha halali. Vile vile kufanya amali kwa kukisia na kupendelea katika kutoa hukumu ya sharia.

Na wanapoambiwa! Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu husema: Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.

Dhamiri ya wanapoambiwa inamrudia kila anayefuata mwingine bila ya hoja wala dalili, na kuacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume, kwa sababu ya kauli ya mababa. Makusudio ya aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ni kila yale yaliyo na dalili na hoja na yakaingia katika akili zilizo timamu.

Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?

Yaani wanafuata baba zao hata kama hawafahamu chochote katika mambo ya dini. Makusudio sio kukanusha kufahamu kila kitu, ijapokuwa kwa dhahiri Aya hii inaonyesha hivyo. Bali makusudio ni kukanusha kufahamu, kwa vile maneno yanahusikia na mambo ya kidini.

Tutaonyesha katika kifungu kifuatacho kwamba Aya hii inafahamisha ubaya wa kufuata mambo ya upotevu. Ama kufuata ya uongofu, hilo ni katika kufuata mwendo mzuri.

Kufuata Na Msingi Wa Itikadi

Kufuata (Taqlid) kulivyo hasa si kuzuri wala si kubaya kwa ujumla, bali kunatofautiana kwa aina zake zifuatazo:

1. Kufuata mkumbo, ambako kwa binadamu na wanyama ni sawa sawa; kama vile kuwika kwa jogoo anapomsikia mwenzake amewika na kulia kwa punda anapomsikia mwenzake. Hali kadhalika kwa upande wa binadamu, mmoja anaweza kupiga kofi kwa ajili ya hotuba, basi wengine wote wanaigiza bila ya kutambua, hata kama hawakufahamu kitu katika yaliyosemwa. Au mtu anaweza kuangalia upande fulani basi kila anayemuona naye huangalia huko bila ya kukusudia. Huku ndiko kufuata ambako si kuzuri wala kubaya. Kwa sababu kuko nje ya hisia na matakwa.

2. Kufuata mitindo na desturi fulani ya jamii; kama vile namna ya mavazi na mengineyo katika mambo ya jamii ambayo yamefanywa na wakubwa na wadogo, na wajuzi na wasiokuwa wajuzi. Hii ni katika aina ya kufuata ambako kunaweza kuwa kuzuri au kubaya kulingana na mtazamo wa watu.

3. Asiyejua kumfuata mtaalam katika mambo ya kidunia; kama vile utabibu, uhandisi, kilimo, ufundi, n.k. Huku ni kufuata kuzuri bali ni muhimu sana katika ustawi wa jamii. Lau kama si hivyo, basi utaratibu ungeharibika na kazi zingelisimama. Kwani mtu hawezi kujua kila kitu na kupata kilaanayoyahitajia peke yake. Mtu alikuwa na ataendelea kuwa na haja ya kusaidiana na kubadilishana huduma.

4. Mujtahid kumfuata mujtahid mwenzake katika mambo ya kidini. Huku kunakataliwa na akili na ni haramu kisharia. Kwa sababu, aliyoyajua ni hukumu ya Mwenyezi Mungu katika haki yake, haijuzu kuyaacha kwa sababu ya kauli ya mtu mwingine. Na ni mjuzi gani anayeacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake aliye Masum na kutegemea kauli ya anayekosea?

5. Asiye na elimu kumfuata mujtahid mwadilifu katika masuala tanzu ya kidini, kama vile hukumu za ibada, halali na haramu, twahara, najisi na kusihi muamala, n.k. Kufuata huku ni wajibu kisheria, kwa sababu ni kumfuata aliyechukua ujuzi wake kutokana na hoja na dalili; sawa na mgonjwa kumfuata daktari. Asiyejua anakalifiwa na hukumu, na haku- na njia ya kuzifuata isipokuwa kumrudia mjuzi.

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ {43}


“...Basiwaulizeniwenyekumbukumbu(wajuzi)ikiwanyinyihamjui.” (16:43).

Hata hivyo, asiyejua akiswali na kufunga kwa kufuata baba zake na mfano wao, sio kwa kufuata mujtahid mwadilifu, na ibada zake zikaafikiana na fat-wa za mujtahid, hizo zitakuwa sahihi na kukubaliwa. Kwa sababu kufuata (taqlid) si sehemu wala sharti la yanayoamrishwa, isipokuwa ni nyezo tu ya kufikilia kwenye amri. Hata inaweza kusihi maamiliano yake kama yakiwa ni sawa sawa.

