read

Aya 172-173: Kuleni Vizuri

Maana

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwaambia watu wote kwa kauli yake “kuleni vilivyomo ardhini” amerudia kusema tena, lakini akiwahusisha waumini: “Enyi mlioamini! kuleni vizuri tulivyowaruzuku.”

Ili awabainishie kwamba imani sahihi sio kujizuia na vitu vizuri, kama wanavyofanya baadhi ya watawa, makasisi na wengineo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametuhalalishia kustarehe na maisha na neema za kimwili na akatuamrisha kuzishukuru; na maana ya kuzishukuru ni kuzitumia katika njia inayotakikana.

Amirul Muminin Ali (a.s.) anasema: “Uchache zaidi wa yanayowalazimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kutozitumia neema zake kwa kumwasi.” Huenda wale wenye jaha na utajiri, wakapata onyo kutokana na hekima hii iliyo fasaha ili wasizame katika anasa iliyoharamishwa na kuwa na kiburi na kupetuka mipaka.
Hakika ameharamshia mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilisomewa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Hakuna mwenye shaka kwamba makusudio ya uharamu hapa ni uharamu wa kitendo ambacho ni kula sio uharamu wa kitu chenyewe. Kwani kitu hakiwezi kutajwa kwa uhalali na uharamu.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja , katika Aya iliyotangulia, uhalali wa vinavyoliwa, hapa anatupa aina nne ya vilivyo haramu kuliwa:

1. Mfu: Ni kila mnyama aliyekufa bila ya kuchinjwa kisheria.

2. Damu: Makusudio ni damu iliyojitenga na nyama, kwa sababu iliyo pamoja na nyama inasamehewa.

3. Nguruwe: Nyama yake, mafuta yake na mwili wake wote, kinyume na anavyosema Daud Dhahiri aliposema: “Ni haramu nyama ya nguruwe tu, sio mafuta yake,” kwa kuchukulia dhahiri ya tamko, eti Aya imetaja nyama tu. Ilivyo ni kwamba imetajwa nyama kwa sababu ndio inayotumika zaidi.

4. Kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu: yule aliyetajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni sawa kuchinjwa kwa ajili ya masanamu matambiko, mazindiko au vitu vingine.

Hekima ya kuharamishwa aina tatu za kwanza ni kiafya ambayo watabibu wanaijua. Ama hekima ya kuzuia kile kilichotajiwa aisyekuwa Mwenyezi Mungu, ni ya kidini yenye lengo la kuchunga Tawhid na kumwepusha Mwenyezi Mungu na ushirikina.

Kwa ujumla ni kuwa ni wajibu kumtaja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wakati wa kuchinja. Mwenye kuacha kufanya hivyo kwa makusudi, basi alichokichinja ni haramu, ni sawa iwe aliacha kwa kujua au kutojua. Ama akiacha kwa kusahau, basi haiwi haramu. Inatosha kutaja Allahu Akbar au Al- hamdulillah au Bismillah au Lailaha illa Ilahu, n.k. Ufafanuzi zaidi unaweza kuupata katika vitabu vyetu vya Fiqh; kama vile kitabu chetu cha Fiqh Imam Jaffar Sadiq (a.s.)

Unaweza kuuliza; Dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba hakukuharamishwa isipokuwa aina hizi nne tu za vyakula, kwa sababu neno tu linafaahamisha mambo mawili:

• Kwanza: Kuthibitisha yale yanaelezwa ambayo hapa ni kuharamishwa vitu vinne.

• Pili: Kukanusha ambako hapa ni kutoharamishwa vitu vingine ispokuwa vitu hivi vine tu; na ilivyo ni kuwa kuna vyakula vingine vilivyoharamishwa; kama mbwa, wanyama wanoshambulia, wadudu, baadhi ya samaki. n.k.

Jibu: Ndio dhahiri ya Aya inafahamisha hivyo, lakini halitumiwi hilo baada ya kongamano la wanavyuoni na kuthibiti Hadith za Mtume. Hii siyo Aya pekee ambayo dhahiri yake imeachwa na kongamano la wanavyuoni kutokana na Hadith.

Mwenye Dharura Na Hukumu Yake

Basi aliyefikwa na dharura bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi.

Mwenye dharura ni yule ambaye anahofia nafsi yake kufa ikiwa hatakula kitu cha haramu, anayehofia kuzuka maradhi au kuzidi maradhi, kuhofia madhara na adha juu ya nafsi nyingine yenye kuheshimiwa; kama vile mwenye mimba kuogopea mimba yake au mwenye kunyonyesha kumhofia mwanawe; au mwenye kulazimishwa kwa nguvu kula au kunywa kitu cha haramu, kwa namna ambayo kama hakufanya hivyo atapata adha ya nafsi yake au mali yake au utu wake.

Yote haya na mifano yake ni katika mambo yaliyosamehewa katika kutumia kitu cha haramu, lakini kwa kiasi kile tu kinachoweza kuondoa madhara. Kuanzia hapo ukawa mashuhuri msemo wa mafaqihi: “Dharura hupimwa kwa kiasi chake”. Hilo linafamishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Basi aliyefikwa na dharura bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi.” Mwenye kutamani ni yule anayefanya haramu bila ya dharura, na mwenye kupitisha kiasi ni yule anayepitisha kiasi cha haja.

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ أُولَٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ {174}


Hakikawalewafichaoaliyoyate


r


emsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto: wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha siku ya Kiyama, wala hatawatakasa; nawaowanaadhabuchungu.

أُولَٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ {175}


Haondiowalionunuaupotevu kwa uongofu, na adhabu kwa maghufira.BasiniujasiriuliojewakuvumiliaMoto?

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ {176}


Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amete


r


emsha Kitabu kwa haki, na wale waliohitalifiana katika Kitabu (hiki) wamo katika upinzaniuliombali.