Kuhusu kauli ya anayesema kuwa ibada inahitajia nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kwamba nia hiyo haithibitiki ila kutokana na mujtahid au mwenye kumfuata, kauli hiyo ni madai tu. Kwa sababu, maana ya nia ya kujikurubisha ni kutekeleza yaliyoamriwa kwa nia safi yenye kutakata na kila uchafu wa kidunia. Hapana mwenye kutia shaka kwamba hayo yanaweza kupatikana bila ya mujtahid. Kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “...Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala kuongoka?” Inafahamisha kuwa ikiwa baba alikuwa kwenye uongofu na akafuatwa na mtoto, itasihi.

6. Kufuata katika misingi (itikadi) ya dini kama kumjua Mwenyezi Mungu na sifa Zake, Utume wa Muhammad isma yake na ufufuo. Wanavyuoni wengi wa Kisunni na Kishia wameikataza aina hii ya kufuata, wakasema kuwa haijuzu (haifai). Kwa sababu kufuata (taqlid) huko ni kufuata bila ya dalili.

Na huo ndio ujinga hasa; yaani mwenye kusema juu ya kuweko Mwenyezi Mungu kwa kufuata tu, ni sawa na mwenye kusema Mungu hayuko. Wanavyuoni hawa wamesema: “Tumejuzisha kufuata katika matawi ya dini na masuala ya kuamiliana, lakini sio katika misingi ya kiitikadi. Kwa sababu linalotakiwa katika matawi ni amali tu kwa kufuata kauli ya mujtahid, jambo ambalo linawezekana, lakini kwa misingi ya kiitikadi, linalotakikana ni elimu na itikadi.”

Wahakiki katika Sunni na Shia wamesema kuwa kufuata kukiafikiana na uhakika ulivyo ni sahihi, kwa sababu hilo ndilo linalotakikana; na ijtahidi sio sharti wala fungu la imani na kusadikisha, isipokuwa ni njia tu.

Hii ni kweli kabisa, kwa sababu linalozingatiwa katika misingi ya itikadi ni imani sahihi yenye kuafiki. Kwa ajili hii ndio Mtume (s.a.w.w) akakubali Uislamu wa kila mwenye kuuamini na ikatulia nafsi yake kwa ukweli wake na Utume wake bila ya kufanya ijtahidi na kuangalia. Ama Aya zilizokuja kukemea wanaofuata mababa, mfumo wake unafahamisha kuwa makusudio ni kufuata batili na upotevu, sio haki na uongofu. Hakika hii inadhihiri kwa kila mwenye kufikiria kwa undani maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ {104}


“Na wanapoambiwa: Njooni katika hukumu alizoteremsha Mwenyezi Munguna(anazozisema)Mtume’husema:
Y


anatutoshayaletuliyowakutanayobabazetu’...”(5:104).

أَوَلَوْ جِئْتُكُمْ بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدْتُمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ {24}


“Hata kama nawaleteayenye mwongozo bora kuliko mliyowakuta nayo babazenu.”(43:24).

أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ {170}


“Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochotewala kuongo- ka?”(2:170).

Ufahamisho wa Aya zote hizi ni kwamba, kama mababa zao wangelikuwa na desturi yenye uongofu ambao umeteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume, basi ingelifaaa kuwafuata mababa hao. Kwa sababu linalotakiwa ni kufuata aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu! Wakiyafuata, basi wamefuata amri na wametii, na hawataulizwa kitu kingine baada ya twaa.

Kwa ufupi ni kwamba kila anyefuata kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume, atakuwa amefuata haki yenye kuthibiti kwa dalili, ni sawa awe amejua dalili hiyo au la. Inatosha kujua kwa jumla kwamba kuna dalili sahihi waliyoifuata wahusika wanaofanya ijtihadi. Bali mwenye kufuata haki bila ya kuijua kwamba hiyo ni haki, hataadhibiwa kwa kuacha kujifundisha hata kama hastahiki thawabu na kusifiwa. Hayo yanafahamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

وَإِنْ جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَنْ تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ {15}


“Na (wazazi wako) wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo,usiwatii...” (31:15).

Hiyo vile vile inafahamisha kuwa wakikushurutisha kumwamini Mwenyezi Mungu na ukawatii bila ya kuwa na elimu nayo, basi hapana ubaya kwako.

Tumefafanua kuhusu kuwafuata (taqlid) Maimamu wane katika kufasiri Aya ya 167 ya sura hii, mwenye kutaka na arudie.

وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ {171}


Namfanowawalewalioku-


furu


,


n


i


kam


a


mfan


o


wa


anayempigia kelele asiyesikia ila wito nasauti tu; ni viziwi, mabubu, vipofu kwa hivyo hawafahamu.